Gemini Are Forever
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 1,508
- 2,619
Anasimulia dereva wa Fuso Jangwani.
Hiyo siku wamekaa maskani kama kawaida wakisubiri wateja, haukupita muda akaja mzee wa kiarabu hivi(mburushi).
Mzee akaulizia huduma ya kupelekewa mizigo yake wanapopandia boti za kwenda Mafia, wapo waliomkatalia, akajitokeza kidume, akamwambia mzee twende. Akamwambia kuna vity vyangu nimenunua vingi viko Kariakoo, twende tuvipitie, swala la muda lisikupe tabu, nitakulipa kijana.
Huyu alikuwa ni mzee wa makamo kidogo, basi jamaa mpaka Kkoo, wakapakia safari ikaanza. Kufika pa kupandia boti, mzee akamwambia dereva sasa kijana wangu naomba unielewe hili, naomba twende nyumbani tuvuke pamoja nikakupe pesa yako, swala la muda wa kukuweka huku isikupe tabu. Dereva keshayavulia tena ikabidi akubali tu, safari ikaanza. Wamekwenda, boti ikafika pahala ni kwenye maji bado, yule mzee akamwambia muendeshaji kuwa simamisha hapo mi nimefika.
Kila mtu mle ndani haamin mzee anachokisema, mzee akawaambia simamisha, kweli nahodha wa chombo akatii, mzee akakuta wameshamsubiri tayari vijana wake, wakaanza kupakua mzigo ukaisha boti ikaendelea na safari. Sasa yule dereva akaamua kuwa mpole tu, akaambiwa na yule mzee kwa ukarimu kabisa, usiogope kijana karibu nyumbani, yule jomba akashukuru, wakaingia ndani, kwanza aliposhuka toka chomboni akaona bonge moja la mji, hajawahi fikiria kuliona. Kakirimiwa vizuri, akaambiwa ukitaka kuoa, njoo tu huku nina mabinti zangu hawajaolewa usiogope. Jamaa akapewa pesa yake akapelekwa pale pale aliposhukia akapandishwa chomboni mpaka ng'ambo. Baada ya tukio lile yule jomba hata umwambie nina mzigo nipelekee Temeke, humpeleki.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu umesahau na maandaz hapa[emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
dah nmesoma sana ngoja na mimi ntoe kisa kilichosababisha niape kuwa sitakwenda kwa mganga tena kwenye maisha yangu.
ilikuwa 2002,tunatoka dar tunakwenda mkoa wa kigoma kwa wanojua bara bara enzi hizo wanajua ni jinsi gani kulikuwa na majambazi hasa ndani ya mapori ya Tabora,bahati haikuwa yetu mida ya saa 5 usiku wakati tupo road tukakuta bara bara imewekwa bonge la gogo mzee akataka kujitahid aligeuze ghafla walitokea watu wamebeba bunduki ndo kwa mara yangu ya kwanza kuone mtu kashka bunduki huku kajizungushia mkanda wa risasi mwilini bro wangu ile kuwaona tu akakata moto tuliokuwa hatujazmia tulikuwa watatu 3 mimi mzee na bimkubwa.
Tulichezea sana vitasa mzee alidhalilika mno mwisho wa siku walichukua mpka viatu nakumbuka viatu vyangu vya kitoto vya kuwaka taa,then wakaondoka mpka na gari tulikaa pale mpka saa 11 ndo tukapata msaada tukaenda polisi but hawakuwa na msaada mzee akapiga simu kigoma ikatumwa nauli tukaenda moja kwa moja mpka kwa baba yake(means babu),sasa babu yeye kila alivyokuwa anahadithiwa alikuwa anacheka mno hasa akimuangalia bro na ujanja wake ote et kazimia,upande wa baba yeye alikuwa na hasira mno alichokuwa anataka yeye ni wale watu awashikishe adabu hata kufa wafe basi ilivyofika usiku tukaelekea sehemu fulani inaitwa ujiji kwa mzee fulani alikuwa anaitwa juma njemba.
Nadhani kwa watu wa kigoma wanaweza kuwa wanamjua,akaelezewa kila kitu akasema hicho ni kitu kidogo sana,huku na yeye anacheka kisha akasema kuwa pale kwake kuna mbuzi alimchinja sababu ya sherwhe ya mwanae hvyo itatubidi tumtafutie mbuzi mwengne amreplace ili iwe kama malipo yake baba akakubali,kilichofata akawaita wajukuu zake walete (ubumba) ni udongo fulani hivi wa mfinyanzi kisha akawa anatengeneza kimdoli kidogo cha udongo kama vile vya kitoto toto,baada ya kukitengeneza akaanza kukiandika maneno yake kisha akakisimamisha chini,then akaanza kuongea maneno yake aliongea sana baada kama ya saa 1 akasema mtu yoyote ndani ya hichi chumba haruhusiwi kukimbia wala kupiga kelele kwani kwa kufanya hivyo ndo itakuwa kifo chake.
Basi aliendele kusema maneno yake ghafla yule mdoli pole pole alianza kukua na kuwa mkubwa pole pole,baada kama ya dakika arobaini alikuwa ni mkubwa kama binadamu mwenye mwili mkubwa alikuwa anamkono na kifua kikubwa na mrefu,kwa mara ya pili bro tena akazimia kwa mara ya pili mim mkojo ulishantoka natetemeka kama nmepatwa na dege dege,mwisho yule mdoli akaambiwa shtaka letu kisha akaambiwa nenda hivi vitu vinatakiwa leo leo,theb yule mtu akafungua mlango akatoka mbio alikuwa ni mwanaume lakini yupo uchi na ni mweusi tii kama mkaa mpka macho hakuwa na ichi kiini cheupe ye alikuwa na kiini cha moja kwa moja cha weusi,alivyoondoka tukaanza kumpepea na kumwagia maji bro alivyoshtuka yule mzee akatuambia kazi imeshakwisha kesho mtayapata majibu yenu.
Ilivyofika asubuhi tukapigiwa simu nakumbuka enzi hizo kulikuwa kuna buzz siyo hii tigo na hata simu zilikuwa za mezani,tukaambiwa kuwa kuna gari imepatikana Tabora yenye namba kama tuliyoripoti pamoja na vitu vingine,tukaanza safari na treni mpka tabora kufika kule tukakuta vitu vyetu na vingne vingi tu ila mzee alisema vyote vilikuwa vyetu hela zilikuwa kama 1m lakini zilipatikana 7m polisi hawakuchukua hata cent na hata walivyopewa walikataa kata kata hakikupotea hata kifungo kisha baada ya kuchukua tukaambiwa kuwa hao majambazi waliotuibia walikutwa msituni wakiwa wameuwawa wakasema wanahisi ni wanyama wakali ndo waliwauwa maana walikuwa wanaalama za meno makali milini mwao na kucha.
lakini wakashndwa kuelewa kama ni wanyama ndo waliwashambulia ni wanyama aina gani na kwanini hawakuwapiga hata risasi moja hao wanyama na wakati walikuwa na silaha nzito?Baada ya maelezo mengi mzee akawasha gari mpka kigoma stend ya kwanza mpka kwa yule mganga tulinunua mbuzi na zawadi nyingne nying lakini mzee aligoma hakutaka chochote zaidi ya mbuzi tu,basi tukampka mbuzi wake, akasema imebaki kazi moja tu na kazi yenyewe ni kumrudisha yule kiumbe(mdoli mtu)ili asitudhuru na sisi maana ni wetu hapo mdipo ilipokuwa mtihani maana kuna msharti mengi tulikosea plus kujisahau sasa akawa anatuandama sisi atuue dah kila mmoja nyumbani anaalama ya yule kiumbe yangu ni kungatwa skio na kula kipande nikipata mda ntawamalizia kisa changu but mpka leo mimi kwenda kwa waganga ni big no,but thanks god tulitoka salama
picha ya nilipongatwa kwenye skio ambyo ni alama ambayo sitaweza isahau mpka kifo
Sent using Jamii Forums mobile app
Hatimae nimemaliza uzi wote
Ila nasikitika sijaona comment ya Mshana jr
Ndio hivyo tu mkuu??Mimi nitaandika vitu vichache tu
_Nimewahi kuwaona usiku wachawi wakicheza ngoma nje ya nyumba niliyopanga
_Nimeona misukule sana,Sana mingine ilikua inaiba mboga usiku,yenyewe inaiba Nyama &Unga wa ugali ama ulaxe kiporo asubuhi hukuti
_Nimewahi kumshuhudia mzee maarufu mtaani kila siku hua anabeba ndoo moja ya Unga pamoja na madumu mawili ya baiskerli anapeleka ktk nyumba moja hivi kila siku saa 12 jioni kumbe anafuga misukule mingi mno,Sasa niliwahi kumfumania ametoka kuwanga saa 11 jioni kachelewa kurudi kwake tukapishana naenda kuoga ametoka nyuma ya mwembe
_Nimewahi kua karibu na mchawi mkongwe kiasi Cha kutaka kununua Misukule
Bei hutofautiana maximum 3,00,0000per kichwa Bei huzid kutokana na nguvu matumizi na nyota ya msukule
_Nimeshakutana na waganga&wachawi wengi njiapanda wakiwa katika shughuli zao usiku mnene
_Nimefanikiwa kujua lugha za kichawi
Mshirika_Mchawi
Kijakazi_Maukule
_Nimefanikiwa kufahamu viongozi kadhaa was kichawi na kupiga nao stori
_Nimefanikiwa pia kurogwa na kutumiwa jini
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mwamba humu JF aliwai kusimulia alichomoa hii ishu ya vyeti feki ya magufuli wenzake waliogopa wakapigwa chini yeye aliingia tanga hapo akafanya mambo hakudakwa mpaka leo yuko kazini
labda nikupe connection ya fundi tu jamaa fundi amefanikiwa hadi kumpa mmoja wa mawaziri uwaziri ni noma huyo alafu hana tamaa ukifanikiwa ndio unaenda kumshukuruNataka kupata mwenyeji wa tanga kuna ishu nafuatilia,sijui nitampate,we we u mwenyeji tanga? Nampango wa kuja huko
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaaaa halafu kama utani kumbe hao watu wapolabda nikupe connection ya fundi tu jamaa fundi amefanikiwa hadi kumpa mmoja wa mawaziri uwaziri ni noma huyo alafu hana tamaa ukifanikiwa ndio unaenda kumshukuru
Hii imewahi nitokea mkuu ilikua mkesha wa mwaka mpya usiku kama saa nane nimemsindikiza demu hadi kwao ile narudi ukapita mwanga mkali halafu wa moto kama jua wakati kulikua na giza totoro aisee zile mbio ingekua mashindano hata Hussein bolt ningemshindaMwaka flani wilaya ya rombo nimetoroka zangu shule usiku wa giza nene kias kwamba hata miti unaiona kwa tabu sana ,nikakatiza mitaa flani ilikua kipindi cha baridi lakini ghafla nikaanza kuhisi joto la hatari mara paaap kumekua kweupe kama mchana wa saa sita na jua kali aiseee nilitimua mbio ile hali ilidumu kama dk moja hivi
Ikawa mwanzo na mwisho kutoroka shule usiku.
Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo fundi hatarilabda nikupe connection ya fundi tu jamaa fundi amefanikiwa hadi kumpa mmoja wa mawaziri uwaziri ni noma huyo alafu hana tamaa ukifanikiwa ndio unaenda kumshukuru
Haya mambo ni kuwa na ujasiri tu.Kupiga mtungi na kuvuta bangi inaonesha bado unauoga na hofu moyoni. Nenda ukiwa haujatumia hivyo vitu sababu ukiona halafu ukatoka nduki ukaenda kuwasimuliwa watu watakuona bangi na pombe ndizo zinakuchanganya. Hapo utakuwa umefuta ushahidi wote. Nenda ukiwa mzima. Uvute bangi na umelewa halafu uje uniambie umeona mchawi makaburini siwezi kukuelewa.
labda nikupe connection ya fundi tu jamaa fundi amefanikiwa hadi kumpa mmoja wa mawaziri uwaziri ni noma huyo alafu hana tamaa ukifanikiwa ndio unaenda kumshukuru
Nasikia yule jirani na msomali ni hatariHaya maisha yana mambo mengi nyuma ya pazia.
Kuna watu wazito huwa wanaenda kwa mafundi Handeni na Pangani.
Hao mafundi wapo, kuna siku sitosahau kuna kijiji huko Pangani nilikuwa napenda kwenda weekend kupiga story jioni kuna kuwa na kahawa.
Nitamuuliza kuna mzee yeye ndio anajua nani mkali kama Messi na Ronaldo.Nasikia yule jirani na msomali ni hatari
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi
Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri
Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma
Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma
Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea
Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge
si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.
wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.
Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele
Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"