Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 2,858
- 5,123
Kama hukuwahi kufahamu sababu ya kambi ya jeshi ya LUGALO, iliyopo jijini Dar es Salaam, kuitwa hivyo – basi leo nakufahamisha. Watu wengi huamini kuwa kambi hiyo ilipewa jina hilo tangu mwanzo, lakini si kweli. Jina la "LUGALO" lina chanzo chake ambacho si Dar es Salaam, bali ni sehemu maalumu iliyopo mkoani Iringa.
Wenyeji wa Iringa wanajua kuwa kuna eneo linaitwa Lugalo, lakini Dar es Salaam hakuna sehemu yenye jina hilo isipokuwa ndani ya hiyo kambi ya jeshi. Sasa, kwanini kambi hiyo ya jeshi iitwe Lugalo kama sehemu hiyo haipo Dar?
Kambi ya Jeshi ya Lugalo ni mojawapo ya kambi za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizopo jijini Dar es Salaam. Kambi hii ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Waingereza na awali iliitwa Tanganyika Kings African Rifles (TKAR), kama ilivyo kwa kambi nyingine nyingi za Waingereza barani Afrika zilizokuwa chini ya jina la Kings African Rifles.
Baadaye, kufikia tarehe 19 Mei 1941, kambi hiyo ilibadilishwa jina na kuitwa Colito Barracks, kutokana na ushindi wa kikosi cha TKAR katika vita dhidi ya Waitaliano huko eneo la Alaba Colito, nchini Ethiopia, wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Vita hivyo viliongozwa na jenerali wa kikosi hicho, ambaye aliheshimiwa kwa kutumia jina lake “Barracks” katika jina la kambi. Jina hili lililenga kuenzi ushindi huo mkubwa wa kikosi cha Tanganyika.
Hata hivyo, baada ya nchi kupata uhuru, Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alifanya juhudi kubwa za kuondoa majina ya kikoloni na kuyaweka majina ya kizalendo yenye historia ya nchi yetu. Moja ya mabadiliko hayo ilikuwa ni kubadilisha jina la kambi hiyo kutoka Colito Barracks na kuiita Lugalo, kama heshima kwa mapambano ya kihistoria yaliyotokea Lugalo, Iringa.
Lugalo ya Iringa ni sehemu muhimu kihistoria ambapo kulifanyika mapambano makubwa kati ya Wajerumani na wapiganaji wa kabila la Wahehe chini ya uongozi wa Chifu Mkwawa. Katika awamu ya kwanza ya vita hivyo, Wahehe walishinda na kumlazimisha kiongozi wa kijeshi wa Kijerumani, Schultztuppe, kukimbia. Baadaye, alirudi tena na baada ya mapambano makali, aliweza kupata ushindi kwa tabu sana.
Kwa kuenzi ushindi na ushujaa wa Wahehe dhidi ya wakoloni wa Kijerumani, Mwalimu Nyerere aliona ni vyema kubadili jina la kambi ya kijeshi ya Colito na kuiita Lugalo, ili kuenzi historia ya mapambano hayo. Vilevile, aliagiza kufutwa kwa majina mengine ya kikoloni, kama ilivyokuwa kwa klabu ya Sunderland ya Tanzania, ambayo baadaye iliitwa Simba SC.
Hivyo basi, jina la kambi ya Lugalo si la kubahatisha, bali ni sehemu ya historia ya mapambano ya ukombozi wa Watanzania dhidi ya wakoloni