Nina visa vitatu kama ifuatavyo.
Utotoni nikiwa naupiga mwingi, nikajikuta katika shida ya goti kuuma kila ninapokuwa uwanjani, akili ya utoto ikaniambia, 'mpira bongo tena kijijini huku nani atakuona, achana na soka fanya vitu vingine'.
MUNGU si ng'wanamalundi, nikafaulu kuendelea na elimu sekondari huko nikawa kwenye kamati za uhamasishaji pamoja na ufundi kwenye ligi za ndani za shule pamoja na mashindano ya nje.
Kwenye shule yetu kulikuwa na mwamba anaupiga mwingi na ndo alikuwa mshika hirizi, maana yeye kwao ni waganga, tukiwa tunakabiliwa na fainali dhidi ya shule jirani, jamaa akaja asubuhi mazoezini akatuambia iko hatari ya kupoteza kama vipi ile kamati ya ufundi tufanye jitihada za maksudi kutetea taji.
Wanakamati tukaingia mzigoni, ikumbukwe mie nimeingia kwenye kamati kwa sababu ya uwezo wa kuhamasisha ila hizo ishu sijui a wala ba, tumehangaika mishe zinafeli, baadae mwana mmoja kwenye kamati akaja na wazo la kwenda kijiji cha tatu toka shule ilipo, maana kuele kuna babu ni mzuri wa hayo mambo.
Jioni ya siku ile tukaenda wana kama wanne hivi tumefika kwa mzee, tukamkuta tukayasema yetu, babu akatuingiza ofisini kwake, tuka kaa duara kuzunguka ungo babu akachukua punje kumi za mtama akampa kiongozi akazihesabu, akampa anayefata akazihesabu zikapita kwetu sote kila mtu akawa anazihesabu.
Tulivyomaliza, babu akaziweka zile punje kwenye ungo, halafu akawa kama anazipikichia kwenye ungo, ghafla kitu ikawaka full tv aisee kwa mara ya kwanza naona mpira kwenye ungo na ni mpira unaopigwa kesho. Ukapigwa hadi mwisho tukala tano, babu akaanza kufuta, mpqka likabaki goli moja, ikawa kila akijaribu kufuta, inatapakaa damu.
Mwisho babu akaamua kumsaka aliyeroga, mara akatokeza lakini ni chogo tu jitihada za kumgeuza yule mwamba tuone uso zikafeli, babu alichofanya akatupatia op
1. Tukubali kulala kwa lile 1
2. Tufute lile goli ila mtu afie uwanjani.
3. Tumpige sindano yule mwamba pale kwenye ungo na ieleweka kuwa ukichoma sindano kwenye picha ya jamaa hapo kwenye ungo ndo umeua.
Tukaona tabu yote ya nini wacha ikae, cha kushangaza siku ya game ilikuwa kama unaangalia marudio yaani kila tukio unaliona kama lilivyo.
******KISHA CHA PILI******
16.05.2008, tukiwa tumemaliza mock 4m4 tulipo kuwa tunaishi tulikuwa kama watu 50-60 kwa kuwa wengi walikuwa wanatoka maeneo jirani wana wakalaza mishale tukabaki watu kama saba hivi, jioni wenzetu wakaenda sokoni tukabaki watu wanne.
Shule yetu ilikuwa imejengwa kati ya kijiji na kijiji na hapo vijiji viko umbali wa 7-10 kufika shuleni na eneo lile tulikuwa na wanakijiji wacache sana waliojitenga huku wengine ikisemekana walifukuzwa toka vijiji vingine kwa sababu za ushirikina.
Jioni ile tukiwa ndani, tukasikia kelele toka kwa jamaa ambaye ni mwanafunzi mwenzetu ambaye pia tulikuwa naye ndani ila alitoka kwenda kujisaidia haja ndogo, jamaa kaingia anatweta, tukamuuliza, akasema kamuona mwamba mrefu anafikia nusu ya mkaratusi sasa tulipo kuwa tukiishi kulikuwa na miti ya mikaratusi, moyoni nikajisemea hapa ligi imeanza.
Nikatoa wazo, kwa wale ambao walikuwa hawajala wafanye fasta halafu tulale room moja, wakati tunafanya miamala ya msosi mara walio kuwa sokoni wakaja tukawaeleza mkasa mzima na mipango iliyopo wakakubaliana nasi,
Wakati wengine wanaendela kumalizia kunya miamala ile mwana mmoja akawa kabanwa na mkoja ikamlazimu kwenda nje, lile jengo lilikuwa na kolido lefu halafu kulia na kushoto ndo kuna vyumba ile jamaa anakaribia mrango wa kutokea akakutana na kajitu kafupi kanachungua, jamaa alifunguka huku akisindikiza na yowe, mpaka kwenye rum ambayo wana walikuwa wanakula, ugali ukakanyagwa wana wakawaza fasta wafungue mrango wa mbele tutoke tusepe, ile tunafungua mrango tukakutana na yule ngongoti tukarudi ndani ikawa ni fujo tu full kukanyagana.
Tunakuja kutulia tukashauriana kusepa kwenda kulala kwingine.
*********KISA CHA MWISHO********
Shule yetu ilikuwa karibu na eneo tulilokuwa tunaliita mtoni kwa kuwa kulikuwa na chemchemi na hapo ndo tulienda kuoga, kufua na kuchota maji ya kutumia, ilikuwa hukosi mtu kila jioni.
Siku moja nikaenda kufua, nilivyofika nikaendela na kilichonipeleka wakati nafua akaja dogo mmoja akachukua sabuni yangu nikamfata nikamnyang'anya, dogo akaenda analia baada ya muda kaja wameongozana na dada ake, walivyofika wakaniazishia tifu wakidai nimemnyanga dogo soap, nikawaeleza hawanielewi. Kumbe ishu ni kuwa dogo alikuja kufua akasahau soap sasa alivyofika akachukua yangu akijua ni yake. Nilivyokqza wakaondoka wakidai nitaona.
Siku hiyo nimepiga msuli hadi saa 4, ile nataka kulala usingizi hakuna nikaona nivute muda kufika saa 8 ndo nikahisi usngizi, nikatoka kujisaidia haja ndogo ile nageuka kurudi ndani, nikasikia kama kuna mtu anatembea batini kucheki sioni mtu, akili ikaniambia hapa tupo vitani.
Nikaingia ndani nikiwa na hofu si ya kawaida, nilivyofika ndani nikazima taa nikaanza kuhangaika kujunjua shuka na kama mjua vyo shuka linakunjuliwa kwa mikono na miguu ile miguu inakunjua kutafuta msawazo wa shuka nikashangaa rum yote imejaa mwanga kama taa za gari aisee nilitetemeka nikashusha miguu taratibu nikajikutanimepitiwa na usingizi nakuja kustukanasikia kelel kwa jamaa wa rum ya jirani, nani atoke full utulivuvwa woga.
Kesho yake asubuhi jamaa nasema alihisi kama anapapaswa awali alidhani ndoto ila baada ys kutuliza akili akanotce ni kweli kujaribu kujinua mikono akagusa kifua cha mwanamke yaani alihisi kama vile kashika matiti, hapo ndo akaachia ukunga.
Vipo vingi ila hivi ni baadhi tu.
Tusameheane tu ikiwa kutakuwa na shida ya maandishi
Sent using
Jamii Forums mobile app