Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Naona umeshindwa kabisa kuvumilia?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji477][emoji477][emoji477][emoji477][emoji477]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wengi walinitafuta na kutaka kuwaelezea ni kipi hasa kilitokea hasa baada ya kupata vitu vyetu na wapo walonibeza mpka nikafikia hatua ya kuwaonyesha evidence. Mtanisamehe kwa kuwa siyo mzuri sana kwenye uandishi

NAMALIZIA,

Nakumbuka baada ya kuchukua vitu vyetu vyote pale polisi na vingine vilikuwa siyo vyetu but tulipewa vyote na nahisi polisi walitupa vile sababu,baada ya kupata vile vitu vyetu pamoja na zile fedha kuna baadhi walitaka kuchukua lakini kuna mambo yalitokea hivyo wakaone vile vitu vilikuwa siyo vya kawaida hivyo walitupigia sana simu nakumbuka simu ilikuwa inapigwa kila baada ya dakika tano,na la mwisho nakumbuka hata ticket ya treni hatukukata bali tulipanda treni bure second class(ni chumba ndani ya behewa mnakaa na kunakuwa na vitanda)

Nakumbuka tuliingia jioni ilikuwa mida ya saa jioni nakumbuka wakati huo kupata ticket ilikuwa ni ngumu mno,tulivyofika tu Stesheni tukapokelewa na polisi kisha msafara ukaanza mpka polisi ambapo tukakutana na mkuu wa pale nakumbuka tulikuta vitu vingi sana lakini tulichoambiwa ni chukueni kila kilicho chenu, tulikuta mpka hizo fedha tukasema zetu wakatupa bila kuuliza na kingine cha ajabu siku ya pili asubuhi tukapewa escort na polisi gari mbili moja mbele moja nyuma mpka tunaingia kigoma mjini.

wakati tupo njiani mzee alijaribu kumuuliza askari mmoja tuliyekuwa nae ndani ya gari inakuwaje mbona mnatufanyia yote haya haliyakuwa mlipaswa kutukabidhi na kutuacha tuondoke? jamaa ndo akatoa mkasa mzima.

kuwa siku moja baada ya lile tukio kutokea walipata simu,kuwa kuna watu wanaohisiwa majambazi wameuliwa na wanyama,kila mtu akawa anasema la kwake wengine simba,wengine chui,basi baada ya kupata hyo case wakaamua wawapigie watu wa maliasili ili waende kwa pamoja lakini cha ajabu ni kwamba baada ya kufika eneo la tukio,wakakuta miili imetapakaa sehemu yote ya porini mingine ikiwa haina mikono, miguu nk,lakini kitu cha ajabu waliwakuta wakiwa na silaha zaidi ya 15,lakini haikutumika silaha risasi hata moja.

wale majambazi pale lilipotokea tukio lile kulikuwa jirani kabisa na kambi yao ambapo ndipo walipokuwa wanaficha mali zote baada ya kuibia watu kwenye mabasi hvyo mali zilikuwa za kutosha pale hivyo ilikuwa unaweza kichukulia hvyo unaweza kupata picha kama binadam unaweza kufanya nini?

basi kuna baadhi wali...............,sasa kuna mambo yaliwatokea mazito sitapenda kuyasema kwaiyo kilichotokea ili usalama na uzima uwepo ilibidi wenyewe tukabidhiwe mizigo yetu yote na sharti la mwsho ni kwamba ni lazma tufikishwe kigoma mjini salama la sivyo .............,

Tulivyokifka kigoma ujiji ile gari ya mbele ilisimama nakumbuka ni zile difenda 110 nyeupe akashuka askari na wengine ote wakashuka kisha akatuambia jamani sisi safari yetu ndo imeishia hapa muende salama tukaagana pale lakini walikuwa wanatushangaa sana na hofu za wazi wazi na sisi tuliliona hilo sababu tulikuwa tumeshaambiwa nini kilichotokea.

Tukawasha gari mpka sokoni ambapo tulinunua mbuzi mzuri pamoja na zawadi zingine baba akasema lazima kituo cha kwanza twende kwa mzee juma njemba kumpa zawadi zake na shukrani zake,tulivyofika tukamkuta ameenda sokoni basi alivyofika akatuambia kuwa kila mlichopewa ni cha kwenu basi tukampa yule mbuzi japo hela na zawadi nyingine aligoma kupokea ila furaha ikapotea alipotuambia kuwa kile kiumbe ni cha kwenu na nyinyi ndo mtatumika kama mlivyotumika kukileta.

Ninachokumbuka ni mzee aliingia kwenye mfuko uliokuwa na zile fedha zote akampa yule mzee ili hilo swala alishughulikie yeye mwenyewe,mzee aligoma kata kata nachokumbuka ni chozi tu lilinitoka hasa baada ya kuambiwa kuwa kile kiumbe kama kitaendelea kuwepo bila kurudishwa kilipotokea basi kitaturudia wenyewe tukiisha kitaingia kwenye ukoo mzima kitamaliza na hata mkoa mzima.

Basi tukaambiwa kuwa ili kile kiumbe kiweze kurudishwa ni wahusika wakuu tutoe zawadi ya damu yah damu,tukauliza dawa gani mganga akatuambia kila mmoja anatakiwa atoe damu yake kidogo,lakini damu hiyo apatikane mbuzi au kondoo au ngombe then kila mmoja atoe damu hiyo kwa atavyojua yeye then hyo damu ichanganywe na apakwe mnyama huyo mwili mzima then mganga atatupatia maelezo nini cha kufanya,

Basi siku hyo mzee aliomba hilo swala tulifanye kesho,maana kwa leo ni ngumu ukizingatia tumechelewa na safari ndefu mganga akakubali ila ajasema hakikisheni mnafanya haraka sana kwani mwenye uwezo wa kukirudisha hicho kiumbe ni mimi na nyinyi mlioingia kwenye hilo agano maana anayeijua kesho ni mungu,sisi hao tukaondoka.

Tumefika zetu nyumbani ilikuwa ni kama kinisherehe kidogo bimkubwa alikuwa amepika msosi wa kutosha nakumbuka ilikuwa pilau mbuzi na vinywaji maana waliitwa mpka watoto wa mtaani kula siku hiyo ikapita.

siku ya pili ilivyofika nikamkumbushia broo kuhusu kwenda kumaliza ile kazi kwa mganga bro akanambia kausha na mimi nae nkasema ngoja nikaushe kwani mambo yameshakwisha, ilivyofika usiku ndo bimkubwa akatukumbusha jana mlinambia kuwa leo mnatakuwa kwenda kumaliza ile kazi mbona hamjaenda?kumbe mzee nae alikuwa anakumbuka ila akajikausha kimya kuambiwa ndo akajifanya kuzinduka,akamwambia mama bwana e hayo sisi tumeshayamaliza tutaenda hata week ijayo,bimkubwa aliongea sana ila ote tukamuona kama anapiga kelele tu.

nakumbuka tulikaa sana kwa raha nadhani unaweza kujua 7m ilikuwa inathamani gani miaka hyo,kwani mzee akitupa kila mtu laki 1 nilikuwa don mtaani naweza kwenda dukani nikanunua creti zima la soda dah ujana huu.


Kasheshe ilianza siku ya tatu,tumetoka kule mida kama ya saa 3 usiku,tunaingia zetu kulala ghafla ikapiga radi ambayo sikuwahi kuiskia toka siku ile mpka leo,baada ya kama dakika 5 tukasikia kishindo kikubwa sana juu ya bati ghafla ikawa kama mtu anakimbia juu ya bati letu,hali hiyo ilidumu kama dakika 10 nzima,ikafuatia sauti ya ngombe zizini kupiga sana kelele kutokana na kutokukutana na masuala ya kishirikina nikatoka nikafungua geti ilikwenda kuona kulikoni(kunifanya shujaa)ila kabla sijatoka nje kabisa nikatoa sura sasa ile nmetoa kichwa nje nachungulia ile kurudisha kichwa ndani lilikuwa limebakia skio nje niliskia kitu kama kisu kinakata skio kwa kasi ya ajabu mnoo alafu nkaishia kuona kivuli tu.

Nilipata maumivu ambayo makali mno,mzee alitoka ndani mbio japo walikuwa wanaogopa kuangalia skio linaruka damu nikahudumiwa nikakimbizwa mawezi hospital nilishonnwa nyuzi zaidi ya 12 lakini donda lilikuwa na alama kama nmengatwa na mbwa vile au mnyama mkali.nikabaki hospitali mpka asubuhi.

asubuhi mzee akaenda kwa mganga,bahati wakamkuta mke mtu lakini cha kusikitisha ni kwamba mganga alienda Kaleni (kuna kiongozi fulani alienda kumtibu) dah mzee alipagawa ndo akaanza kumuekezea kilichotokea mke mtu akamwambia tu ukweli yani hapo mwanako ilikuwa anatolewa shingo ni mungu tu,mimi cha kufanya sina msubirini mpka mwenyewe arudi kwa maana siku 3 mpka 4 mbele. kumbuka toka watu wanipeleke hospitali mda ule mpka sasa wako kwa mganga hakuna aliyerudi nyumbani.

basi mzee akakubaliana na mke wa mganga basi wakarudi nyumbani sasa wakati wanafungua geti wakawa wanasikia harufu kali ya damu na uozo,wakawa wanafuata damu iliyokuwa imetapakaa pale uani ambayo usiku wa jana haikuonekana wakaifata mpaka zizini walichokiona kilikuwa ni gombe mmoja yani alikuwa ameraluliwa mwili ote yani kama vile mtu alikuwa na panga alafu akamkata kata vipande vipande.basi wakasafisha pale na baadhi ya vipande vikazikwa,jioni nikaruhusiwa nikarudi nyumbani.

naomba niweke nukta hapa but naahid kuimalizia tulipata mitihani mingi mpka kuamua kwenda congo kumfata mganga huko huko ambako,tulikutana na viongozi wazito mno,ambao sitopenda kuwataja lakini la mwisho ni tulivyonusurika kuliwa nyama ndio nyama tena na watu wenzetu ntawasimulia vyote na jinsi gani tulivyoponea kutoka kwenye tundu la sindano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilitokeapo kisa kimoja cha wahuni wa Kigogo walipokwenda kwa Babu kutafuta utajiri, wahuni hawa walipofika kwa mganga na kuwaelezea kusudio lao ni kuwa matajiri, Basi Babu akawapa mayai mawili akiwaambia mkifika makwenu kila mmoja atavunja yai Hilo wakati akitamka kitu anachokitaka.

Basi wahuni wale wakafunga safari kurejea makwao, walipokua njiani mmoja wa wahuni wale akateleza na yai likiwa linaelekea kuanguka chini akatamka KU*A, Basi unaambiwa K zikamjaa mwili mzima hadi usoni (tena zenye nywele zake) muhuni wa pili kuona mwenzie kaadhirika ikabidi avunje yai lake huku akitamka mateno haya KU*A futika kwa msela wangu basi zile K zikafutika na ndoto za utajiri nazo zikafutika pia.

Usiku morooo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuh hii mkuu ifungulie uzi wake ikibidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tungekuwa na watalaam wa kutengeneza Movie, huu mkasa ungeuweka kwenye movie, ingekuwa Tamu sana. Usiache kumalizia story, hii Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo chonjo apa kuiskilizia.
 
Mkuu unaonaje ukaifungilia uzi wake coz sii tukuwa inasisimua Bali hata kufundisha piaa. Litandike jamvi stori izi zinabadilisha sana mawazo ya watu wengi humuu jf na hasa Katika utafutajii huu wa mali by the way poleni Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
movie gani ya kinigeria hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii tamu sana mkuu. Ukija next time usiache kuni-tag!
 
Walikuwa wanakuvulisha kivuli Cha maiti ili ufe..... Mungu ni mkubwa Sana na muweza wa yote
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na shuhuda kama hizi bado kuna raia hawa amini kama ushirikina upo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…