2014 usiku niko hoi afu asubuhi yake ilitakiwa tuwahi kwayani..kwaya yetu ndio ilikua imepangwa mbele kabisa kwenye sherehe ya kumpokea Mwasham Askofu joseph mlola jimboni kwetu.
Nikamuomba mama dawa akanipa Diclopar nikanywa zote bila paracetamol na usiku sikula ajiki sina hamu. Asubuhi naamka Mama ananiambia mbona paracetamol bado zipo nikasema sikuziona hapo nishavaa sare zangu nawahi kanisani. Mama aliogopa sana akasema mwanangu una damu imara Hukula na hukumeza paracetamol na umeamka vizuri! Ila nilikua nasikia kizungu zungu kiasi. Nilikula saa 8 siku hiyo ulimi umenitoka kwa njaa