mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Kama ulisoma kidumu na ufagio, miaka ya 90s bila shaka uliwahi kukimbia mchaka mchaka ule wa asubuhi. Nakumbuka moja ya nyimbo zilizokuwa zikihamsha hamsha!
Kuna huu!
'Nelson Mandela, afunguliwe uhuru, katika jela ya makaburu' ......
Halafu kuna huu;
Jua lile literemke mamaa.....aiya ya ioooh ioh mama!
Na huu!
Idd Amin akifaaa, mimi siwezi kuliaaa
Nitamtupa Kageraaa, awe chakula cha mambaaaa! Teh!
Huo wimbo wa Idd Amini, nimeukumbuka muda huu wakati natafakari kipigo cha walemavu kutoka kwa jeshi letu pendwa la polisi. Ni aibu!
Mambo haya yalitokea pia wakati wa utawala wa Nduli Idd Amin Dada wa Uganda. Moja kati ya falsafa za Idd Amin ilikuwa kwamba, walemavu hawazalishi, kwamba wao wanategemea kwa sehemu kubwa wasio walemavu. Kwa hiyo hawachangii kukua kwa uchumi bali wao ni watumiaji tu, hawazalishi. Ni falsafa ya kijinga sana. Sio ubinadamu kabisa, ni unyama.
Kwa sababu ya falsafa hiyo, katika utawala wa Idd Amin Dada, walemavu na maadui wengine walisombwa kwenye malori na kutupwa katika mto wa Kagera ambao una mamba wengi.
Ndio maana tukawa tunaimba kuwa Idd Amin akifa, hatuwezi kulia bali na yeye tutamtupa Kagera. Awe chakula cha mamba.
Falsafa hiyo ya Idd Amin, haikuanzia Uganda. Ilianzia Ujerumani wakati wa utawala wa NAZI chini ya Adolf Hitler. Kwa hiyo unaweza kuona kuwa sio falsafa ya mtu mmoja aliyeaminika kuwa na ugonjwa wa zinaa ulioathiri ubongo, (Neurosyphilis) bali ni falsafa ya madikteta wengi.
"Kuna vilevi vya aina nyingi, pombe, marijuana, cocaine, heroine, nk hivi vyote vinaweza kuwa na tiba. Lakini ukilewa madaraka, hakuna daktari wa ubingwa wowote ataweza kukutibu".
Sent using Jamii Forums mobile app