Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kuna kila dalili na ishara kwamba minyukano inayoendelea ndani ya CHADEMA imeratibiwa na kupenyezwa kwa mbinu za siri ili kukivuruga chama hiki ambacho kimsingi ndicho chama kikuu cha upinzani. Baada ya hali ya chama tawala kuonekana tete kuelekea uchaguzi mkuu 2025 hususan baada ya dalili zote kuonesha kutokukubalika kwa mgombea mtarajiwa. Uimara wa chama cha upinzani ni hatari kwa mstakabali wa CCM hivyo kila mbinu zinatumika ili kuudhoofisha upinzani.
Kama ni uchaguzi wa ndani ya chama ambao upo kikatiba, Hapakuwa na haja ya kurushiana maneno hadharani unless kama kuna malengo na drama fulani ambazo hatuzifahamu (kuonyesha kwamba uchaguzi ulikuwa mkali kumbe matokeo wanayajua wao)
Anyways, Tukiyaacha hayo yote, huu ni mtazamo wangu kuhusu viongozi hawa wawili
1. FREEMAN MBOWE
SIFA NJEMA
(i) Ni mtu mwenye misimamo ila ni mwepesi kubadilika kulingana na upepo
(ii) Hekima na busara za uongozi hapa ndipo mahala pake. FAM ni kiongozi mwenye maamuzi ya utulivu yasiyo na ukurupukaji.
(iii) Diplomasia za kisiasa. FAM anaijua vyema diplomasia ya kisiasa, anajua namna ya kushirikiana na taasisi, mashirika na vyama vingine vya siasa katika kukijenga chama
(iv) Ubunifu na mikakati. FAM ni kiongozi mbunifu na fundi sana katika kupanga na kuweka mikakati ya chama pale inapohitajika.
SIFA HASI
(i) Misimamo inayoyumbishwa kirahisi. FAM ni kiongozi mwenye msimamo ila ni mwepesi kuyumbishwa kulingana na upepo unavyoenda.Si aina ya kiongozi mwenye misimamo ya kufa kupona.
(ii) Kiongozi asiyeweza kusoma alama za nyakati na kwenda kulingana na muda unavyomtaka.Si kila wakati upole ni suluhisho kwa mambo fulani, hususan kwa chama kikuu cha upinzani.
(iii) Si mwanaharakati, Si mpinzani wa kweli, Ni muumini wa maridhiano na siasa za kistaarabu, Jambo ambalo chama tawala anachokabiliana nacho sivyo walivyo.Anaambiwa vita ni ya fimbo kumbe mwenzake ameficha kisu na anakuwa mwepesi kukubali.Kulingana na alama za nyakati na zama za upinzani wa kisiasa uliopo aina hii ya uongozi ni irrelevant. Haswa baada ya chama tawala kuonyesha waziwazi nia ya dhati ya kutokutoka madarakani kamwe iwe kwa njia halali au isiyo halali, mfano kutokuwa tayari kufanya mabadiliko ya katiba mpya, tume huru ya uchaguzi nk.
(iv) Kukaa muda mrefu madarakani, Kuishiwa mbinu na mikakati mipya ya kuongoza chama, Kushindwa kuwafikia na kushawishi wananchi wa chini katika ngazi za vijiji,kata,vitongoji nk. Kushindwa kuweka misingi ya upinzani katika ngazi za chini na kuconnect na watanzania wa hali ya chini inaonyesha CHADEMA kukosa nia ya dhati ya kuwa chama tawala.
2.TUNDU LISSU
SIFA NJEMA
(i) Ni kiongozi mwenye misimamo.Anamaanisha kile anachokisema, si mwepesi kushawishika,Amenyooka kama ruler, Nadhani baada ya Dr.Slaa, TAL anafuata kwa misimamo.
(ii) Ni mpinzani na mwanaharakati wa kweli, hivyo ana uwezo mkubwa wa kushawishi na ku mobilize watu
(iii) Relevant kwa mahitaji ya chama kwa wakati huu ambapo CHADEMA kimeonekana kupoa baada ya maridhiano yasiyokuwa na tija na baada ya chama tawala kuonyesha nia ya wazi ya kukataa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
(iv) Ujuzi na ufahamu wake mkubwa katika uwanda wa sheria ni nyongeza.
SIFA HASI
(i) Si kiongozi mwenye busara na hekima za kiuongozi na kiutawala. Kukosa utulivu wa kimaamuzi pasipo na kukurupuka kunaweza kukigharimu chama.
(ii) Si mwanasiasa mzuri, Ni mwanaharakati mzuri.
(iii) Si mzoefu katika diplomasia ya vyama vya kisiasa, mbinu sahihi za kujenga mahusiano na taasisi za kimataifa katika kukiendeleza chama hususan kiuchumi.
(iv) Uvumilivu wa kisiasa. TAL si mvumilivu wa kisiasa, mfano mzuri ni pale baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu wa 2020, baada ya hapo, TAL ni kama hajawa sawa tena, hata haya maamuzi ya kugombea uenyekiti ni kama ameamua liwalo na liwe.
Hayo ni machache kuhusu viongozi hawa wawili, Je, kwa mtazamo wako unadhani nani anafaakusimamishwa na CHADEMA kama
(i) Mwenyekiti wa chama
(ii) Mgombea urais 2025