Tajiri wa Magomeni
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 4,274
- 2,935
ilikuwa mchana?Hii ya kua macho halafu naona nanyuliliwa juu kwa kuvutwa na kitu kisichoonekana imeshanitokea mara mbili sitakaa nisahau, uwa ninasali sala zote mkuu
umewahi kuwasiliana naye tena?ulizaa naye?Nikiwa na miaka Tisa ya ndoa yangu sikuwahi dhani wala kujua wife ni mchawi maana alikuwa msomi wa juu sana na mtu wa kanisa sana.siku moja nikiwa nimelala ulivuma upepo mkali mno gafla nikiwa macho nikajikuta nanyanyuliwa juu aisee nilisali sala zote gafla nikarudishwa chini.Kuangalia pembeni yangu alipolala mwenzangu naona mbwa aisee ulikuja kama usingizi hivi sekunde wife akarudi ktk hali yake ya ubinaadamu.Kesho yake nikahama home na ndoa ikafa.
Sent using Jamii Forums mobile app
mtafute gwajimaapo kwenye kurudisha msukule....nna shida napo...kuna mganga anaiweza iyo kazi..? maana kuna mtu.nampenda kweli na walimchukua msukule..na hata kila siku namuota ila haongei...nahisi washamkata ulimi....nahitaji sana kama kuna mtu anaiweza iyo kazi
wazungu kumbe haya mambo na wenyewe wamoachana nae falasi uyo..anajifanya anaongea kingereza na elimi ya wazungu..akati mezani kuna dili la wazungu wanataka msukule mwenye sifa fulani wakafanyie kazi zao..na wazungu hao anaowaamini nao ni wachawi balaa
umeokoka?Me bado sijakutanaga na vimbwanga vya live, nimekutana na vya kwenye ulimwengu wa roho navyo navitoaga knock out
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3],aiseeengoja tu nimalizie kisa changu kingine,but huwa nikimsikia mtu anasema uchawi hakuna namwangalia na kutikisa kichwa tu.
Nimezaliwa na mama ambae ni mgonjwa wa sicle cell hali iliyokuwa inamfanya mama yangu kuumwa mara kwa mara hasa mifupa na hata kuishiwa damu mara kwa mara naweza kusema mama yangu haikuwahi kupita week bila ya kuumwa au kulazwa hospitali,hali iliyopelekea kuwa anatumia mara kwa mara dawa za valium na hata wakati mwengine kuwa anajichoma mwenyewe sindano za valium ili apunguze maumivu apate usingizi,ilikuwa ni usiku wa saa 8 usiku nimelala na bimkubwa naskia anaugulia maumivu makali mno ya mifupa,nikaanza kutafuta dawa hakuna sindano wala vidonge na nyumba tulikuwa mimi na yeye tu wakati huo simu ni anasa na usafiri huu wa boda boda hakuna na gari ilikuwa saa 4 mwisho, basi kila akiugulia maumivu akili yangu inahangaika mwisho wa siku nikamchukua nikamuweka mgongoni kulikuwa kuna dispensari fulani hvi ipo kigoma ujiji na sisi wakati huo tunakaa bimala kwa wenyeji wa kigoma wanakujua ni umbali wa kama dakika 10 kwa gari,basi nikamuweka mama yangu mgongoni safari ikaanza wakati huo nina umri wa miaka 12 tu,tembea sana kila nikiskia anazidi kuugumia na mm ndo naongeza spidi,basi tukafika sehemu moja inaitwa shine cinema ni ukumbi fulani hivi walikuwa wanaonyesha movies na pembeni kuna shule ya msingi ujiji, baada ya kufika pale ile shule tuliona imegeuka treni watu wanashuka na kupanda wakati huo upande wa pili kwenye ule ukumbi kwa nje tukaona watu wengi mno wapo nje wanapiga kelele mno wanasherehekea wako uchi wa mnyama wanauza vichwa vya watu ulimi na viungo vingne vya binadamu na kulikuwa kunanuka damu kweli kweli cha ajabu ajabu kufika pale nikashikwa na bumbuwazi kiasi cha kanga kulegea bimkubwa akaanguka lakini kwa kusimama sasa alivyofungua macho kuona kilichopo mbele yetu nilishangaa tu amenibeba juu alitoka mbio za ajabu huku akiwa amenibeba mgongoni mpaka ujiji kwenye ile dispensary alivyofika tu akazimia pale pale nakumbuka alikuja kuzinduka siku ya tatu na mtu wa kwanza kuniita alivyoamka tu nilikuwa mimi alinikumbatia na kuanza kulia sana(kisha akanitamkia nimekusamehe leo na siku zote za maisha yako) kauli hii aliirudia akiwa anafariki ndani ya mikono yangu mwaka 2007 kwa kunambia(nakufa mwanangu nakupenda sana na nakufa nikiwa radhi nawe uishi maisha ya kumpendeza mungu na uwapenda nduguzo kama ulivyokuwa unanipenda mama yako)
R.I.P my beloved mom
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Me mpaka leo huwa nikikumbuka huwa machozi yanakaribia kunilenga ilikuwa hv cku hiyo ilikuwa jmosi huwa ni siku ya mnada ilikuwa mida ya saa 2 kasoro kulikuwa na mbalamwezi imeangaza sana kiasi cha kuweza kumjua mtu ambaye yupo umbali wa 50m ile ya kama jua la saa 4-5 hv tupo watatu kuna sehemu tumeagizwa na wazee kwenda kuchukua mzigo wake kwaajili ya safari ya kesho yake basi tupo na story zetu na kuna njia tuliikwepa ambayo ni shortcut kwa sababu hzo hzo huko kuna miti mikubwa imeshona sana na makazi yako mbali basi tupo na story zetu kuna barabara ni pana tu wala haina miti pako plain kabisa mara kwa mbali tukahisi harufu kama mtu anajisaidia haja kubwa na tukaona kama kuna mtu amechuchumaa mbele na tukaona kitu cheupe kama shuka lililokunjwa kwakuwa ilikuwa kiangazi na cku ya mnada tukajua mtu kanunua mifuko anaenda kuhifadhia mazao lakn kadiri tunasogea harufu inaongezeka tena kali zaidi ikabidi tupunguze mwendo lakn mtu huyo hakunyanyuka mpaka tukafika kama hatua 15-20 ndipo hali ikabadilika na kuwa joto la hatari sana niliskia mwili unasisimka ghafla ni kama upepo flani kitendo cha haraka sana tulikuwa mbele ya kitu kirefu sana na kuona kama giza mbele aiseeee tuligeuza kwa speed ya hatari sana niliwaambia wenzangu tunakufa ila mmoja cjui aligeuza saa ngapi maana kitendo cha kugeuka ashasepa huyu niliyebaki nae alikuwa mfupi nilimshika kwenye mkanda kiunoni tulikimbia jamaa akawa hagusi chini vzr tulikimbia mpaka barabara kubwa tukakutana na watu wanatoka mnadani walituuliza maswali lakn hakuna aliyeweza kuwajibu midomo ilikuwa na kigugumizi sana uzuri walitujua wakatupeleka nyumbani maana tulikuwa tunatetemeka sana hakuna aliyeweza kuhadithia chochote zaidi ya kutokwa machozi wote hadi kesho yake ndio tuliweza kueleza nini kilitukumba ila siku hiyo mzee aliogopa sana sitakuja kusahau kamwe labda lije litokee lingine zaidi ya hilo but namwomba Mungu aniepushie mbali
Sent using Jamii Forums mobile app
uliona nini mzee?Mimi na mshkj wng niliwahi kuenda kwa mtaalam mmoja nilimsindikiza uyo mshkj wng mimi nilikuwa sina imani na nguvu za giza insuch kipindi iko afu nilikuwa mbishi, sas bana yule mzee alisema kimasihara kuwa kuna dawa nikiwapa unaona wachaw na majin usiku, mshkj wng aliogopa akaikataa mm kwa kiherehere changu niliiomba uku nikijichekesha nakudhan ni mchezo wa kuigiza. Alinipa akaniambia hii utaoga usiku alafu na hii utaipaka kabla ya kulala afu hii kesho asubuhi utaogea na kupaka ili kuiondoa iyo hali ya kuendelea kuona ila sharti ni moyo usizungumze chochote pindi utakapokuwa uona ukizungumza utajijengea mazingira ya uadui..nikakubali, Haha ayse yanii ule usiku siusahau kwa vituko nilivyokuwa naviona dunia ina mambo mengi nyiny zaidi ya unavyoiona..
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa
Sawa
Tuko Pamoja Sana Mkuu digba sowey
Samahani pia
Ngoja tuendelee kuburudika na Visa Aseee
Wakujifunza wajifunze
hahahaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3],madenge mwenyewe ndo wale waleHahaha kwahyo unaniambia madenge haongei chochote kwa huyo jamaa japokuwa ni bogus...[emoji23][emoji23]
aliwahi kukurogaMimi nakaa ujiji na hapa ninavyocomment niko ujiji,,ni kweli kabisaaa huyu mzee juma njemba alikuwepo ila ameshafariki,,na nilikuwa namjua alikuwa mchawi hatariiiii
vipi hati hamna?Kama una namba nipm mkuu,
Kuna mzee anataka kunidhulumu kiwanja changu kimagumashi.
Sent using Jamii Forums mobile app
huyo kimbambala bila shakaSiku hizi PhD nyingi tu zinapiga hodi kwa mafundi. Lakini wakiwa kwenye majukwaa wanatangaza wanazo degree 5.
Sijui degree hizi zinalinyajuaje taifa ikiwa madaktari both wa siptali na wa PhD wanategemea akili za mafundi??
NTAKUJA WEWE WAZIRI TULIYEPISHANA NAWE KWA MGANGA
Ina maana mganga alishindwa kupindua dawa za mwenzie?[emoji3][emoji3]Miaka mingi nyuma wakati nipo kanda ya ziwa. Timu yetu ya mtaa ilifanikiwa kuingia nusu fainali ya kombe la wilaya. Kutokana na kuwahofia wapinzani wetu, tukashauriana twende kwa mganga. Tulipofika nakumuelezea shida zetu, akatwambia kamateni yule kuku pale (kulikuwa na kuku wanakula kula pale nje kwa mganga).
Tulikamata kuku jike, mwenye madoa doa kama kanga. Mganga akaongea maneno yake pale, alaf akamchinja. Yule kuku hakutoa damu hata kidogo, mganga akashtuka. Alivyompasua ndani akakuta vitu vyote kuanzia figo, maini, moyo, utumbo n.k vimeoza. Palepale mganga akatwambia nendeni tu mkakamilishe ratiba vijana wangu wenzenu wameshawawahi.
Ile mechi tulipigwa 5-1.
Sent using Jamii Forums mobile app