Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nililia msiba wa mzee miezi 7 au 8 before ajafariki ghafla, ilikua mara kwa Mara naota amekufa, tumezika na tumekaa vikao vya familia kujua hatima yetu maana tulikua wadogo, nilikua nalia ndotoni Nikiamka Nna machozi kabisa, ila Nikiamka baba yuko mzima kabisa nilikua sielewi naona Ndoto tu... Ilikua haipiti wiki mbili mfululizo. Now ndio naelewa.
Ni mengi, naweza nika predict kitu kwa usahihi kabisa. Naweza kuona mazingira nitakayofanya kazi hata mwakani ndotoni au kwa hisia
 
Kisa kingine cha Kaka yangu mtoto wa Mama yangu mdogo.

Yeye kipindi hicho alikuwa amemaliza chuo akarudi Kijijini nyumbani kwao.
Huko akawa na mahusiano na binti fulani,baada ya muda alipata kazi akaja huku mjini..Mambo yakakaa sawa akataka kumuacha yule mwanamke, yaani alirogwa mdomo ulipinda .. Sasa Kuna siku alikuja nyumbani kwetu(kwa mamkubwa wake) kusalimia nikawa namshangaa mdomo upo pembeni kabisa ila haumwi chochote.
Kumuuliza mama ndiyo akanihadithia kwamba huko kwao familia ya binti ilimroga.

Ilibidi aendelee na yule mwanamke,baadaye akamuoa..tukafunga safari Hadi huko Kijijini tukacheza harusi.
Akamchukua mkewe wakaenda kuishi mjini.Yule dada alikuwa mrembo jamani huwezi amini Kama ni mchawi.
Mkewe akapata ujauzito,wanaendelea kuishi na mimba ilikuwa kubwa tu Kama miez 6-7.

Kumbe usiku wakilala yule dada alikuwa anaondoka kimazingara anaenda anakoenda asubuhi anarudi.
Wachawi wao kanuni yao akiondoka usiku ,mwili unabaki pale kitandani na inabidi usimuamshe.
Sasa yule Kaka alistuka usiku akamstua akaona mtu hatikisiki.
Yule dada aliondoka akaenda Kwenye anga ya sumbawanga huko na mama yake ,wameenda kuwanga huko wakazidiwa nguvu.(haya yalikuwa maelezo ya mama ya huyo dada)..huku Kaka alivyozidi kumuamsha ndipo alipoharibu Mambo.
Amsha dada haamki,kuita majirani amsha mtu haamki,kumpeleka hospital kumpima amekufa yeye na mtoto tumboni.

Mama wa huyu dada msibani alilia Sana,akaanza kumlaumu huyu Kaka kwanini alimuamsha mwanawe,alivyoona Mara ya kwanza hajatikisika angemuacha na asingeita watu.
Yule dada akawa amekufa hivyo,mtoto akatolewa tumboni ..wakazika.
Huyo binti ndiye alikuwa anaenda naye safari zake zote.

Baadaye mama mtu anamwambia yule Kaka kwamba ampe binti yake mwingine aliyebakia..
Huyo Kaka aligoma kabisa.
Hicho Kijiji hakijaendelea bado.. yaani Kuna wachawi hatari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Smart911 Ana moyo[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah aise dunia tunayoishi ina mambo mengi sana ya kutisha! Hivi haya ynafanywa na wadamu hawa hawa tunaopishana nao kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app

Binadamu ni kiumbe kikatili mno pengine hata wanyama wa porini. Huwa wakati mwingine namuelewa Mungu alivyoamua kuweka moto wa milele kwa ajili ya mwanadamu. Uovu unaofanywa na mwanadamu dhidi ya binadamu mwenzie ni mzito mno na hauchukuliki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwe unajitahidi kufwatilia
Hasa haya Mambo mabaya,huwa yanatokea kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu

hawa misukule huwa wanaumwa?

Naje wakifa wanazikwa?

Pia mwenyewe akifa inakuwaje?

Je kuna wachawi ambao hawaoa misukule wao au kuolewa na misukule?

kuna misukule wazungu au foreigners?

Watoto wadogo misukule hua wanakua wakubwa?
Kwanini wasiumwe mkuu, possibility ya wao ni kubwa kupata maradhi kuliko watu wengine

Wakifa Sitakua na jibu la moja kwa moja either huliwa nyama ama huzikwa

Mkuu unawajua au unawasikia? unapowaona wachawi,wanaushirikiano , wanajuana,na wana umoja ,atakapofariki Mchawi,mrithi lazima atawepo kwa ajili ya kurithi mikoba yake.

Sijawahi ona kwa muda ambao nimefanya nao kazi,Mchawi kua na mahusiano na msukule, pengine yawezakua lakini binafs Sitakua na jibu la moja kwa moja.

Kuhusu misukule foreigners hapana sijui Kama Ni worldwide au it's only Africa

Ipo , ipo ipo sana,japo si wote watazaa na wakalea watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakiwa wanafanya kazi huko shambani wanaonekana? Kama hawaonekani majirani watasemaje pindi wanapoona shamba limelimwa asubuhi na jana mpaka jioni lilikuwa halijalimwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio Mashambani hata barabarani,masokoni, wanatembeamo ,wanafanya shughuli za kawaida je hamna wanaowaona?

Jirani Hana nguvu yoyote,kila mtu anapambana kitu kiingie kinywani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtumishi ktk ubora wako [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ela za ndagu hizo.Huu utajiri gani bora niwe maskini


Kuna mzee na akili zake bosi tu mkubwa ye anakunya pembeni sio kwenye choo halafu hayaondoi au hasafishi yeye kuna mdada amemuajiri ndo anayasafisha na anamlipa kwelikweli na amekaa nae mda kweli yaani ukitaka ugombane nae yaani mzingue huyo mdada uone au mchokoze au mletee chokochoko huyo mdada ila nikajua tuu haya ni masharti



Nishawahi kuwa dereva wa coaster Fulani hivi baada ya kutoka route narudisha coaster tunapopaki kwa boss kwa ajili ya kesho siku nyengine boss anakwambia umuendeshe mtoto wake ana matatizo ya akili (taira) boss anataka tu umzungushe mpaka afurahi acheke kwahyo utakuta siku hyo tunazunguka na Costa mpaka basi hapo umechoka kichizi dogo akisema kata pale we Fanya hvyo sjui nyoosha we Fanya hivyo ili mradi afurahie mzunguko acheke tu baadae usiku tunarudisha Costa tunamshusha dogo kwa boss hapo boss lazima atutoe mshiko kidogo kisa cha kufukuzwa kazi hapo siku hiyo tumerudi mi na konda wangu boss akasema mzungushen dogo ukicheki siku hyo tunawahi mpira usiku nakumbuka ilikuwa Manchester derby tulikasirika kweli kwakua ni boss tukasema poa


Basi dogo akapanda tukaondoka naa tukaendesha tukafika karibu na bar maarufu tukamuacha ndan kuchek Mpira dogo alilia mpaka akatoa kamasi hadi utee daah si wapuuz mpira umetukolea dogo anataka azungushwe baada ya mpira tukamrudisha nyumban nashkuru mungu alikaa mulemule ndani ya gari akatoka maana angetoka akapotea aisee

Tunafika nae boss anamuona ametoka kulia hadi kamasi alijua tu ni mpira huo ndo umetuchanganya akasema kesho nisiwaone hapo ikawa ndo imetoka hivyo ila nashkuru nikapata dayworker ya haice
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tomino's Hell ni Shairi Ambalo Unaambiwa Hutakiwi Kusoma Kwa Sauti!, Soma Kimya Kimya na inaelezwa Ukisoma Kwa Sauti Shairi hili Kuna Mawili, Either Utakufa au Utapambana na Mauzauza Katika Maisha Yako!. .
.
Shairi Hili Liliandikwa Mwaka 1919 na Mwandishi 'Saijou Yaso' Raia wa Japan na Wakati Anaandika Shairi hili Alikua na Umri wa Miaka 26 tuu, Inaelezwa pia Mtu Huyu Hakuwa Mtu wa Kawaida!. .
.
'Saijou Yaso' Alikua Mwandishi Maarufu sana wa Mashairi Kutoka Nchini JAPAN, Alizaliwa January 15, 1892 Huko Tokyo Japan na Kufariki August 12, 1970. .
.
Shairi Hili Linamhusu Mtu Mmoja Anaeitwa 'Tomino', Tomino Alikua Anasafiri Kwenye KUZIMU!. Mwaka 1974 Muongozaji wa Movie wa Kijapan 'Terayama Shuji' Alitaka Kutengenezea Movie Shairi hili, Ajabu ni Kwamba Miaka Michache Baada ya Movie Kutoka ALIKUFA!. Movie Inaitwa 'To Die in the Countryside'. .
.
Je Kwanini Shairi Hili Linatisha? Kwanini Lazima Usome Kimya Kimya? na Je Huyu TOMINO ni Nani? .
.
Kuna Story Nyingi sana Kuhusu Mtu Huyu 'Tomino' Aliyeandikwa Katika Shairi Hili, Kuna Siri Kubwa isiyojulikana Kirahisi Kumhusu Mwandishi huyu ambaye Inaelezwa kuwa Hakuwa Mtu wa Kawaida!. .
.
Hiki ni Kipande tuu cha Shairi la Tomino, Kuna Lugha Tatu Tofauti Hapa, Liko Tlanslated.

姉は血を吐く、妹(いもと)は火吐く、
ane wa chi wo haku, imoto wa hibaku,
His older sister vomited blood, his younger sister vomited fire,

可愛いトミノは 宝玉(たま)を吐く。
kawaii tomino wa tama wo haku.
And the cute Tomino vomited glass beads.

ひとり地獄に落ちゆくトミノ、
hitori jigoku ni ochiyuku tomino.
Tomino fell into Hell alone,

地獄くらやみ花も無き。
jigoku kurayami hana mo naki.
Hell is wrapped in darkness and even the flowers don't bloom.

鞭で叩くはトミノの姉か、
muchi de tataku wa tomino no ane ka,
Is the person with the whip Tomino's older sister,

鞭の朱総(しゅぶさ)が 気にかかる。
muchi no shubusa ga ki ni kakaru.
I wonder whose blood is on it?

叩けや叩きやれ叩かずとても、
tatakeya tatakiyare tatakazu totemo,
Hit, hit, without hitting,

無間地獄はひとつみち。
mugen jigoku wa hitotsu michi.
Infinite Hell's one road.

暗い地獄へ案内(あない)をたのむ、
kurai jigoku e anai wo tanomu,
Would you lead him to the dark Hell, .
.

KIRANGA KAMA UNAJITIA UBISHI WA KISHABIKI EMBU FANYA HIKI KITU ARAFU ULETE HAPA MREJESHO..[emoji102]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shuhudia nguvu za MUNGU sio shetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…