Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Ukiachilia mbali mkataba wa bandari ambao Serikali imesaini kuwapa bure waarabu wa Dubai bandari zote za Tanganyika za bahari na maziwa makuu, kumbe pia;
1. Inadaiwa serikali imeingia na kusaini mkataba wa kuwapa waarabu hawahawa hekta za misitu ya Tanganyika milioni 8 eti watusaidie kutunza. Na mkataba huo haukupita bungeni kama ambavyo sheria ya ulinzi wa rasrimali asili zetu ya mwaka 2017 inavyotaka..
Je, hili nalo ni la kweli Rais Samia?
2. Inadaiwa Serikali imesaini mkataba wa kuwamilikisha Waarabu hawahawa tena hifadhi za Ngorongoro na Loliondo Kwa namna na mtindo ule ule na ndiyo maana huko Kuna mgogoro mkubwa kati ya serikali vs wananchi vs mwaarabu huyo..
Je, hili nalo ni la kweli Rais Samia.?
3. Kwa mtindo ule ule wa kinyemela, inadaiwa Serikali inammilikisha mzungu mmoja wa Kimarekani aliyefadhili sinema ya Royal Tours ekari 6,000,000 ndani ya hifadhi za taifa.
Rais Samia, hili nalo likoje? Utakaa kimya mpaka lini? Na ili iweje ukiamua kukaa kimya?