Salange, Mimi kwenyewe nimewahi kusumbuliwa na kuumwa sana na kichwa nikiwa na umri baina ya miaka 14-16. Kichwa kilikuwa kinauma mpaka napoteza faham. Nikipelekwa hospital hawagundui tatizo. Siku moja mshua akanipeleka kwa MZEE mmoja(mtaalam). Yule MZEE akacheki vipimo,akachukua pembe ya Ng'ombe. Akawa ananichanja chale maeneo mbalimbali ya kichwa,baadae akawa anaibana na pembe ya Ng'ombe kila chale mithili ya MTU anayebana kizibo cha bic kwenye ulimi.
Baadae pembe inaachia taratibu kisha inadondoka. Kila ikidondoka kinatolewa kijiwe cheupe mithili ya goroli. Vilitolewa vijiwe 4, tangu siku hiyo mpaka Leo hii,sijawahi sumbuliwa na kichwa. Uchawi upo,asiyeamini amuombe Mungu aendelee kumpa uhai. Maana ukiwa hujafa,hujaumbika.
Sent using
Jamii Forums mobile app