matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Hivi mtu anaanzaje kwenda kwa mganga?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
WW walikusaidiaje?Matapeli wapo pia waaminifu wapo na kazi zao ni chap kwa haraka unapata matokeo ndani ya dakika kadhaa tu
Matokeo ya fast lakini siyo ya kudumu, Yesu anatoa maokeo ya muda mrefu.Matapeli wapo pia waaminifu wapo na kazi zao ni chap kwa haraka unapata matokeo ndani ya dakika kadhaa tu
Huu ni ukweli mtupuNaomba niseme kuwa waweza kufurahia matokeo ya kwa waganga ila ipo siku mambo yatabadilika.
Yakija kubadilika utatamani uishi haya haya ambayo leo unayakataa.
Jifunze kujikubali na kuridhika, zaidi kuweka imani kwa Mungu. Kubali njia za Mungu na si za waganga.
hivi mtu anaanzaje kwenda kwa mganga?
Mkuu mimi nimeshajiapiza, hata Mungu akiruhusu mabaya yanitembelee Mimi au mtoto wangu ntakufa tu bila shida ila sio kwenda kwa mganga mpiga ramli.Sababu zipo nyingi .
Usiseme hautaenda ila omba MUNGU akulinde usiende.
Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Na huo ndio mwanzo wa ulozi. Mwisho wa siku utapata mlozi mbobezi mwenye mabomu makali kuliko wa awali, utatakiwa kuweka mzigo mpya wa ndumba ili mabomu mapya yasikukute. Hapo unakuwa ushaingia katika maagano na ibilisi.We acha tu!! Niliambiwa ili uishi kama mfalme unatakiwa kutoa "kafara" niliondoka bila kuaga wala sikuuliza ni kafara gani. Ridhika na unachopata halali ila ukimpata mganga atakaekukinga kiasi mtu akitupa bomu linarudi kwake poa. Mabomu yapo mengi na yanarushwa kila siku.
AiseeNakumbuka niliendaga kwa mganga mmoja hivi ili anisaidie shida niliyokuwa nayo
Basi nilivyofika pale akasema kwanza toa elfu10 hapo mapokezi then uje uonane na mie, nikafanya hivyo
Hatimaye niliruhusiwa kuingia ndani kwa yule mganga kisha akanipa kalatasi na kuniamulu niandike majina yangu mawili
Akaniambia ikiandika ikunje kalatasi kisha niletee nikafanya hivyo, nilipompa ile kalatasi akaichoma na akaniambia unaitwa fulani nikasema ndiyo, hii nikabaki najiuliza? Hiyu jamaa oajuaje jina langu wakati hata kalatasi hajaifungua anyway Acha tuendelee
Akanambia una nyota ya utajiri na ya kupendwa pia inaonyesha huko mbele utakua tajiri hivyo hizi nyota zako zimefifia, acha nikusaidie kusafisha
Basi akanambia nenda kanunue mafuta ya nazi pamoja na wembe kisha ulete nikaenda kununua nikampelekea, nilipofika akanambia vua nguo zako ubaki na boxer, nikafanya hivyo akanichanja kwenye miguu na mikono kisha akaniambia nenda nyumbani kesho uje ila usipeane mikono mtu wala kugusana bega, acha nicheke kwanza kwa vioja nilivyokutana navyo[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ebana ile natoka tuu nikakutana na yule mfuasi wake anaingia ndani c nikajisahau nakutaka nimpe mkono bahati nzuri jamaa akanikwepa, Kimbembe nilipofika nyumbani, nakumbuka ilikua majira ya saa moja nikiwa ndani nachukua maji nikaoge ndipo nilisikia sauti ya jamaa niliyekuwa nalala naye akiniita huku anaingia ndani kumbe alikua na rafiki yake aliyekuwa anafanya naye biashara ya mkaa yule jamaa alivyoingia ndani nikashangaa ananilete mkono ili tusalimiane bwana weee nikajikuta nampelekea mkono hiii nikakumbuka masharti niliyopewa najikuta naurudisha mkono haraka[emoji16][emoji16] aisee lile sharti lilinishinda kimtindo. Yote na yote niporudi nilimulezea akanambia najaribu kukuonyesha kuwa mimi siyo hao matapeli, basi alinisaidia kimtindo ingawa kwani alinipa dawa yakuondoa mikosi then akanambia ukipata hela njoo nikusaidie matatizo iliyokuwa nayo nikaachana naye kwa namna hiyo. Hicho ndicho nilichokutana nacho kwa mganga kutoka kigoma.
Jerrybanks anazinguaMi nauliza tu yule jamaa alieng'atwa sikio kamalizia stori yake ya juma nchemba !