Kama ulizaliwa baada ya mwaka 1995 haya mambo yalikupita

247

Senior Member
Joined
Mar 29, 2016
Posts
188
Reaction score
197
1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin
5. Kupamba kadi na pamba sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa kwa mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..
12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..
13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini
14. Kukata ndala, eti ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..
17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.
18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kola Ya Shati.
19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".

20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakwambia ngoja shule ikifungwa



WEWE UNAKUMBUKA KIPI?
 
umesahau wasichana kwa wavulana kuvaa chupi ya 'tajiri'
 
Reactions: 247
Ilishakuwepo hapa umeirudia tu.
Hata hivyo namba 7,8,12 na 15 bado yapo...
 
Reactions: 247
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] kuunguzana na ubuyu baada ya kuusugua chini tena zile mbegu zake hadi lile ganda gumu linaisha
 
Reactions: 247
Kucheza kamari ya mabetri na gololi,mpira wa visoda,nduti,kuendesha ringi na magari ya waya,box na mbao,kushinda kukojoa mkojo mrefu,dobo dunda au tobo dunda,mchezo wa wali na nyama mnaweka kimlima cha mchanga na kijiti katikati mnaanza kuupunguza mchanga olewako ukiangushe kijiti ni mkong'oto mpaka ukimbie kushika mahali mlipo pateuwa,kucheza sembo(mpira wa malailoni) mnatoka kilimahewa hadi nera au isamilo
 
Daaa we acha huyo namba 4 nakumbuka Moira bwana kucheza kila Sikh kidonda hakiponi basis kila Sikh kuwekwa huyo dawa inauma huyo,namba 10 nimeitumia sana
 
Yani ata kabla ya kumaliza kusoma post yako, nilihisi utakua jamaa kutoka mwanza tu wew, maana majina ya michezo na mtililiko mzima una utofauti na sehemu zingine.
Shukrani kwa ukumbusho.
 
Kuzimana nguo kwenda kwenye sherehe
 
Kulala chumba kimoja guest watu zaidi ya mmoja hata kama hamfahamiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…