Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kama viongozi wa umma waliowatandika watu viboko hadharani wanadhani suala hilo limeisha au kusahaulika, bila shaka watakuwa wanajidanganya.
Hii ni baada ya suala hilo kuibuka juzi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Sheria na Wakili Mwandamizi Anthony Nasimire aliyezungumza kwa niaba ya mawakili wa kujitegemea Mkoa wa Mwanza.
Akisoma hotuba yake yenye kurasa sita mbele ya mgeni rasmi, Dk Severine Lalika ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ilemela aliyemwakilisha mkuu wa mkoa, John Mongela, Nasimire alisema vitendo hivyo vya karibuni vya viongozi kuwatandika watu viboko hadharani vinakiuka katiba na sheria.
Wakili Nasimire ambaye ni miongoni mwa mawakili wakongwe na wenye uzoefu Kanda ya Ziwa, alisema kisheria ni mahakama pekee nyenye mamlaka ya kutoa adhabu baada ya mtuhumiwa kushtakiwa na kutiwa hatiani.
“Adhabu ya kupigwa viboko ni mojawapo ya adhabu ambazo mahakama inaweza kutoa endapo kosa aliloshtakiwa nalo mtu linahusu utoaji wake. Utekelezaji wa adhabu hiyo hufuata mwongozo uliotolewa chini ya sheria ya `The Corporal punishment Act’ sura ya 17 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019,” alisema wakili Nasimire
Akifafanua zaidi alisema “ni marufuku kwa mfano adhabu ya viboko kutolewa hadharani (kifungu cha 8(5)). Aidha viongozi wa umma hawana uhalali wowote kisheria kutoa adhabu ya kumpiga viboko au kutekeleza adhabu hiyo. Ni Mahakama pekee yenye mamlaka kisheria kutoa adhabu hiyo. Na wenye mamlaka kutekeleza adhabu hiyo ni watumishi wa Serikali walioruhusiwa kisheria.”
Mbele ya Jaji mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Sam Rumanyika, Wakili huyo alishauri wanaoathirika na vitendo vya viongozi wanaotumia vibaya madaraka yao kuitumia Mahakama Kuu kwa sababu ndicho chombo ambacho kimekuwa kikitumiwa na wadau mbalimbali kupata nafuu dhidi ya madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi wa umma waliopewa dhamana.
Pia Wakili wa kujitegemea jijini Mwanza, Majid Kangile aliunga mkono hoja ya Wakili huyo kwa kusema vitendo vya viongozi kutandika watu viboko hadharani vinakiuka Ibara ya 13 (6) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayomhesabu mtu kuwa na haki mbele ya sheria hadi pale kosa lake litakapothibitika mbele ya Mahakama.
“Kwa madhumuni ya kuhakikisha usawa mbele ya sheria, Mamlaka ya nchi itaweka taratibu zinazofaa au zinazozingatia misingi kwamba ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo inasema sehemu ya ibara hiyo ya katiba,” alieleza Kangile.
Akifafanua, Wakili Kangile alisema viongozi hao pia wanakiuka Ibara ya 4 (1) inayotoa mgawanyo wa madaraka kwa mamlaka za Serikali ikiwemo Utawala, Bunge na Mahakama.
“Shughuli zote za mamlaka ya nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vya kutunga na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma -- Bunge na Baraza la Wawakilishi.”
Chanzo: Mwananchi