Kupona kwa hayo maumivu kwa namna uliyosema inategemea na chanzo/aina ya hayo maumivu. Mfano kama ni aina ya magonjwa ya athritis ni changamoto kidogo.
Ila kama yanahusiana na labda aina ya kazi au lifestyle yanaweza kuondolewa kwa kuchukua mfumo bora wa maisha kwa mfano mapumziko ya wastani wa masaa 8, kulalia au kuegamia, magodoro rafiki ya mgongo na mifupa (orthopaedic matress), au godoro gumu, vyakula vya kuimarisha mifupa na uroto, mazoezi ya yoga, mavazi yenye kurekebisha mkao wa mifupa n.k
*Kuna kazi hatarishi kama udereva, kazi za kukaa muda mrefu labda ofisini, kazi za kusimama muda mrefu mfano viwandani, kazi za ubebaji vitu vizito, vilalio visivyofaa, n.k