Kama umetoka mkoani kuja Dar kutafuta maisha, tulia nikupe siri ili utoboe

Nimesoma hapa nikakumbuka zile story zenu za macasino nimecheka sana
Mkuu bado unaukumbuka ule uzi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]

Pesa inatafutwa asee we acha tu
 
Usiwe mgomvi, wala usipigane, hapa mjini kuna msemo "ukinipiga umepiga hela zako "
 
Kumbuka kwenye mitandao ya kijamii hakuna masikini wala mwenye Shida
 
Usi generalize kiasi hicho
Mjini kuna wachungaji wanaishi kishua kabisaa na hawana life style unayoitetea.

Maisha ya watu wala bata yana kipi Cha ziada zaidi ya kuchafua boxer, magonjwa ya zinaa, na kupata vitambi ?

Hoja ni kujitambua wewe ni mtu wa namna ipi, nani awe rafiki yako, na rafiki zako wanapatikana maeneo yapi ? Then set goals za kufanikiwa.

Maisha ni hustle, usikate tamaa ila lazima ukumbuke maarifa, bidii, na nidhamu ni msingi na nguzo ya mafanikio.
 
Usidanganyike kwamba fursa zinapatikana bar
usiige maisha ya mtu
Kuna binti alikuwa anatembeza sambusa bar yupo ndani ya rav 4, wanaume tukawaza kumbe hata deal hizi hizi za hela ndogo ndogo zinaweza kukutoa. Now yupo ndani ana hukumu ya 15yrs na mme wake dhidi ya meno ya tembo.
 
*Usiongee hovyo hovyoo ndoto zako, mipango yako, maisha yako, kuwa msiri wa mambo yako muhimuuuu, yasio ya muhimuuu yaongeee sanaa (yatumiee kuuza chai) ili uufahamu mjiii na walimwengu wakeee.
Hii sio kwa watu wa Dar tu
Hii itumie popote
Kuna Shekh nilimsikiliza ktk mawaidha yake akiizungumzia suala la kutopenda kuweka mipango yako kwa watu mana si kila unayemwambia anafurahi.
 
Point kubwa niliyoielewa sana n ya kuwa msiri kwa mambo yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…