Kwanza hongera mkuu kwa kupata selection maana mpaka umechaguliwa jua kuwa umekidhi vigezo. So unastahili pongezi.
Pili juu ya gharama za maisha. Kiujumla maisha ya Mwanza au chuo pale gharama zake tukianza na jambo muhimu kuliko yote ( chakula ) sahani full na samaki na kila kitu ni kuanzia 1500/= hadi 2000/= hiyo ndio ilikuwa bei mpaka naondoka and i hope haijabadilika kwa saaana. Ila kama utataka uhuru nakushauri weka ndani stock ya chakula japo kwa uchache maana kuna miezi maaruf inaitwa "mwezi dume" huwa hali inakuwa ngumu almost kwa watu wengi chuoni.
Gharama za stationeries ni cheap kwa ujumla kutokana na competition ya mastationery yaliyojazana. So ni wewe tu na uchaguzi wako pindi utakapohitaji toa copy au kuprint kazi tofauti tofauti. Copy hadi naondoka zilifika page sh. 50/= na mapunguzo kibao ukiwa na page nyingi au kama unaprint.
Gharama za hostel: hapo mkuu kwa sasa SAUT naweza kukutoa shaka maana kipindi chetu kulikuwa na idadi kubwa sana ya wanafunzi so DEMAND ya hostel ilikuwa juu sana na wenye nyumba wakaongeza bei za hostel had kufikia Mil. 1+. Ila kwa sasa naona idadi ya wanafunzi imepungua japo sijajua mwaka wenu na mpaka tunaondoka hostel zilifikia hadi laki 5, so mnajichanga wawili mnakaa kwa amani. Hostel zitakuwa zinapatikana kwa urahisi kutokana na uzoefu wangu na jinsi nilivyoziacha nyingine zipo ktk matengenezo ( mpya ) baada ya kwenda fuata vyeti vyangu mwezi uliopita mwaka huu. →→Disadvantage ya off campus ni gharama za malipo ya maji na umeme japo si kubwa kama utakavuodhani. Maana maji ni bwerereee kutoka ziwani.
Ama kuhusu suala la hostel za ndani ni bei nafuu zaidi. Nadhani unalipia kwenye LAKI 2 hivi, sina exact info on that maana aijawahi kaa hostel za ndani. Ila disadvantage ni nyingi. Watu mnapokusanyika wengi ktk sehemu moja toka culture tofauti kidogo huwa ni challenge but i hope you'll be able to face it.
Nadhani hapo kidogo umepata mwanga wa maisha na cost zake zilivyo.
Usisite uliza lolote ambalo wahitaji maelezo ya ziada. Karibu.