Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nilivyokuwa narudi nilikutana na mtu tu wakawaida sana ila sijawahi muona akaniuliza unahisi kitu unachotaka fanya ni sahihi?? nikamwambia sijakuelewa akaniambia umenielewa ila tu hutaki kuelewa akaenda zake niliogopa sana ila niliamini Mungu yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana.Nakazia hapa kwa huu mstari.

Ayubu 33:14-15

14 Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nililia msiba wa mzee miezi 7 au 8 before ajafariki ghafla, ilikua mara kwa Mara naota amekufa, tumezika na tumekaa vikao vya familia kujua hatima yetu maana tulikua wadogo, nilikua nalia ndotoni Nikiamka Nna machozi kabisa, ila Nikiamka baba yuko mzima kabisa nilikua sielewi naona Ndoto tu... Ilikua haipiti wiki mbili mfululizo. Now ndio naelewa.
Ni mengi, naweza nika predict kitu kwa usahihi kabisa. Naweza kuona mazingira nitakayofanya kazi hata mwakani ndotoni au kwa hisia
 
Kisa kingine cha Kaka yangu mtoto wa Mama yangu mdogo.

Yeye kipindi hicho alikuwa amemaliza chuo akarudi Kijijini nyumbani kwao.
Huko akawa na mahusiano na binti fulani,baada ya muda alipata kazi akaja huku mjini..Mambo yakakaa sawa akataka kumuacha yule mwanamke, yaani alirogwa mdomo ulipinda .. Sasa Kuna siku alikuja nyumbani kwetu(kwa mamkubwa wake) kusalimia nikawa namshangaa mdomo upo pembeni kabisa ila haumwi chochote.
Kumuuliza mama ndiyo akanihadithia kwamba huko kwao familia ya binti ilimroga.

Ilibidi aendelee na yule mwanamke,baadaye akamuoa..tukafunga safari Hadi huko Kijijini tukacheza harusi.
Akamchukua mkewe wakaenda kuishi mjini.Yule dada alikuwa mrembo jamani huwezi amini Kama ni mchawi.
Mkewe akapata ujauzito,wanaendelea kuishi na mimba ilikuwa kubwa tu Kama miez 6-7.

Kumbe usiku wakilala yule dada alikuwa anaondoka kimazingara anaenda anakoenda asubuhi anarudi.
Wachawi wao kanuni yao akiondoka usiku ,mwili unabaki pale kitandani na inabidi usimuamshe.
Sasa yule Kaka alistuka usiku akamstua akaona mtu hatikisiki.
Yule dada aliondoka akaenda Kwenye anga ya sumbawanga huko na mama yake ,wameenda kuwanga huko wakazidiwa nguvu.(haya yalikuwa maelezo ya mama ya huyo dada)..huku Kaka alivyozidi kumuamsha ndipo alipoharibu Mambo.
Amsha dada haamki,kuita majirani amsha mtu haamki,kumpeleka hospital kumpima amekufa yeye na mtoto tumboni.

Mama wa huyu dada msibani alilia Sana,akaanza kumlaumu huyu Kaka kwanini alimuamsha mwanawe,alivyoona Mara ya kwanza hajatikisika angemuacha na asingeita watu.
Yule dada akawa amekufa hivyo,mtoto akatolewa tumboni ..wakazika.
Huyo binti ndiye alikuwa anaenda naye safari zake zote.

Baadaye mama mtu anamwambia yule Kaka kwamba ampe binti yake mwingine aliyebakia..
Huyo Kaka aligoma kabisa.
Hicho Kijiji hakijaendelea bado.. yaani Kuna wachawi hatari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kweli hata huyo houseg wangu alisema. .kuna kazi mbali mbali wanapewa kama yeye kazi yake ilikua jikoni na kutumwa kuua tu. .eti pia kuna siku za kusherekea tu hio siku wanaimba wanakula wanafurahiii. .lakini pia alisema kule hawawi na maumbo ya kibinadamu bali wanakua na maumbo ya wanyama au ndege wengine ng'ombe kuku n.k sasa Sijui inakuaje hapo

pia yule binti aliyeletwa kanisani baada ya kuonekana kwa miaka 5 kupita alikua anakula kwa mkono ila kama ndege au kuku yani kama anadonoa vile iwe wali iwe ugali
sijui inakuaje hapo

Cc Smart911
Smart911 Ana moyo[emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah aise dunia tunayoishi ina mambo mengi sana ya kutisha! Hivi haya ynafanywa na wadamu hawa hawa tunaopishana nao kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app

Binadamu ni kiumbe kikatili mno pengine hata wanyama wa porini. Huwa wakati mwingine namuelewa Mungu alivyoamua kuweka moto wa milele kwa ajili ya mwanadamu. Uovu unaofanywa na mwanadamu dhidi ya binadamu mwenzie ni mzito mno na hauchukuliki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nililia msiba wa mzee miezi 7 au 8 before ajafariki ghafla, ilikua mara kwa Mara naota amekufa, tumezika na tumekaa vikao vya familia kujua hatima yetu maana tulikua wadogo, nilikua nalia ndotoni Nikiamka Nna machozi kabisa, ila Nikiamka baba yuko mzima kabisa nilikua sielewi naona Ndoto tu... Ilikua haipiti wiki mbili mfululizo. Now ndio naelewa.
Ni mengi, naweza nika predict kitu kwa usahihi kabisa. Naweza kuona mazingira nitakayofanya kazi hata mwakani ndotoni au kwa hisia
Uwe unajitahidi kufwatilia
Hasa haya Mambo mabaya,huwa yanatokea kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu

hawa misukule huwa wanaumwa?

Naje wakifa wanazikwa?

Pia mwenyewe akifa inakuwaje?

Je kuna wachawi ambao hawaoa misukule wao au kuolewa na misukule?

kuna misukule wazungu au foreigners?

Watoto wadogo misukule hua wanakua wakubwa?
Kwanini wasiumwe mkuu, possibility ya wao ni kubwa kupata maradhi kuliko watu wengine

Wakifa Sitakua na jibu la moja kwa moja either huliwa nyama ama huzikwa

Mkuu unawajua au unawasikia? unapowaona wachawi,wanaushirikiano , wanajuana,na wana umoja ,atakapofariki Mchawi,mrithi lazima atawepo kwa ajili ya kurithi mikoba yake.

Sijawahi ona kwa muda ambao nimefanya nao kazi,Mchawi kua na mahusiano na msukule, pengine yawezakua lakini binafs Sitakua na jibu la moja kwa moja.

Kuhusu misukule foreigners hapana sijui Kama Ni worldwide au it's only Africa

Ipo , ipo ipo sana,japo si wote watazaa na wakalea watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakiwa wanafanya kazi huko shambani wanaonekana? Kama hawaonekani majirani watasemaje pindi wanapoona shamba limelimwa asubuhi na jana mpaka jioni lilikuwa halijalimwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio Mashambani hata barabarani,masokoni, wanatembeamo ,wanafanya shughuli za kawaida je hamna wanaowaona?

Jirani Hana nguvu yoyote,kila mtu anapambana kitu kiingie kinywani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishawahi kuota pia mama yangu yangu amepata tatizo.
Nimeamka sikujua Ni tatizo gani ila yale mawazo yakawa yananijia Tena na Tena,
Nikawa napata alert kichwani kwamba Kuna kitu lakini nikapuuzia sikufanya lolote..nadhani ujinga wangu pia ulichangia

Ule mwaka mama yangu alipata matatizo,yaani siji kusahau.
Ni Mungu tu alitenda.

Mwaka Jana december pia nimelala nikawa naota nyumbani, naona km Kuna kitu kibaya kitatokea na kitamuathiri mama.
Asubuhi nilivyoamka Yale mawazo yakawa yananijia Tena...nikasali.
Baadaye nikatulia kusikiliza mawazo yatakayonijia baada ya maombi.
Kuna mstari ukaja akilini nikashika Bible nikafunngua palepale ulipo ilikuwa habakuki nadhani.
Nikamtumia mama message nikamwambia asali, nikamwambia simama kwa miguu yako..usisubiri mtu akusalie.
Kweli haikupita wiki Kuna mtu mbaya alienda nyumbani..lakini lilipita.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtumishi ktk ubora wako [emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ela za ndagu hizo.Huu utajiri gani bora niwe maskini


Kuna mzee na akili zake bosi tu mkubwa ye anakunya pembeni sio kwenye choo halafu hayaondoi au hasafishi yeye kuna mdada amemuajiri ndo anayasafisha na anamlipa kwelikweli na amekaa nae mda kweli yaani ukitaka ugombane nae yaani mzingue huyo mdada uone au mchokoze au mletee chokochoko huyo mdada ila nikajua tuu haya ni masharti



Nishawahi kuwa dereva wa coaster Fulani hivi baada ya kutoka route narudisha coaster tunapopaki kwa boss kwa ajili ya kesho siku nyengine boss anakwambia umuendeshe mtoto wake ana matatizo ya akili (taira) boss anataka tu umzungushe mpaka afurahi acheke kwahyo utakuta siku hyo tunazunguka na Costa mpaka basi hapo umechoka kichizi dogo akisema kata pale we Fanya hvyo sjui nyoosha we Fanya hivyo ili mradi afurahie mzunguko acheke tu baadae usiku tunarudisha Costa tunamshusha dogo kwa boss hapo boss lazima atutoe mshiko kidogo kisa cha kufukuzwa kazi hapo siku hiyo tumerudi mi na konda wangu boss akasema mzungushen dogo ukicheki siku hyo tunawahi mpira usiku nakumbuka ilikuwa Manchester derby tulikasirika kweli kwakua ni boss tukasema poa


Basi dogo akapanda tukaondoka naa tukaendesha tukafika karibu na bar maarufu tukamuacha ndan kuchek Mpira dogo alilia mpaka akatoa kamasi hadi utee daah si wapuuz mpira umetukolea dogo anataka azungushwe baada ya mpira tukamrudisha nyumban nashkuru mungu alikaa mulemule ndani ya gari akatoka maana angetoka akapotea aisee

Tunafika nae boss anamuona ametoka kulia hadi kamasi alijua tu ni mpira huo ndo umetuchanganya akasema kesho nisiwaone hapo ikawa ndo imetoka hivyo ila nashkuru nikapata dayworker ya haice
Kuna jamaa flani nilishawahi kufanya naye biashara. Kwa kweli jamaa nilikuwa namuuzia mzigo mkubwa sana. Tulifanya biashara nzuri sana.

Baadae jamaa akajipanua sana akafungua matawi ya biashara yake, akanunua usafiri wa kutembelea, akaoa na akapata mtoto.

Siku 1 nimekaa maeneo ya baishara yangu nikamuona jamaa anapita upande wa pili wa barabara anachechemea kama mtu aliyeumia kwa kunyaga kitu chenye ncha kali.


Marafiki niliokuwa nimekaa nao wakaanza kumuongelea yule jamaa kwamba pesa zake ni za kishirikina, na pesa zake ziko kwenye kidonda mguuni kinachomfanya anachechemea.

Nikawauliza mnamfahamu na pesa ziko kwenye kidonda kivipi?

Majamaa wakaniambia yule jamaa kuwa anatajirika na kufilisika, alishawahi kumiliki costa daladala 4, magari ya kutembelea, nyumba, na kituo cha kuuza mafuta halafu akafilisika akafungua genge la kuuza nyanya nk.

Wakasema kile kidonda chake kikianza kuuma anaanza kufilisika anapoteza kila kitu anajifungia ndani hata miezi 3 anaugulia maumivu tuu hataki kwenda hospital anaomba mnunulie panadol, kutuliza maumivu.

Kidonda kikipona tuu anaaza kushika pesa nyingi za kufa mtu. Yule jamaa nilianza kumfuatilia kibiashara. Tuliendaa baadae akaacha kununua mzigo akaanza kuuza biashara zake, nikimuuliza kulikoni anasema anataka kubadilisha biashara.

Uza usafiri wake, uza pikipiki alizokuwa amewapa bodaboda wamletee pesa. Jamaa kutembea shida kidonda kimebamba moto, mke mtoto wakamkimbia, alikuwa bonge akakonda baraaaa, ukikutana naye anaomba pesa ya kula.

Baadae akatoweka kabisa. Alikaa muda kweli akarudi yuko vizuri kabisa pesa zimeanza kumchanganyia tena. Kwahiyo huyu jamaa kazi yake ni kutajirika kufilisika kutajirika kufilisika

Sent using Cash Money Wings

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tomino's Hell ni Shairi Ambalo Unaambiwa Hutakiwi Kusoma Kwa Sauti!, Soma Kimya Kimya na inaelezwa Ukisoma Kwa Sauti Shairi hili Kuna Mawili, Either Utakufa au Utapambana na Mauzauza Katika Maisha Yako!. .
.
Shairi Hili Liliandikwa Mwaka 1919 na Mwandishi 'Saijou Yaso' Raia wa Japan na Wakati Anaandika Shairi hili Alikua na Umri wa Miaka 26 tuu, Inaelezwa pia Mtu Huyu Hakuwa Mtu wa Kawaida!. .
.
'Saijou Yaso' Alikua Mwandishi Maarufu sana wa Mashairi Kutoka Nchini JAPAN, Alizaliwa January 15, 1892 Huko Tokyo Japan na Kufariki August 12, 1970. .
.
Shairi Hili Linamhusu Mtu Mmoja Anaeitwa 'Tomino', Tomino Alikua Anasafiri Kwenye KUZIMU!. Mwaka 1974 Muongozaji wa Movie wa Kijapan 'Terayama Shuji' Alitaka Kutengenezea Movie Shairi hili, Ajabu ni Kwamba Miaka Michache Baada ya Movie Kutoka ALIKUFA!. Movie Inaitwa 'To Die in the Countryside'. .
.
Je Kwanini Shairi Hili Linatisha? Kwanini Lazima Usome Kimya Kimya? na Je Huyu TOMINO ni Nani? .
.
Kuna Story Nyingi sana Kuhusu Mtu Huyu 'Tomino' Aliyeandikwa Katika Shairi Hili, Kuna Siri Kubwa isiyojulikana Kirahisi Kumhusu Mwandishi huyu ambaye Inaelezwa kuwa Hakuwa Mtu wa Kawaida!. .
.
Hiki ni Kipande tuu cha Shairi la Tomino, Kuna Lugha Tatu Tofauti Hapa, Liko Tlanslated.

姉は血を吐く、妹(いもと)は火吐く、
ane wa chi wo haku, imoto wa hibaku,
His older sister vomited blood, his younger sister vomited fire,

可愛いトミノは 宝玉(たま)を吐く。
kawaii tomino wa tama wo haku.
And the cute Tomino vomited glass beads.

ひとり地獄に落ちゆくトミノ、
hitori jigoku ni ochiyuku tomino.
Tomino fell into Hell alone,

地獄くらやみ花も無き。
jigoku kurayami hana mo naki.
Hell is wrapped in darkness and even the flowers don't bloom.

鞭で叩くはトミノの姉か、
muchi de tataku wa tomino no ane ka,
Is the person with the whip Tomino's older sister,

鞭の朱総(しゅぶさ)が 気にかかる。
muchi no shubusa ga ki ni kakaru.
I wonder whose blood is on it?

叩けや叩きやれ叩かずとても、
tatakeya tatakiyare tatakazu totemo,
Hit, hit, without hitting,

無間地獄はひとつみち。
mugen jigoku wa hitotsu michi.
Infinite Hell's one road.

暗い地獄へ案内(あない)をたのむ、
kurai jigoku e anai wo tanomu,
Would you lead him to the dark Hell, .
.

KIRANGA KAMA UNAJITIA UBISHI WA KISHABIKI EMBU FANYA HIKI KITU ARAFU ULETE HAPA MREJESHO..[emoji102]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasilisha kama ilivyosimuliwa :

Kuna mwalimu Shule X, huko kanda ya ziwa, aliamka saa tisa usiku kuwahi usafiri asubiri gari kwenda mjini, kijiji cha ndani huko mkoa mpya uliopo ziwani.

Akasubiri gari na baada ya mda likaja, akasimamisha na kuingia. Gari ikaondoka, kakaa baada ya mda kumcheki abiria mwenzake kainama, akahisi labda ni usingz, lakini alipocheki waliopo nyuma pia dizaini kila mtu kainama. Akaona isiwe shida akamsemesha jamaa kainama tu kwa siti yake.

Sasa na yeye akatulia, gari imeenda lakini ghfla kama kausingz kakamwingia, akshtuka ghafla ni saa kumi na mbili asubuh na amesimama pale pale alipokuwa saa tisa kituoni.

Akapanic, kachukua baiskeli hadi wilayani hakurudi tena, ikabidi afisa elimu aende kule na timu yake kuongea na waalimu na wananchi ila jamaa hakuweza kukubali kurudi kituoni. In short walimpa uhamisho.

Nyingine mwalimu kapangiwa kituo Shule X huko kanda ya nyonyo. Kama ujuavyo vita ya kugombea mwalim binti mpya kati ya wanakijiji na wafanyakazi wenzake. Kumbe akawa kawakatalia, ikawa nongwa!

Siku moja anaosha ndizi kamaliza vizuri kwa sufuria, ghafla kikashuka kinyesi kingi kika replace ndizi zote, kinyesi fresh kinatoa hadi Moshi. Madam yule alikimbia kwenda kwa Bro nae ni mwalimu jirani Yake. Hakurudi tena kwa ile nyumba anaogopa.

Nina visa kama 10 kidogo ila mzembe kuhadithia.

Haya Mambo yapo kanda ya Nyonyo hasa kwa tuliokulia Bush huwa hata hatutetereki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shuhudia nguvu za MUNGU sio shetani
 
Back
Top Bottom