Kama ulisoma kidumu na ufagio, miaka ya 90s bila shaka uliwahi kukimbia mchaka mchaka ule wa asubuhi

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,588
Reaction score
11,668
Kama ulisoma kidumu na ufagio, miaka ya 90s bila shaka uliwahi kukimbia mchaka mchaka ule wa asubuhi. Nakumbuka moja ya nyimbo zilizokuwa zikihamsha hamsha!

Kuna huu!
'Nelson Mandela, afunguliwe uhuru, katika jela ya makaburu' ......

Halafu kuna huu;
Jua lile literemke mamaa.....aiya ya ioooh ioh mama!

Na huu!
Idd Amin akifaaa, mimi siwezi kuliaaa
Nitamtupa Kageraaa, awe chakula cha mambaaaa! Teh!

Huo wimbo wa Idd Amini, nimeukumbuka muda huu wakati natafakari kipigo cha walemavu kutoka kwa jeshi letu pendwa la polisi. Ni aibu!
Mambo haya yalitokea pia wakati wa utawala wa Nduli Idd Amin Dada wa Uganda. Moja kati ya falsafa za Idd Amin ilikuwa kwamba, walemavu hawazalishi, kwamba wao wanategemea kwa sehemu kubwa wasio walemavu. Kwa hiyo hawachangii kukua kwa uchumi bali wao ni watumiaji tu, hawazalishi. Ni falsafa ya kijinga sana. Sio ubinadamu kabisa, ni unyama.
Kwa sababu ya falsafa hiyo, katika utawala wa Idd Amin Dada, walemavu na maadui wengine walisombwa kwenye malori na kutupwa katika mto wa Kagera ambao una mamba wengi.

Ndio maana tukawa tunaimba kuwa Idd Amin akifa, hatuwezi kulia bali na yeye tutamtupa Kagera. Awe chakula cha mamba.

Falsafa hiyo ya Idd Amin, haikuanzia Uganda. Ilianzia Ujerumani wakati wa utawala wa NAZI chini ya Adolf Hitler. Kwa hiyo unaweza kuona kuwa sio falsafa ya mtu mmoja aliyeaminika kuwa na ugonjwa wa zinaa ulioathiri ubongo, (Neurosyphilis) bali ni falsafa ya madikteta wengi.

"Kuna vilevi vya aina nyingi, pombe, marijuana, cocaine, heroine, nk hivi vyote vinaweza kuwa na tiba. Lakini ukilewa madaraka, hakuna daktari wa ubingwa wowote ataweza kukutibu".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule ya msingi Mwananyamala, Dar. Jua kali mno unanikimbizaje mchaka mchaka asubuhi?
Hatukuwahi kukimbia.
 
Mbona hata siku hizi ufagio,kidumu na mchakamchaka vipo tena shule za sekobdari jaribu kutembelea shule za mkoa wa tanga haswa muheza,handen sehemu ambazo zina shida ya MAJI sana. wanafunz wengi unawakuta wamebeba vidumu kwenye gar wakat wa kwenda skuli
 
hivi la kupigwa walemavu wetu mwigulu kakaa kimya kabisa, ina maana watasema wale waliowapiga walemavu sio askari wao

nitakuunga mkono pale utakapoacha chuki, ubaguzi na visasi
 
Mchakamchaka umerudishwa now watoto wanakimbia,msingi na sek

May Allah bless Me and You
 
Mbona hata siku hizi ufagio,kidumu na mchakamchaka vipo tena shule za sekobdari jaribu kutembelea shule za mkoa wa tanga haswa muheza,handen sehemu ambazo zina shida ya MAJI sana. wanafunz wengi unawakuta wamebeba vidumu kwenye gar wakat wa kwenda skuli
Hawa yaelekea wana maisha mazuri sana! Yaani anaenda shule kwa kutumia gari.....!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom