Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kiranga, acha kujishusha hata kama mtu, amezikwa akiwa mzima, kuna uwezekano wa kujitoa yeye mwenyewe, kaburini. Kwa dongo lile linawekwa pale, kwa Wakristo mtu huzikwa ndani ya jeneza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Some how littly i believe you, hasa wale wanaopata comma,ikaunganika na faint hapa huwa viungo vinafanya kazi in a very low heart pulse huwa na interval ndefu,hapa daktari akiwa na papara unapigwa kwenye freezer dadek....😛
 
Mganga alitaka kuwatatua marinda aisee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipenda dini ama lipenda damu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haaaahaaahaaa hii nzurii
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili tatizo hata mimi nikiwa mdogo nilikuwa nalo, nilikuwa na miaka 6-7. Kilikuwa kinaanza usiku wa manane kuelekea alfajiri yaani kilikuwa kinauma balaa. Ila kiliacha chenyewe sijui kama wakubwa walifanya kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilimtokea Mshiakaji wangu dereva wa lori
Anatoka zake Zambia akavuka Tunduma boda, alipoona yupo Bongo akaenda kuna mahali wanalalaga madereva basi usiku mnene akasikia kama watu wanapita nje akachungulia dirishani akaona kikosi cha WANGA wanawake wako msururu, ile bado anaangalia akamuona mzee mmoja yuko kwa nyuma ndo kama anawa command, basi kufika usawa wa dirisha yule mzee akawa kama kastuka hivi akageuka upande aliko jamaa(jamaa yupo ndani) akaanza kupiga hatua akilifata dirisha, jamaa kuona hivyo akaegesha kama amelala akiskilizia nini kinafuata, Ebana yule mzee alifika akaingiza kichwa kuchungulia ndani bila kufungua dirisha huku mwili wake ukiwa nje na kichwa mpaka usawa wa mabega kaingia ndani, jamaa akakausha mzee akawacheki akaona kama wote wamelala akazepa zake.
 
Kwenye soka ndo kuna uchawi first class
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi nipo maskani kuna wajomba walikuwaga wanakuja kila siku ya gulio kutokea bush, so wanalala maskani asubuhi wanasepa. Basi siku hiyo wakawa wamekaa sehemu hivi wanasukuma nda mara akapita paka akitokea upande wao wa kushoto, jamaa mmoja kumona akasema huyu paka ngoja nimponde, basi akainuka kutafuta jiwe akaenda umbali kidogo ile anapata jiwe akizani paka atakuwa amefika mbali anamwangalia alikokuwa naelekea hamuoni, anapotupa jicho anamuona kasimama mahali alipokuwa wakati jamaa anasema amponde, jamaa kuona hivyo akatupa jiwe akarudi kukaa na wenzake, Ebana Paka si akaanza kuelekea walipokaa, niko maskani nashangaa watu wazima wanakuja nduki wanapitiliza ndani wanafunga mlango.
 
Kuna ofisi niliajiriwa miaka mingi kidogo nyuma. Hapo nilipofika sababu ya uchangamfu wangu walinzi walinizoea na kunifungukia mambo yanayofanywa hapo na kunitahadharisha ikiwemo baadhi ya Managers kuchinja mbuzi (kafara) usiku kukiwa hakuna staff hata mmoja.

Haikupita mwezi nikaanza kuumwa kichwa cha ajabu na kutetemeka! Kila nikipima tatizo halionekani na nikipata nafuu kidogo nikakanyaga ofisini kinaanza upya!

Tukaona na wife hapa tuingie kwenye spiritual warfare na kushirikisha waombaji. Siku nimefanyiwa maombi nilikuwa na hali mbaya zaidi lakini baada ya maombi ya nguvu nilitoka jasho jingi na kichwa kikakoma pale pale kuuma!

Mtumishi akanishauri nisikanyage ardhi ya ofisi bila kujifunika kwa damu ya Yesu, ndio imekuwa desturi yangu hadi leo sigusi ardhi ya ofisi bila kujifunika kwa damu ya Yesu na nikiingia ofisini nachukua kitabu cha mawaridi ya sala na kusali kabla ya kazi!

Uchawi upo na shetani yupo kazini kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwongo tu na stories,pangine umevuta bangi Kama kweli uchawi unafanya kazi mlogeni Kiranga awe chizi mkiweza nilogeni na Mimi
Hayo ni mawenge tu!
Yule mzee eti kaniambia kakutana na mtu mweusi mwenye mkino mingi ya chuma upuuzi
Hakunaga uchawi shetani Wala mungu
Naami hivyo
 
Mzee baba uko siriaz au unatania? maana hata mie nilikuwaga siamini mambo ya kusikia, Nakumbuka siku moja nipo chuo nakula msuli kimbweta jamaa alinifata akidai hajala tangu usiku wa siku moja kabla ya jana( nimekutana nae jumatano mchana halafu akasema hajala tangu alipokula usiku wa jumatatu), nikaona kama ananipanga tu nikampa buku 2 akasepa. Ila nilikuja kufulia kuna kipindi nikawa nakoroga uji tu geto nakunywa asubuhi afu navunga mpaka usiku tena, ilifikia kipindi nikawa tena sioni haja ya uji navunga tu tangu asubuhi mpaka usiku napiga maji tu ya dawasco, ndo nikajua hakuna jipya chini ya jua.
 
Duuuh! ndo kali yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisema habari ya njombe unantisha,mwanangu anasoma huko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la kushikwa tako ni jingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuu naokoka na ujambz naacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…