Kama umekuwa ukitoa sadaka lakini hubarikiwi, sababu hizi hapa

Kama umekuwa ukitoa sadaka lakini hubarikiwi, sababu hizi hapa

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Kuna watu wanatoa zaka/sadaka kila mara makanisani, kwenye mikutano, kwa maskini, lakini hawaoni Mungu akiwamwagia baraka nyingi katika maisha yao, kama alivyoahidi katika Malaki 3:10, kwamba ukitoa atakumwagia baraka zake hata ukose nafasi ya kuziweka. Tatizo ni nini?

Kama hujaona baraka tele tangu uanze kutoa, sababu ziko nyingi. Ntakueleza baadhi ya sababu hizo:

Kutoa zaka/sadaka ni kama kupanda mbegu. Ukipanda mbegu kwenye udongo mbaya, mbegu hazioti, hivyo usitarajie kupata mavuno. Na pia ukipanda mbegu haba, usitarajie kupata mavuno mengi.

2 Wakorintho 9:6
“Lakini ninasema hili: Apandaye haba atavuna haba; naye apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu.”

Lengo kuu la kutoa zaka/sadaka ni ili chakula kiwemo nyumbani mwa Bwana. Katika Yn 4:34 Yesu anafafanua vizuri chakula hicho ni nini.

Yohana 4:34
"Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake."

Mahali ambapo mapenzi ya Mungu hayafanyiki, hapo sio penye udongo mzuri. Mahali ambapo watu wako huru kufanya chochote kilicho kinyume na Maandiko, hapo sio penye udongo mzuri. Kama sehemu unayopanda mbegu zako, hawajali kazi ya kuhubiri Injili na kuwafundisha watu kuyashika yote aliyoyaagiza Yesu, hapo pia sio kwenye udongo mzuri.
 
Kama unatoa sadaka lakini maisha yako bado ni ya dhambi, sadaka hiyo ni chukizo kwa Mungu, hivyo usitegemee kuona baraka zake.
Methali 15:8
Sadaka ya waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu
 
Ukitoa, toa kwa furaha. Kama unatoa huku unalalamika lalamika tu na kusema: "Ah, michango imezidi," usitegemee kubarikiwa.
2 Wakorintho 9:7
“Kila mtu na atoe kadiri ya alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa kulazimishwa; kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa furaha.”
 
Kama huna upendo, hata ukitoa sana huwezi kuona baraka za Mungu
1 Wakorintho 13:3
"Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini...kama sina upendo hiyo hainifai chochote..”
 
Kabla ya kumtolea Mungu, wasamehe waliokukosea
Mathayo 5:23-24
“Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utoe sadaka yako.."
 
Usitoe sadaka ili kujionyesha au ili usifiwe
Mathayo 6:1-4
"Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao. La sivyo, Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo. Basi, unapomsaidia maskini, usijitangaze. Usifanye kama wanafiki wafanyavyo katika masunagogi na njiani ili watu wawasifu. Kweli nawaambieni, hao wamekwisha pata tuzo lao. Lakini wewe unapomsaidia maskini, fanya hivyo kwamba hata mwandani wako asijue ufanyalo. Toa msaada wako kwa siri, na Baba yako aonaye yaliyofichika, atakutuza."
 
Ukitoa, toa kwa furaha. Kama unatoa huku unalalamika lalamika tu na kusema: "Ah, michango imezidi," usitegemee kubarikiwa.
2 Wakorintho 9:7
“Kila mtu na atoe kadiri ya alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa kulazimishwa; kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa furaha.”
" Kila mtu na atoe kadri ya alivyokusudia moyoni mwake" je sheria ya fungu la kumi inatoka wapi? Haikinzani na kifungu hiki cha maandiko?
 
Wapo waliotoa chote walichonacho lakini ngoma bado ikadunda... Unawakumbuka wale waliotoa sadaka ya kujimaliza?

Bahati ni nini? Bahati ni fursa iliyokutana na maandalizi
 
" Kila mtu na atoe kadri ya alivyokusudia moyoni mwake" je sheria ya fungu la kumi inatoka wapi? Haikinzani na kifungu hiki cha maandiko?
Andiko la Malaki 3:10 ndilo linalohusu sheria ya zaka(fungu la kumi). Zaka inapaswa kuwa kamili.
Kifungu ulichotaja kinahusu sadaka. Sadaka ndiyo ambayo mtu anatakiwa atoe kwa hiari yake(kama alivyokusudia moyoni mwake).
Kwahiyo hakuna ukinzani wa Maandiko
 
Kuna watu wanafikiri zaka au fungu la kumi ni sheria ya Agano la kale tu.

Katika Agano Jipya, Yesu ametaja pia suala la utoaji wa zaka(fungu la kumi).
 
Kuna watu wanafikiri zaka au fungu la kumi ni sheria ya Agano la kale tu.

Katika Agano Jipya, Yesu ametaja pia suala la utoaji wa zaka(fungu la kumi).
Katika fungu kifungu kipi cha maandiko?
 
Ukitoa, toa kwa furaha. Kama unatoa huku unalalamika lalamika tu na kusema: "Ah, michango imezidi," usitegemee kubarikiwa.
2 Wakorintho 9:7
“Kila mtu na atoe kadiri ya alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa kulazimishwa; kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa furaha.”
Kweli kabisa mkuu hapo umegonga penyewe. Tumekuwa na upumbavu mwingi wa kulalamika oooh sasa hivi kanisa Katoliki limezidi michango! Sasa hapo utapata wapi baraka? Bora hata usingetoa kabisa!
 
Katika fungu kifungu kipi cha maandiko?
Mathayo 23:23
Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa, bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.

Kifungu hicho maana yake ni kwamba tunapaswa kutoa zaka na pia tusiache mambo ya adili, rehema na imani.
 
Back
Top Bottom