Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mwaka 2016 kwenye upadrisho parokia ya buhangija shinyanga mjini..Tumeimba kwaya ya shirikisho. Kwaya moja ilikua inatoka Gamboshi.. Wanapakuza tu huko
 
Kuna rafiki etu mmoja walikuwa na party koko beach,sasa yeye ni mnywaji wa pombe zote.sasa akiwa coco beach akaja muhudumu àkamletea soda,jamaa akamfokea wewe mimi nimeagiza kitu fulañi na sio soda.yule mwanamke ambaye ni muhudumu àkàmsogelea na kumfungulia huku akimwàmbia utàkunywa soda.
Muda huo ni yeye ndie anayemuona muhudumu wale wenźie hawamuoni.
Baada ya muda ndugu zake wanamuona kaka yao àkiogelea kweñda kati kati ya bahari,sasa wao wanamshangaa si ameagiza kinywàji na kuogelea hajui anaogeleaje kufika kule (maji mengi) .Wakainuka na kuañz kumkimbilia huku wakimwita jina lake jamaa hakugeuka wakamwita sana hakugeuka mara àka wapotea baharini.
POLISI na familia źikamtafuta kando wa mbambao siku tatu jàmaaa hakuonekana hai wala màiti.siku ya tatu usiku ndio jamaa kaja mwenyewe anajokokota hajiwezi na kufika nchi kavu akadondoka.wàtu kumuokota muhimbili.
Alipopona ndio akatusimulia kuwà baada ya kukataa soda yule mwanamke alikasirika sana na akamchukua na kwenda nae baharini çhini kabisa kuna mwamba ambao walikuwa wàkibishana muda wote .yule mwanamke alikuwa anamwambia kuwa anampenda na jamaa alikuwa na msimamo wa kumkataa na alivutwa kutaka kuelekea chini ya mwamba zaidi ndio jamaa alijizatiti ende zaidi na wamepambana muda wote mwishowe yule mwanamke àka mwambia una bahati mizimu ta kwenu ina nguvu na imekulinda.
akaçhwa ,jamàa akawa ana hangaika kupanda ule mwamba wa mawe maana alikuwa ànaona njia ya kutoka shida ni kupanda amehangaika kupanda juu wabmwamba wa jiwe mpaka akatoka.ndio kutoka amepoteza fahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kisa hiki kilitokea mbuga ya katavi ambayo sasa ni mkoa, kuna mzungu alinunua kitaru kwa ajiri ya kuwinda wanyama. sasa siku moja akaenda kuangalia kitaru chake akiongozana na askari pamoja na wazungu wenzie Ile kufika akamkuta Mzee mmoja anatoka kwenye kitaru chake huku kabeba mnyama begani. Mule kwenye gari walibaki baadhi ya askari, inabidi askari wamwamulu Mzee kunyosha mikono juu na kuelekea kwenye gari ile kugeuka tu gari haipo pamoja na watu waluomo Ndani ya gari. mzungu akuamini kilichotokea inabidi amruhusu Mzee aende na myama ile mzee anaondoka gari ikaonekana ipo pale pale.
 
Wale waliosoma boarding mnamkumbuka miss corridor sjui nyie mlimwiitaje in short huyu ni jini huwa anatembea ukumbuni kwenye mabweni mashuleni au makambini au maholi tulitunga hilo jina sababu akitembea unaskia "ko, ko, ko " ile sauti kama ya viatu vya kike vyenye visigini virefu ukienda angalia huoni mtu ukibahatika unamuona mwanamke ana nywele ndefu kakupa mgongo anamalizia kukata kona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] miss corridor,, umenikumbusha mbali sana.. vyooni kulikuwa hakuendeki usiku hata mbebane kumi mkisikia hiyo "ko" au mlango umejibamiza "pa" wote mnatoka nduki kila mtu na hamsini zake,, chumba kilicho karibu yako ndiyo unaingia unajibanza humo humo hamna kuulizana tutajuana asubuhi.. wallahi maisha ya boarding kuna muda yananifanya namiss sana skuli
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah we acha tu ukiskia hvo ukumbini kwenye Dom unajifunika gubigubi wale wanaolala vitanda vya chini balaa sana wanajikunja [emoji3]

Olevel tulikuwa tunamuogopa advance tukiskia hvo tunaamka kwenda angalau tumfume wapi ila siku tuliona anakatiza anamalizia corridor tunaona mgongo na nywele ndefu nyuma tulikoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikawaje halafu
 
Kubababake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Username yako imetokana na hiki kisa??
 
Alikuwepo mfanya biashara mmoja huko(alikuwa anafanya biashara za magendo) basi kila alipokuwa anapita na pikipiki yake akawa anasumbuliwa na askari mmoja wa barabarani ikabidi awe anatoa hongo ili asikamatwe ilifika time akachoka kutoa hongo.

Siku mmoja akapita kama kawa akasimamishwa na yuleyule askari. Alikuwa na ndoo amefunga kwenye pikipiki yule askari akaenda kukagua haaa akakutana na kichwa cha mtu kinatoa damu mbichi kana kwamba kimekatwa muda huohuo.

Askari aliruka kwa mshtuko maana hakutarajia kuona kitu kama hicho wenzake kufika pale kwenye ndoo hawaoni kitu.

Unaambiwa alitoka pale moja kwa moja kuomba uhamisho kurudi kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya “ mafanikio” yako kiboko kabisa.
 
Yaani kwanza mie ndiyo maana maisha yangu yote ya boarding nilikuwaga napendelea kulalia vitanda vya juu tu sikumbuki kama nimeshawahi kulalia cha chini
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…