Nakumbuka niliendaga kwa mganga mmoja hivi ili anisaidie shida niliyokuwa nayo
Basi nilivyofika pale akasema kwanza toa elfu10 hapo mapokezi then uje uonane na mie, nikafanya hivyo
Hatimaye niliruhusiwa kuingia ndani kwa yule mganga kisha akanipa kalatasi na kuniamulu niandike majina yangu mawili
Akaniambia ikiandika ikunje kalatasi kisha niletee nikafanya hivyo, nilipompa ile kalatasi akaichoma na akaniambia unaitwa fulani nikasema ndiyo, hii nikabaki najiuliza? Hiyu jamaa oajuaje jina langu wakati hata kalatasi hajaifungua anyway Acha tuendelee
Akanambia una nyota ya utajiri na ya kupendwa pia inaonyesha huko mbele utakua tajiri hivyo hizi nyota zako zimefifia, acha nikusaidie kusafisha
Basi akanambia nenda kanunue mafuta ya nazi pamoja na wembe kisha ulete nikaenda kununua nikampelekea, nilipofika akanambia vua nguo zako ubaki na boxer, nikafanya hivyo akanichanja kwenye miguu na mikono kisha akaniambia nenda nyumbani kesho uje ila usipeane mikono mtu wala kugusana bega, acha nicheke kwanza kwa vioja nilivyokutana navyo[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ebana ile natoka tuu nikakutana na yule mfuasi wake anaingia ndani c nikajisahau nakutaka nimpe mkono bahati nzuri jamaa akanikwepa, Kimbembe nilipofika nyumbani, nakumbuka ilikua majira ya saa moja nikiwa ndani nachukua maji nikaoge ndipo nilisikia sauti ya jamaa niliyekuwa nalala naye akiniita huku anaingia ndani kumbe alikua na rafiki yake aliyekuwa anafanya naye biashara ya mkaa yule jamaa alivyoingia ndani nikashangaa ananilete mkono ili tusalimiane bwana weee nikajikuta nampelekea mkono hiii nikakumbuka masharti niliyopewa najikuta naurudisha mkono haraka[emoji16][emoji16] aisee lile sharti lilinishinda kimtindo. Yote na yote niporudi nilimulezea akanambia najaribu kukuonyesha kuwa mimi siyo hao matapeli, basi alinisaidia kimtindo ingawa kwani alinipa dawa yakuondoa mikosi then akanambia ukipata hela njoo nikusaidie matatizo iliyokuwa nayo nikaachana naye kwa namna hiyo. Hicho ndicho nilichokutana nacho kwa mganga kutoka kigoma.