Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeona hicho tu eti😃Unawafunza watu umalaya sio?
Naonaga watu wanasema ukiona mambo yako hayaendi eti ndo umelaaniwa.. Ni stereotypes tuHivi maana haswa ya laana ninini?
Nadhani wazinzi watakua wamekusikiaUzinzi ni tabia, ndoa sio tiba. Binti jithamini 🏃♀️➡️
Ninachojuwa hakunaga mume ila mke wa mtu.mume wa mtu
Vizuri kama ni hivyoNinachojuwa hakunaga mume ila mke wa mtu.
Ndo ulichojifunza??.. okmafunzo ya umalaya
Laana ni kuwa na bidii isiyozaa matunda mema, kukataliwa, majanga, magonjwa na kutokuwa katika mfumo wa kawaida wa maisha kulingana na mila na desturi za mtu husikaHivi maana haswa ya laana ninini?
EwaaaHuu ushauri unawapa hawa wanawake ambao wakiamka wanakimbilia kuwasha data badala ya moto right...🤔
Na hao waume za watu wanasemaje? 🤣🤣🤣Wasalaaam, Hope mko gud☺️☺
( kama unajiona na unajijua wewe ni mwana wa israel basi huu uzi haukuhusu, pita kimya kimya) Sihitaji malaika hapa..
Leo wacha niseme na hawa wadada ambao wao wanaona kama wameshindwa kupata wanaume wao wa maisha, au ni kwamba wameshajikatia tamaa ya kuwa kwenye stable relationship,,, anyways..
Hiii sio tabia nzuri na haipendezi machoni mwa watu na inashusha heshima sometimes, ukiweza kuacha inabidi uache maana unaweza kujizolea laana zisizo na msingi,. Anyways hilo sio ninalotaka kulileta hapa maana ndoa sio ya kwajili ya kila mtu, kila mtu apambane na hali yake…
Iko hivi, kama umeamua kua mchepuko basi unapaswa kuzingatia yafuatayo, Maana kama ndoa umekosa jitahidi usije ukakosa vyote, walau upate hela na utamu maisha mengine yaendeee
1. Kwanza hutakiwi kujihukumu wala kujiona mwenye makosa, maana ndoa sio kwajili ya kila mtu na sidhani kama ulikua na ujasiri wa kumtongoza huyo mume wa mtu, alikufata mwenyewe na wewe kwasababu zako ulizoona zinafaa ukamkubali,. So acha kujilaumu kwanza wanaume wenyewe wako wachache,. Ila kama ulimfata au ulijipeleka mwenyewe jitafakari msichana ikiwezekana uache kabisa🗑️
2. Hutakiwi kumpenda mume wa mtu, yaani from day one unaingia nae kwenye mahusiano jiambie kabisa humpendi na hautakuja kumpenda mume wa mtu, kwasababu haitokaa itokee uolewe nae wala uwe nae milele,. Mambo ya hisia sijui nini nini weka kapuni jua kilichokupeleka kwake kama ni utamu make sure unaupata kwelikweli na kama hela make sure unazikusanya kwelikweli ( ila usijipe umuhimu sana jua mwenzio ana familia na majukumu mengine), so ukae kwa kutulia tena utulize bichwa lako na uache kiherehere kabisa kwenye familia za watu😏😏
3. Achana na mambo ya kucatch feeelings,. Kwanza mpaka umekua mchepuko na umekubali means ulikua unajua kama ana mke na anafamilia yake, kama umekubali kua option basi tulia kwenye position yako., Yale mambo sjui ya kujinunisha akimpost mkewe na watoto wake acha,. Ukisikia mke wake ana mimba jitulize hutakiwi kuona wivu yaani uwe na moyo mgumu kwelikweli( si ulitaka mwenyewe🤪🤪), tena sometimes akipost wanae msifie kwamba ana mbegu nzuri nanini nini , wetu tutazaa lini nikuzalie malaika na vitu kama hivyo..,,
Yaani jifanye hujali na ikiwezekana msifie kwelikweli , sometimes mwambie tu kabisa kama mke wake ni chombo mashallah ( umpe kichwa)huku ukijua nini unafanya, nitaeleza point inayokuja…
4. Hakikisha unajitoa ufahamu kwelikweli,. Yaani hapa nazungumzia uache ujuaji, Mtu ushajijua mchep unataka uanze na kutoa mawazo ya biashara mara sijui unamshauri ajenge mara sijui afanye nini, mwisho wa siku anaenda kufanya na mke wake huko unabaki unashangaa shangaa,. Wewe kama una mawazo yako ya biashara sijui kujenga omba tu mtaji ujifanyie zako mwenyewe( tena hatakiwi kujua ) ikiwezekana hata unavyoomba hela asijue kama unaenda kufanya nini msichana( sema hata ya wigi au kutengeneza kucha, ndo vitu wanavyopenda kusikia, atajua amepata boya asiye na akili atajikusanyia point, huku nawe unakusanya zote kimyakimya😃😂😂) .. kwasababu mwisho wa siku hakuna tuzo ya mchepuko mwenye akili., Ushakua plan b wewe jitulize fanya mambo yako ya msingi😃😂..
5. Usithubutu kumzalia mume wa mtu kama hana hela za maana., Yanini malaika aje asumbuke kwasababu ya dhambi zako for real??🧐🤨🙃. Yaani hili suala ni la kuzingatia kwelikweli , labda yeye mwenyewe mhusika akuombe na hakikisha mnaweka mkakati maalum wa namna ya kuhudumia mtoto ikiwezekana msainishane kabisa kabla hujabeba mimba,. Chakufanya wewe hutakiwi kukataa moja kwa moja ila mpe conditions zako maalum achague mwenyewe kusuka au kunyoa( Hapa nazungumzia kwa yule mwanaume unayeona kabisa hata akifa leo au kesho familia yake haitokaa ihangaike, means na mwanao pia hata pata tabu….)
Last but not least,. Fanya kila namna unayojua na ukae ukijua kwamba hii tabia sio nzuri na ikiwezekana kwa nguvu zote omba na ukemee kabisa utoke kwenye hiyo circle ya kudate na waume za watu,. Utazeeka vibaya sana na usipoangalia utasababisha laana kwenye ukoo wenu mzima.,.
Ila kama unaona umeshashindwa na jua lishazama na huna namna ya kufanya basi zingatia hayo,. Kama ndoa umekosa basi hakikisha unaishi sio kuishia,. Hizo mambo sijui za machozi ya mke wake yatakufanya nini nini ni . Karma ni hekaya tu kama hekaya nyingine,. Dhambi kila mtu atajuana na Mungu wake mbele ya safari ( jiamini mwanamke)
Am out😌😌😌
Ndo ulichokielewa mwana wa israel.. Anyways sawa😃Uzi wako unafundisha wanawake umalaya.
Japo umeuleta kitaalamu usisanukiwe!!!
My friend umalaya sio deal
Ni mateso matupu shauri watu wawe na watu wao permanent
Dhambi kwa waislamu ni kula nguruwe. Kuwa na mchepuko kwao siyo dhambiNdo ulichojifunza??.. ok