Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

JF imevamiwa na matahira
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2002 nikiwa bado yanki wa chekechea tu nina miaka yangu saba nilikuwa na katabia kamoja matata sana.

Wazee wangu wanapotoka then wananiambia nibaki nilikuwa nakubali then nawafuatilia nyuma wakifika mbali sana najitokeza kwa vile ni mbali wanakosa jinsi inabidi twende wote tu.

Tulikuwa tunaishi ubungo msewe kwa chini kidogo,kwenye lile ghorofa la Tanesco lililovunjwa,ukivuka barabara na kuteremkia bondeni,unavuka mto kisha ukupandisha unakutana na uwanja wa mpira,kushoto mwa uwanja kuna makaburi na katikati ya makaburi kuna njia ndogo ya mkato.

Mandhari ya eneo la makabuli,kulia kuna nyumba mbili ama tatu hivi zimejengwa kuzunguka makaburi,kuna vichaka vya maua na miti ya vivuli,kushoto kuna nyumba moja kubwa ya kifahari,miti ya maua na vivuli inakutana katikati ya njia,njia hii ina ukubwa wa hatua mbili hivi za mtu mzima,kingo zake zimepandwa maua,njia inayagawa makaburi katika sehemu mbili zilizo sawia.


Miti hii kwa juu imeshonana kiasi na kufanya njia iwe mfano wa barabara zinazotobolewa katikati ya mwamba au mlima(Tunel)sehemu ya kuingilia imepambwa kwa maua na kuwa kama mlango wa pango hivi sawia na upande wa pili wa kutokea eneo hili(ilichagizwa na maua yanayotambaa kama mapesheni siyajua jina lake maua yametambaa juu ya miti)


Basi hiyo siku nimeona wazazi wangu wanajiandaa kutoka kwenda kwenye harusi ,Mikocheni na sijataarifiwa na mimi nijiandae,nikaelewa! Nikachukua nguo nzuri(mayanki wa kipindi hiko wanaelewa maana ya nguo nzuri) nikazificha nje pamoja na viatu,nikawangojea watoke na mimi nikatoka,nikavaa chap na kuamza kuwafuata nyuma,huo muda ilikuwa saa mbili usiku kuelekea saa tatu.


Nikiwa nimewaacha umbali wa kama hatua kumi hivi,mwendo wa dakika tano tu ulitosha kutufikisha eneo la makaburi,nikasimama na kuwaacha waingie kuvuka nikawahesabia timing kuwa washavuka na mimi ndio nikaanza kuvuka.

Kwa vile nyumba zile tatu hazikuwa mbali sana mwanga wa taa uliangazia kidogo sana eneo hili,nikaanza kupiga hatua,harufu kali ya marashi ambayo hadi leo sijawahi kuyasikia niliyasikia vizuri sana,ile kutupa macho mbele namuona msichana mburushi,sijui mwarabu kasimama tuli pembeni ya njia ananiangalia ninavyozidi kumkaribia.


Nywele zake zilikuwa ni nyeusi na ndefu karibia kugusa kiuno,gauni jeusi lenye mng'ao hafifu,midomo ilikuwa na lipstick nyekundu,macho makubwa meupe na alikuwa amefumbata mikono yake kwa kuipishanisha kifuani kama wafanyavyo mabosi wengi wa mjini.

Kiroja kikaanzia hapa,kadiri navyomkaribia naye alikuwa anaongezeka urefu,wakati alikuwa mfupi kiasi lakini hadi namfikia ili nimpite tayari asingeweza hata kupita mlangoni labda kwa kuinama kidogo.

Nikamfikia na kumsalimia shikamoo,akaitikia mar habaaaa,wakati huo nimegeuza shingo juu kumtazama naye alinitazama,baada ya kumpita na na kumwacha hatua kama tano hivi,hizo mbio nilizotoka nazo kwakweli sikumbuki kuwahi kuzikimbia mbio kama zile.

Nikaliacha eneo la makaburi na kuteremka bondeni,nikavuka kidaraja na kupandisha barabarani,nikawasili kituoni(hiki kituo kwa mbele ndio unatazamana na jengo la Tanesco lililovunjwa,ile kutazama huku na huko wazee siwaoni na watu ni wengi,kiasi kwamba watu wakaamza kuhisi nimepotea wakataka wanishike wanihoji vizuri,nikawaponyoka nikashusha bondeni ili nirudi nyumbani.

Hatimaye nikafika eneo la makaburi,nikasimama nikijishauri kupita,moyo wangu uligoma,ulikataa katakata na hapo inaelekea saa nne na nusu usiku,nilichokifanya ni kuzunguka njia ndefu kwelikweli,nilitumia lisaa na nusu kuzunguka wakati kama ningekatiza makaburini ingekuwa safari ya dakika kumi tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi PhD nyingi tu zinapiga hodi kwa mafundi. Lakini wakiwa kwenye majukwaa wanatangaza wanazo degree 5.
Sijui degree hizi zinalinyajuaje taifa ikiwa madaktari both wa siptali na wa PhD wanategemea akili za mafundi??
NTAKUJA WEWE WAZIRI TULIYEPISHANA NAWE KWA MGANGA
 
HII IMETOKEA JANA USIKU

Nipo kwenye kijiji kimoja kipo katika wilaya ya NKASI huku mkoa wa RUKWA

Mishale kama ya saa 12 hivi jioni(jana) alipita mzee mmoja anatafuta mbuzi wake ambae kwa maelezo yake ni kuwa ameibiwa...amepita sehemu nyingi tu hapa kijijini ikiwemo na sehemu ambayo mimi ninaishi "kuomba arudishiwe mbuzi wake"

Mishale kama ya saa 3 sasa,nimekaa zangu naangalia TV Zilipiga radi 2 za ghafla tu(hakuna wingu wala mvua ilionyesha baada ya hizo radi)

Asubuhi hii naenda sehemu yangu ya kazi,mfanyakazi mwenzangu ndo ananiambia zile radi za jana ZIMEPITA NA WATU WAWILI(kuua)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kweli, naamini.
 
Nimekumbuka hiki kisa,

Mbeya mjini nilikutana na kisanga cha kubebeshwa mkojo na wazee wanacheza drafti, bao na kunywa kahawa,
Unakuta wanacheza wewe unaenda shangaa pale (mimi nilikua nasubiri coaster za usiku za dar) nimeshangaa wee baada ya dk 20 hivi nkabanwa mkojo nkarudi kwa mwenyeji nkamuomba anielekeze pa kujisaidia, nimerudi kujisaidia naenda kushangaa na kuskiliza stori zao, yaani ndani ya lisaa nilienda chooni mara 3, nkawa najisemea mapema yote hii hata maji sijanywa mkojo mwingi hivi?
Kwa sababu nilikua na safari niliogopa kunywa maji japo nilikua na kiu sana kwa hofu ya kusumbua gari njiani kuchimba dawa,

Gari ilivyokuja nkaanza pakia carolight zangu nkamaliza nilipotaka kurudi pale kuendelea kushangaa mwenyeji wangu akaniambia twende huku (hapo tunasubiri gari ijae abiria) tukakaa mahali tunapiga stori za hapa na pale ndio akaniambia nimekuona unabebeshwa mikojo tu hata huelewi, nkabaki namshangaa...
Ndio akaniambia ukienda shangaa pale kama hauko vizuri wale wazee wakiskia mkojo wanakubebesha wewe unaenda kuukojoa badala yao, yaani wanaweza kukaa asubuhi hadi jioni hata chooni wasiende ila wee kila mda unapiga ruti tu..
Hiyo ilikua mwaka 2010 pale uyole.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseeee ina maana uwaziri mwingine si kwa. Juhudi zao ila nguvu za giza

Sent using Jamii Forums mobile app
wote wanatumia nguvu za giza mkuu kuna waziri mmoja rafiki yangu nilikuta kwake kawafungia waganga kama 30 hivi anawalisha kila kitu wamtengeneze mambo yake yawe mazuri na kweli amefanikiwa jiwe anamsikiliza hatari japokua jamaa ni bogus tu
 
Hahaha kwahyo unaniambia madenge haongei chochote kwa huyo jamaa japokuwa ni bogus...[emoji23][emoji23]
wote wanatumia nguvu za giza mkuu kuna waziri mmoja rafiki yangu nilikuta kwake kawafungia waganga kama 30 hivi anawalisha kila kitu wamtengeneze mambo yake yawe mazuri na kweli amefanikiwa jiwe anamsikiliza hatari japokua jamaa ni bogus tu
 
Mimi na mshkj wng niliwahi kuenda kwa mtaalam mmoja nilimsindikiza uyo mshkj wng mimi nilikuwa sina imani na nguvu za giza insuch kipindi iko afu nilikuwa mbishi, sas bana yule mzee alisema kimasihara kuwa kuna dawa nikiwapa unaona wachaw na majin usiku, mshkj wng aliogopa akaikataa mm kwa kiherehere changu niliiomba uku nikijichekesha nakudhan ni mchezo wa kuigiza. Alinipa akaniambia hii utaoga usiku alafu na hii utaipaka kabla ya kulala afu hii kesho asubuhi utaogea na kupaka ili kuiondoa iyo hali ya kuendelea kuona ila sharti ni moyo usizungumze chochote pindi utakapokuwa uona ukizungumza utajijengea mazingira ya uadui..nikakubali, Haha ayse yanii ule usiku siusahau kwa vituko nilivyokuwa naviona dunia ina mambo mengi nyiny zaidi ya unavyoiona..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukio LA kweli
Kisiwani kome ziwa Victoria mkoani Mwanza.
Baba yangu mzazi alitoka Mwanza na mkewe mama yetu mdogo wakaelekea kisiwani kome kutafuta mahali pazuri pa kufanya biashara na shughuli za uvuvi,walikuwa wanamiliki boti na wanafanya kazi wakiume kwa ajili ya kazi za boti,na alikuwepo mama mmoja aliyekuwa mpishi katika hiyo kambi ya faza...sasa Mimi na Dada yangu tukapelekwa kuishi na faza huko kisiwani sasa mambo yakaanza...
Jirani ya kambi alikuwepo Mzee mmoja anaishi umbali kidogo na kambi yetu,nyumba Yake ilikuwa katikati ya migomba palikuwa panatisha balaa mchana lakini kulikuwa na giza kama usiku,kumbe yule Mzee ni mchawi Wa kutupa,akajifanya rafiki mkarimu na kina faza...hadi sisi tukawa tunapenda kwenda kwake kuchukua pilipili,ndizi na viazi...akiondoka anaacha ujumbe pale kambini watoto waje kuchukua viazi tunaenda.
Huyu Mzee alikuwa muumini nzuri Wa kikristo akawa anaenda kanisani kila jumapili hakosi.

Sasa kumbe yule Mzee alikuwa anampenda yule mama mpishi,kila akimwambia yule mama akawa anamkataa hamtaki kwa kuwa ni Mzee..sasa alichokifanya akatumia uchawi wake kumpata yule mama mpishi wetu kambini.

Siku moja jumapili Mzee akapita pale kambini akasalimia huku akiwa kwenye furaha kubwa sana ikionekana dhahiri usoni,akamwambia yule mpishi nenda nyumbani ukachimbe viazi mimi naenda kanisani..akamuelekeza na matuta kabisa..kumbe alikuwa ameshatega mitambo Yake...yule mama kufika bahati nzuri au mbaya alikwenda peke yake hakuenda na sisi maana tulikuwa tunatembea nae kama mkoba.
Sasa alipofika akaanza kuchimba viazi kupiga jembe LA kwanza nyoka akamgonga mguuni..ile anajaribu kukimbia akamgonga tena kisha akapotea..mpaka Mara tatu akawa anapiga kelele kuomba msaada lakini wapi hakukuwa na MTU eneo lile au watu kusikia na kwenda kumsaidi mpaka akaamua kurudi kambini wakamfunga kitambaa ili sumu isipande mwilini na kusambaa...wakaja waganga wakienyeji kama watano kila mmoja anafanya utaalamu wake anashindwa mpaka akaja mganga Wa mwisho akampima kwa kutumia SAA ndogo..akasema mgonjwa ameshafariki kitambo sana,watu walilia sana,na yule Mzee alikuwepo anajifanya anatoa msaada kama msamari mwema.

Ikabidi maiti isafirishwe kwenda kuzikwa Mwanza mjini ,tulipanda boti na maiti kuelekea mwanza....kufika katikati ya ziwa mafuta yakaisha boti likaanza kupelekwa na upepo hovyo hovyo watu wakaanza kuomba dua zote mungu atuokoe maiti ifike salama na roho hai ziokoke!!!,Mungu saidia ikapita boti ya kishimba,wakaipungia mkono kwa mbali ikaja karibu na boti yetu..bahati nzuri faza aliwahi Fanya kazi na maboti hayo wakatusaidia mafuta ..tukafika salama mjini,maiti akazikwa salama msiba ukaisha.

Sasa baada ya siku kupita yule mama akawa anaonekana kwa yule babu mchawi wanaishi pamoja kama Mke na mume,ukimshitukia ukamuona yule mama anapotea...mpaka Leo sijui maisha yao yaliendelea vipi kichawichawi,kama walisha kufa au wapo hai Mungu ndiye mjuzi.
N.B
Ila Mzee alijipatia Mke kwa njia za kishirikina au giza!!!
 
nitapaje contacts za huyo mzee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…