Kama Ulishindwa kwa JK, Je kwa JPM utaweza?

Kama Ulishindwa kwa JK, Je kwa JPM utaweza?

kama ulishidwa kwa JK, je kwa JPM UTAWEZA?

1: Kama ulishindwa kupiga madili kwa JK, je kwa JPM utaweza?

2: Kama ulishindwa kuongea utakavyo kwa JK, je kwa JPM utaweza?

3: Kama ulishindwa kutoka nje ya nchi kwa JK, je kwa JPM utaweza?

4: Kama ulishindwa kujenga hata kibanda chako tu kwa JK, je kwa JPM utaweza?

5: Kama ulishindwa kutajirika kwa JK, je kwa JPM utaweza?

6: Kama ulishindwa kunywa chai kwa JK,je kwa JPM utaweza?

8: Kama ulishindwa kupata shavu kwa JK kupitia mjomba nanii, je kwa JPM utaweza?

9:kama ulishindwa kumtukana JK hata kupitia mitandao tu, je kwa JPM, utaweza?

10: Kama ulishindwa kufanya mikutano mingi ya kisiasa kwa JK, je kwa magufuli utaweza?

11: Kama ulishindwa kupata ajira kwa JK, je kwa JPM utaweza?

12: Kama ulishindwa kuangalia bunge live aliloliweka JK ,je kwa JPM utaweza?

13: Kama ulishindwa kufaulu kwa JK na maBRN yote yale pamoja na kurisit, Je kwa JPM utaweza?

14: Kama ulishindwa kumiliki mtoto mzuri(beib) na kuhonga kwa JK,je kwa JPM utaweza?

15: Kama hukutumia demokrasia na uhuru wako kwa JK, je Kwa JPM utaweza?

Nimechoka kuuliza....
Hebu nisaidieni yawezaekana mimi ni mtoto wa bibi lakini sijafaidika na shamba la bibi.

Hebu nisaidie maswali (ongezea) labda nita achiwa chochote
16_kama Lowasa hakupata Urais wakati JK anamaliza, je wakati huu wa TINGATINGA hadi 2020 atatoboa. Jibu ni ASAHAU
 
Ina maana katika utawala huu hatutajenga? Mkuu mbona unatukatisha tamaa hivi.Sasa kama hatutajenga jamaa ana msaada gani kwetu?
 
16_kama Lowasa hakupata Urais wakati JK anamaliza, je wakati huu wa TINGATINGA hadi 2020 atatoboa. Jibu ni ASAHAU
umetisha mkuu....! tunamsubiri nae lowasa kuhojiwa na polisi tu
 
Ina maana katika utawala huu hatutajenga? Mkuu mbona unatukatisha tamaa hivi.Sasa kama hatutajenga jamaa ana msaada gani kwetu?

rejea bajeti na kodi za bidhaaa zilivyopanda...!! h h h..basi jumlisha na ugumu wa upatikanaji pesa.ukipata jibu nipe mrejesho
 
Ok ni hivi Jahkaya anajua siasa za bongo ameanza kuzichezea akiwa chipukizi anajua kucheza na mass , hapendi kuropoka ropoka kwenye media huyu jamaa wa sasa.

Huyu Ni Kama alihamshwa usingizini na kuambiwa jiandae na safari ya urais ndiyo maana amejaa uwoga na kuona kila anaetoa maoni yake kikatiba anaonekana Kama unataka kufanya treason.

Sasa na zama hizi ambapo vyuo vikuu vipo karibia 70s huwezi uka apply tactics za mkapa ambaye alitawala vyuo vikuu vikiwa vitatu(citation needed) .

Again and again time will tell my nigga sisi huku tunasema. Tiden kommer att tala mitt nigga

Simfahamu sana, nataka unipe darsa tu ondoa shaka Mkuu najua Jk alikuwa mjanja mjanja pengine huo ubabe wengi hatuku notice
 
Bila shaka unaongelea watu waliokuwa na fikra za "kutoka" kupitia "shortcut"...ila kwa wale waliotarajia vya halali, watatoka
Labda wenye mshahara mnono. Sisi wa chini kuhalali hatupati hata hela ya vocha. Yaani hapa nilipo lazima nitumie 10000 kwa siku wakati mshahara wangu ni 240k. Jiulize kodi itakuaje
 
Liserikali la baba Je.sca, ha, ha, ha, ni udikteta mwanzo mwisho. Eti leo wanasema hakuna kuajiri wala hakuna nyongeza kwa watumishi, kisa, ni kutaka kuwabaini wafanyakazi hewa. Sasa sijui ule msako wa mwezi April ulikuwa wa nini!! Yaani huyu Ngosha hana utu kabisa. Vijimishahara vyenyewe vidogo, halafu mwaka unaisha bila hata nyongeza ya japo senti tano. Wafanyakazi si wataendelea kuishi maisha ya kinyama?
 
Ok ni hivi Jahkaya anajua siasa za bongo ameanza kuzichezea akiwa chipukizi anajua kucheza na mass , hapendi kuropoka ropoka kwenye media huyu jamaa wa sasa.

Huyu Ni Kama alihamshwa usingizini na kuambiwa jiandae na safari ya urais ndiyo maana amejaa uwoga na kuona kila anaetoa maoni yake kikatiba anaonekana Kama unataka kufanya treason.

Sasa na zama hizi ambapo vyuo vikuu vipo karibia 70s huwezi uka apply tactics za mkapa ambaye alitawala vyuo vikuu vikiwa vitatu(citation needed) .

Again and again time will tell my nigga sisi huku tunasema. Tiden kommer att tala mitt nigga
Nmekusoma sana Mkuu!

Tangu Zitto amshauri aige style ya Jk ya kuadimika kwa muda sio kila jambo kujibu naona kaadimika kwa muda
 
Jamaa hafai KULUMANGIA wala KUTAFUNIA....
Si Ubuyu si Ukwaju Chachu tupu......
Hasikii la MUADHINI wala MTEKA MAJI MSIKITINI......
NGOJA TUONE MWISHO WA HII MOVE ITAKUWAJE

Mna lenu jambo na kama tulivyokwisha waambia MTAISOMA NAMBA, mkitaka shavu mfuateni mjomba wenu Msoga sisi hapa ni kazi tu!!!
 
Wakati nipo shule siku headmaster akionekana assembly ground basi ujue Kuna kitu kikubwa kimetokea hadi watu wanaogopa . Enzi za Mkapa ukisikia wimbo wa Taifa unapigwa ujue jamaa anaongea mambo ya msingi sasa uncle ngosha daily kwenye kideo asee !

Nmekusoma sana Mkuu!

Tangu Zitto amshauri aige style ya Jk ya kuadimika kwa muda sio kila jambo kujibu naona kaadimika kwa muda
 
Liserikali la baba Je.sca, ha, ha, ha, ni udikteta mwanzo mwisho. Eti leo wanasema hakuna kuajiri wala hakuna nyongeza kwa watumishi, kisa, ni kutaka kuwabaini wafanyakazi hewa. Sasa sijui ule msako wa mwezi April ulikuwa wa nini!! Yaani huyu Ngosha hana utu kabisa. Vijimishahara vyenyewe vidogo, halafu mwaka unaisha bila hata nyongeza ya japo senti tano. Wafanyakazi si wataendelea kuishi maisha ya kinyama?
very true...! lakini wapo nje wanakusubiri ukahojiwe na polisi
 
Mambo ya inji hii ukiyafikiria sana unaweza jikuta pilato anakudai milioni saba na kama ni mdomo mtupu unajikuta kuzimu ya dunia
 
Kama wameweza kuiba kifaru ( sijui ni kweli?) , basi watatoboa....
 
Mna lenu jambo na kama tulivyokwisha waambia MTAISOMA NAMBA, mkitaka shavu mfuateni mjomba wenu Msoga sisi hapa ni kazi tu!!!
Uzuri ni kwamba mapigo haya twayapata wote.....na pengine mimi nina ahueni kuliko wewe.....
 
Back
Top Bottom