ngoja tu nimalizie kisa changu kingine,but huwa nikimsikia mtu anasema uchawi hakuna namwangalia na kutikisa kichwa tu.
Nimezaliwa na mama ambae ni mgonjwa wa sicle cell hali iliyokuwa inamfanya mama yangu kuumwa mara kwa mara hasa mifupa na hata kuishiwa damu mara kwa mara naweza kusema mama yangu haikuwahi kupita week bila ya kuumwa au kulazwa hospitali,hali iliyopelekea kuwa anatumia mara kwa mara dawa za valium na hata wakati mwengine kuwa anajichoma mwenyewe sindano za valium ili apunguze maumivu apate usingizi,ilikuwa ni usiku wa saa 8 usiku nimelala na bimkubwa naskia anaugulia maumivu makali mno ya mifupa,nikaanza kutafuta dawa hakuna sindano wala vidonge na nyumba tulikuwa mimi na yeye tu wakati huo simu ni anasa na usafiri huu wa boda boda hakuna na gari ilikuwa saa 4 mwisho, basi kila akiugulia maumivu akili yangu inahangaika mwisho wa siku nikamchukua nikamuweka mgongoni kulikuwa kuna dispensari fulani hvi ipo kigoma ujiji na sisi wakati huo tunakaa bimala kwa wenyeji wa kigoma wanakujua ni umbali wa kama dakika 10 kwa gari,basi nikamuweka mama yangu mgongoni safari ikaanza wakati huo nina umri wa miaka 12 tu,tembea sana kila nikiskia anazidi kuugumia na mm ndo naongeza spidi,basi tukafika sehemu moja inaitwa shine cinema ni ukumbi fulani hivi walikuwa wanaonyesha movies na pembeni kuna shule ya msingi ujiji, baada ya kufika pale ile shule tuliona imegeuka treni watu wanashuka na kupanda wakati huo upande wa pili kwenye ule ukumbi kwa nje tukaona watu wengi mno wapo nje wanapiga kelele mno wanasherehekea wako uchi wa mnyama wanauza vichwa vya watu ulimi na viungo vingne vya binadamu na kulikuwa kunanuka damu kweli kweli cha ajabu ajabu kufika pale nikashikwa na bumbuwazi kiasi cha kanga kulegea bimkubwa akaanguka lakini kwa kusimama sasa alivyofungua macho kuona kilichopo mbele yetu nilishangaa tu amenibeba juu alitoka mbio za ajabu huku akiwa amenibeba mgongoni mpaka ujiji kwenye ile dispensary alivyofika tu akazimia pale pale nakumbuka alikuja kuzinduka siku ya tatu na mtu wa kwanza kuniita alivyoamka tu nilikuwa mimi alinikumbatia na kuanza kulia sana(kisha akanitamkia nimekusamehe leo na siku zote za maisha yako) kauli hii aliirudia akiwa anafariki ndani ya mikono yangu mwaka 2007 kwa kunambia(nakufa mwanangu nakupenda sana na nakufa nikiwa radhi nawe uishi maisha ya kumpendeza mungu na uwapenda nduguzo kama ulivyokuwa unanipenda mama yako)
R.I.P my beloved mom
Sent using
Jamii Forums mobile app