Kama uliwahi kula mishkaki ya mia mia, Morogoro basi uliwahi kula mbwa, jamaa wamekamatwa huko

Hii kisheria imekaaje?

Mteja amekuja akauliza mishkaki kiasi gani, ukamjibu 100. Akaamua kununua bila kuuliza nyama ya mnyama gani.

Apo muuzaji kosa lake lipo wapi endapo akajitetea kuwa mnunuaji hakuuliza ni nyama ipi.
Hakuna kosa hapo, watawaachia muda si mrefu, kama vile Kitimoto kuna watu hawali na wengine wanakula 😂
 
Kwa taarifa yako ni kwamba wapo wanaouza mishkaki ya nyani sana tu labda wahusika hawajafuatilia, endeni pembezoni mwa mji pelelezi mtaambiwa
 
Kuna kipindi nilikua natoka arusha kwenda mbeya kupitia morogoro, nikanunua chips na mishkaki, nlipokula nilitapika balaa na sijawahi kutapika kwenye gari.. inawezekana ilikua nyama ya mbwa
 
Dah isijekuwa na ya Masika nayo ni idog daaah, kuna kipindi walisema mishkaki ya urojo wa Baba Amina ni ya kenge daah
 
Yaani hata kama ni ugumu wa hela sio kwa hawa jamaa!
 
Hii kisheria imekaaje?

Mteja amekuja akauliza mishkaki kiasi gani, ukamjibu 100. Akaamua kununua bila kuuliza nyama ya mnyama gani.

Apo muuzaji kosa lake lipo wapi endapo akajitetea kuwa mnunuaji hakuuliza ni nyama ipi.
Utakuwa mteja mjinga. Mishikaki ya kuku na ng’ombe hata bei hutofautiana. Unakula mshikaki wa 100 unategemea uwe wa ng’ombe au kuku? Na mishikaki ya mbuzi wala siyo maarufu kihivyo. Kama hutaki hata kuuliza mishikaki ni ya nini, basi wewe ni mla mbwa.
 
Hii njia ya kwanzia morogoro chalinze hadi dar hawa vijana sio waaminifu njaa inaweza ikakukaba upo ndani ya basi na umepigika lakini ndo hivyo huwezi nunua bidhaa zao nyingi ni feki
 
Unakulaje nyama za kuokoteza barabarani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…