Tetesi: Kama ulinunua kiwanja Dodoma jiji, soma hapa utanishukuru

Tetesi: Kama ulinunua kiwanja Dodoma jiji, soma hapa utanishukuru

Kitchener

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
13,833
Reaction score
27,753
Jiji la Dodoma wametangaza yeyote aliyegawiwa kiwanja, ndani ya muda halisi wa kuendeleza, usipoendeleza, wameanzisha kampeni ya kunyang'anya viwanja hivyo.

Wameweka tangazo tayai. Kuna watu wawili nawafahamu, walikuwa na karatasi za uhakiki na mikataba kuuziwa na wazawa, kilichotokea maafisa ardhi walipoona kiwanja kimevuka muda na hawaonekani,wamemgawia mtu mwingine.

Kama wewe ni mmojawapo, panda gari haraka, jenga walau msingi, au uza, muda si mrefu aidha utalia au utaanza kusota ardhi jiji.
 
Aisee! Me nilipiga fence kabisa afu nikasepa nakuja kurudi nakuta nimezungukwa na majengo tupu.
 
Wazanzibari wananunua Kwa WINGI sana Hivyo ambavyo watu wamechelewa kuviendeleza.wanadai wanaimarisha muungano.
 
Me ni mmoja ya wamendea hii fursa ya uvuvi wa Ardhi
 
kuna jamaa alinunua kwa wazawa, akabaki na karatasi asifuatilie hati, juzi kakuta watu wanamwaga mchanga na tofali, kuuliza kwanini wanataka kujenga kiwanja chake, jamaa kaja na hati kabisa amesaidiwa na maafisa ardhi, kwenda jiji wanamwambia ulitelekeza, ulitakiwa kuendeleza, tumempa mtu mwingine ndiye huyo anayekiendeleza. ameambiwa asubir hadi mgao mwingine maeneo mapya yatakapotangazwa apate mbadala, na definately hayo maeneo mapya yatakuwa bush huko pembeni kabisa ya mji, ambako nako huwa hakuna uhakika wa kugawiwa kwani wahitaji ni wengi.
 
Back
Top Bottom