Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Ina nitokea sana
Mshukuru sana M/Mungu kwa kipawa hicho. Amini umejaaliwa nguvu ya kipekee ktk ulimwengu wa roho. Ni watu wachache hupewa kwa ajili ya kuwasaidia wengine wanaoteswa na wazee wa shughuli za giza.
Ila tatizo wengi bila kujua wana uwezo huu wanakuwa walevi na wazinzi na mambo mengine ya kumchukiza Mungu na malaika hivyo huwafanya malaika wakimbie na kuwarahisishia mawakala wa shetani kuwatumia.
Watu wa aina yako ndo watu ambao wanatafutwa sanaa na wazee wa kutumia nguvu hasi kama vile kutafuta utajiri,uchawi na mengine maana nyota zao zinakuwa na nguvu ya kipekee sanaa..
 
Kaka hii uko sahihi napitia mambo magumu sana ilo la pombe ni kweli
 
Kaka hii uko sahihi napitia mambo magumu sana ilo la pombe ni kweli
Oky pole sana mkuu mimi nimepitia magumu kwa miaka mingi sanaa na ndo hapo nikajikuta najifunza mambo mengi sanaa kuhusu Ulimwengu na Walimwengu, ila Mungu na malaika walikuwa wakinipigania kwa kweli.Hata ww kama mpaka sasa hujafa unayo nafasi, kama waweza jitahidi uache pombe halafu uwe mtu wa kusaidia wenye shida(namaanisha wenye shida za kweli) kila uwezapo, jitahidi katika maombi ya manuizi.(unaweza wiki nzima ukanuia kuomba na kusali kwa ajili ya jambo fulani) amini utaona matokeo chanya.
 
Asante nita kufuuta inbox
 
Ushaachia kisa mkuu?mi ninafanya biashara lakin sijazindika kitu siku hizi pesa zinapotea hata niesabu mara ngapi na hata nifiche wapi zinapungua mara ya mwisho nimeweka kwenye sansuku halafu nikafunga na kufuli lakin nimekuta 60 hakuna.
 
Ni kweli, ukiwa na imani Kali sana , na usiwe na dhambi , ila ushirikina una nguvu sana

Usichukulie poa nguvu za giza , Mimi nimejionea nyie mnasikia tu kwa watu[emoji16]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuna jamaa alinihadithia mama yake alikuwa mtu wa dini sana na alikuwa anarogwa ila yeye ni mshirikina kuna dawa alipewa na mganga ndo alienda kwa huyo mama anaemroga mama yake kumkanya amwache mama yake yeye anajua anachomfanyia mama yake,yule mchawi kweli akaomba msamaha na yule mama ake akapona maradhi yanayomsumbua,ila hakumwambia mwenyewe anajua yesu kamponya.
 
Kuna mshkaji alipewa na shart lilikuwa hilo akifanya mapenzi aivue yake ilikuwa kacha zile za shingoni na alale ikifika saa6 usiku hata akiwa safarini au porini alale tu anakwambia alikuwa anaona matukio yote ya kesho yake anakuwa kama anaerudia tu kila kitu,anasema alipiga sana hela ila siku hizi yuko road tu kama chinga anaunga unga ila amejenga na ana mashamba,alijisahau akafanya mapenzi kakivaa kikayeyuka.anachojialaum ni kwamba aliambiwa anaweza kupata chochote anachotaka lakin yeye alikuwa bado yank kwaiyo hakuwaza kupata vikubwa yani hata angetaka kwenda ulaya angefika,yeye alikuwa hajui hawazi ivyo,na hakuna mchawi aliweza kumsogelea hii dunia acha tu ndo aliweza kuona mama yake akiwa mkoani anarogwa na jirani yake yeye akiwa dar akaenda akamaliza tatizo.
 
Uchawi upo tena sanaaa tu kuna tajiri mkoani njombe jina nahfadhi..
Alitoka dar kununua gari kiusalama zaid akamchukua fundi toka dar kuja nae njombe. Walifka mikumi ghafla gari ikazima hakunA kitu kinachofnya kazi milango haifunguki. Tajir akawa amejua nn kimatokea sasa atafnyaje. Hawez kutoka akaongea na simu njee ikabid ampigie mkewe amwambie apulize chungu cha tatu. Fundi akabaki anashangaa baada ya mda gari ikawaka wakaendelea na safarii yule ndie alitupa hichi kisaaa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka hiyo tunasoma kuna jamaa mmoja niliishi naye hostel chumba kimoja wakati tupo chuo...yeye ilikuwa usiku anaamka usingizini anaenda toilet na kurudi kitandani kulala bila ya kujitambua...na asuhuhi mkiamka ukimwambia kuhusu tukio la yeye kutoka chumbani kwenda toilet usiku hakumbuki kabisa...yaani inakuwa siyo ufahamu wake bali ni nguvu za giza
 
Na hili zuio la kutopiga show ndo wengi limewafelisha, yaani ukikutana na watu walioshiriki hizi mambo unakuta anguko lake lilisababishwa na papuchi dah hii kitu hii mimi sijui tuu inamatatizo gani aisee.
 

Umeona sasa , mlokole na bado anarogwa


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huyo alikuwa anawangiwa mkuu, usimpongeze, muhurumie [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja kulikuwa na msiba mganga mmoja alifariki. Alikuwa mganga na mchawi mashuhuri. Sasa waru wakawa wanaingia wachawi wenzake na waganga wezake. Mzee mmoja akaja akawakuta wengine wanakunywa pombe kwa mirija akafika akavua koti lake chafuchafu hivi akatundika hewani lika ninginia, mwingina akaja akakaa hewani hajagusa chini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…