kijiweni jr
Member
- Dec 23, 2019
- 19
- 55
Hahahahaha umenichekesha sana mkuuILE SARE WALIYOTOA YANGA NA SIMBA.WALIIPATAJE!!!
mkuu tunafanana sana:
Mimi mwaka 2010 wakati npo chuo cha cbe dar mzee wangu alikua anaumwa amelazwa muimbili hospital.
Ilikua Mara kwa Mara haipiti wiki lazima nimuote mzee wangu amefariki,basi nlikua nalia sana tena sana ukumbuke nipo ndotoni nikistuka najikuta ninamachozi mengi sana.
Basi nikiamka tu lazima niende hospital kuakikisha je amekufa kwel au laa lkn nlikua namkuta mzima.
siku namaliza tu mitihan ya mwisho ndo siku hiyo hiyo amefariki hakika nililia sana tena sana.
KUHUSU MAONO NDOTONI
Mimi Nina staili mbili za kuota nikiwa nimelala.
Huwa naota kwa kuona tukio kamili lkn pia huwa naota kwa kusikia sauti ya mtu masikioni mwangu akiniambia kitu.
Kuna siku niliota sauti ya mtu ikiwa IPO siriazi inaniambia kwa umakini kabisa kua utaenda kua manager katika kampuni hii theni nikaanza kuoneshwa laivu mazingira ya hiyo kampuni.
Nilivostuka niliomba mungu iyo ndoto na iwe kwel maana nilikua kweli sina kazi ya kuajiriwa naendesha bodaboda yangu.
Ikapita kama miezi mitatu mbaka nishaanza kusahau hiyo ndoto siku moja natoka kwenye interview ya kampuni flani dar wakat nipo chalinze baba yangu mdogo akanipigia simu akaniambia upo tayar kuajiriwa nikamwambia ndio mzee akaniambia nitumie CV yako kuna MTU nimtumie
Nlivotuma baada ya wiki nikaitwa kusailiwa nikaambiwa wiki ijayo niende kuanza kazi tanga.
Huwezi amini nilivofika mazingira ya pale kwenye ile kampuni ndo yaleyale ambayo niliyoyaota nankuoneshwa kwenye ndoto ambayo ilitokea zaidi ya miezi mitatu nyuma
Nilishangaa sana kwa kwel.na mengine mengi tu sitaki kuwachosha na wengine wachangie
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naogopa na huu uzi wako umechochea hali hiyo najuuta kuusoma maana mauza uza mengi yaliyosimuliwa nikiwa peke yangu hasa usiku kama nayaona yote
Kigoma ndo penyewe kwa wazee wa shuguli yan wacha kabsaMkuu naogopa na huu uzi wako umechochea hali hiyo najuuta kuusoma maana mauza uza mengi yaliyosimuliwa nikiwa peke yangu hasa usiku kama nayaona yote
Niko Kigoma
Mkuu sio kigoma hyo kweli!! mana nikikumbuka yaliyonikutaga Op "kilimo kwanza" !! yan hayasimuliki!!Mwaka 2006 nipo Depo mkoa fulani, tulikuwa na utaratibu makuruta kwenda lindo usiku, na zamu ilikuwa ni vyumba, sasa siku hiyo ilikuwa zamu yetu tukaenda lindo mimi na washikaji wawili ambao tulikuwa tunakaa room moja, tukamuacha mmoja analinda room yetu.
Lindo letu lilikuwa karibu mtoto mkubwa, tumefika pale mida ya saa nne ilipotimu saa 7 usiku mauzauza yakaanza wale washikaji wawili wakaanza kupiga kelele kuweweseka kama vile wanagombana na mtu, "hatuji huko, hatutaki" nikawauliza ni nini hawanijibu, baadae wakakimbia wakaniacha mwenyewe kwenye lindo, baadae walikuja na guard commander wakadai kuna mtu alikuwa amekaa katikati ya maji alikuwa anawaita na kuwavuta kwa nguvu.
Kesho yake tumelala chumbani mmoja wa vijana akakimbia akazima taa ya chumbani akatulazimisha wote tujifunike blanket kuna mgeni na akatoa tahadhari atakayechukungulia atakiona, baada ya dakika moja nilisikia kishindo chumbani kama mtu ameshuka toka darini, baada ya robo saa nikasikia yule kijana anaongea anamuaga mtu.
Asubuhi tumeamka kijana amechanjwa chale mwili mzima, nilipomuuliza akasema ndugu zake walikuwa wamekuja kumtenengezea dawa kutokana na masahibu ya jana yake, kijana alikuwa mtu wa Rukwa.
Story ya pili.
Tupo lindo usiku tena tulikuwa watatu tena (sio wale wa mtoni) sehemu tuliyokuwa lindo ni njia ambayo raia wa kawaida hupita wakienda makwao, sasa siku hiyo mida kama ya saa sita kuna njemba moja ilipita, vijana wakaruka nae, pigwa sana, akagaragazwa sana, mimi nilikuwa nimepitiwa na usingizi, niliposhtuka nikawakataza wale wenzangu tukamwaachia akaenda zake, baada ya nusu saa yakaanza mauzauza, walikuja bundi wawili wakatuzunguka, halafu wakaondoka ghafla wale wenzangu wakaanza kuchapwa fimbo, chapwa sana lakini hawakimbii wanalia wanaomba niwasaidie, ilibidi usiku huo tutafute wenyeji waende kuomba msamaha kwa ile njemba iliyogaragazwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu upo serious!? niruhusu nikucheki dmlabda nikupe connection ya fundi tu jamaa fundi amefanikiwa hadi kumpa mmoja wa mawaziri uwaziri ni noma huyo alafu hana tamaa ukifanikiwa ndio unaenda kumshukuru
Ni jambo la kumshukuru MunguMIMI BINAFSI SIJAWAHI KUKUTANA WALA KUONA PILIKA HIZO KABISA.........
OVA
Sent using Jamii Forums mobile app
Nakufata DM mana si kwa connection hzo aisee!!wote wanatumia nguvu za giza mkuu kuna waziri mmoja rafiki yangu nilikuta kwake kawafungia waganga kama 30 hivi anawalisha kila kitu wamtengeneze mambo yake yawe mazuri na kweli amefanikiwa jiwe anamsikiliza hatari japokua jamaa ni bogus tu
Mimi na mshkj wng niliwahi kuenda kwa mtaalam mmoja nilimsindikiza uyo mshkj wng mimi nilikuwa sina imani na nguvu za giza insuch kipindi iko afu nilikuwa mbishi, sas bana yule mzee alisema kimasihara kuwa kuna dawa nikiwapa unaona wachaw na majin usiku, mshkj wng aliogopa akaikataa mm kwa kiherehere changu niliiomba uku nikijichekesha nakudhan ni mchezo wa kuigiza. Alinipa akaniambia hii utaoga usiku alafu na hii utaipaka kabla ya kulala afu hii kesho asubuhi utaogea na kupaka ili kuiondoa iyo hali ya kuendelea kuona ila sharti ni moyo usizungumze chochote pindi utakapokuwa uona ukizungumza utajijengea mazingira ya uadui..nikakubali, Haha ayse yanii ule usiku siusahau kwa vituko nilivyokuwa naviona dunia ina mambo mengi nyiny zaidi ya unavyoiona..
Sent using Jamii Forums mobile app
MkuuTukio LA kweli
Kisiwani kome ziwa Victoria mkoani Mwanza.
Baba yangu mzazi alitoka Mwanza na mkewe mama yetu mdogo wakaelekea kisiwani kome kutafuta mahali pazuri pa kufanya biashara na shughuli za uvuvi,walikuwa wanamiliki boti na wanafanya kazi wakiume kwa ajili ya kazi za boti,na alikuwepo mama mmoja aliyekuwa mpishi katika hiyo kambi ya faza...sasa Mimi na Dada yangu tukapelekwa kuishi na faza huko kisiwani sasa mambo yakaanza...
Jirani ya kambi alikuwepo Mzee mmoja anaishi umbali kidogo na kambi yetu,nyumba Yake ilikuwa katikati ya migomba palikuwa panatisha balaa mchana lakini kulikuwa na giza kama usiku,kumbe yule Mzee ni mchawi Wa kutupa,akajifanya rafiki mkarimu na kina faza...hadi sisi tukawa tunapenda kwenda kwake kuchukua pilipili,ndizi na viazi...akiondoka anaacha ujumbe pale kambini watoto waje kuchukua viazi tunaenda.
Huyu Mzee alikuwa muumini nzuri Wa kikristo akawa anaenda kanisani kila jumapili hakosi.
Sasa kumbe yule Mzee alikuwa anampenda yule mama mpishi,kila akimwambia yule mama akawa anamkataa hamtaki kwa kuwa ni Mzee..sasa alichokifanya akatumia uchawi wake kumpata yule mama mpishi wetu kambini.
Siku moja jumapili Mzee akapita pale kambini akasalimia huku akiwa kwenye furaha kubwa sana ikionekana dhahiri usoni,akamwambia yule mpishi nenda nyumbani ukachimbe viazi mimi naenda kanisani..akamuelekeza na matuta kabisa..kumbe alikuwa ameshatega mitambo Yake...yule mama kufika bahati nzuri au mbaya alikwenda peke yake hakuenda na sisi maana tulikuwa tunatembea nae kama mkoba.
Sasa alipofika akaanza kuchimba viazi kupiga jembe LA kwanza nyoka akamgonga mguuni..ile anajaribu kukimbia akamgonga tena kisha akapotea..mpaka Mara tatu akawa anapiga kelele kuomba msaada lakini wapi hakukuwa na MTU eneo lile au watu kusikia na kwenda kumsaidi mpaka akaamua kurudi kambini wakamfunga kitambaa ili sumu isipande mwilini na kusambaa...wakaja waganga wakienyeji kama watano kila mmoja anafanya utaalamu wake anashindwa mpaka akaja mganga Wa mwisho akampima kwa kutumia SAA ndogo..akasema mgonjwa ameshafariki kitambo sana,watu walilia sana,na yule Mzee alikuwepo anajifanya anatoa msaada kama msamari mwema.
Ikabidi maiti isafirishwe kwenda kuzikwa Mwanza mjini ,tulipanda boti na maiti kuelekea mwanza....kufika katikati ya ziwa mafuta yakaisha boti likaanza kupelekwa na upepo hovyo hovyo watu wakaanza kuomba dua zote mungu atuokoe maiti ifike salama na roho hai ziokoke!!!,Mungu saidia ikapita boti ya kishimba,wakaipungia mkono kwa mbali ikaja karibu na boti yetu..bahati nzuri faza aliwahi Fanya kazi na maboti hayo wakatusaidia mafuta ..tukafika salama mjini,maiti akazikwa salama msiba ukaisha.
Sasa baada ya siku kupita yule mama akawa anaonekana kwa yule babu mchawi wanaishi pamoja kama Mke na mume,ukimshitukia ukamuona yule mama anapotea...mpaka Leo sijui maisha yao yaliendelea vipi kichawichawi,kama walisha kufa au wapo hai Mungu ndiye mjuzi.
N.B
Ila Mzee alijipatia Mke kwa njia za kishirikina au giza!!!
Ndo nini hicho mkuu unaweza kuelezea kidogo kama usipojalcase ya pili deja Vu.
Umekomalia Kigoma tu!!! Ushaambiwa ni Tanga.Ndiko wanasifu kuna waganga hatari kama Juma Njemba (RIP) wa kigoma?
Sent using Jamii Forums mobile app
Anzisheni uzi wenu, mnaharibu uzi. Ngozi nyeusi ni tatizo la Dunia.Una mapepo makali sana. Aiseee...povu limekutoka sana.shida nini hasa? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna watu siyo waelewa kabisa!Upande wa Giza unatambua sana maana ya mzaliwa wa kwanza,kitu ambacho watu wengi hawajui.
Mzaliwa wa kwanza ni Lango La kiroho.vitu vizuri au vibaya katika familia ni lazima vipitie kwake.
Mwanzo 49:3
Reubeni u mzaliwa wangu wa kwanza,nguvu zangu na malimbuko ya uwezo wangu. Umewapita wengine kwa ukuu na nguvu.
i. Amebeba nguvu nyingi za familia.
ii. Amebeba Baraka za aina mbalimbali za wadogo zake.
iii. Amebeba nguvu ya upendo ndani ya familia.
iv. Mzaliwa wa kwanza ni lango, Zab 24:7-9, ambapo Baraka zote za familia kutoka mbinguni zinapitia kwake na kuwafikia wadogo zake wote.
v. Amebeba ustawi wa familia kiroho na kimwili.
Pitia na mistari hii pia itakufungua zaidi juu ya hili.
Kutoka 4:22-23
Kutoka 12:12-13
Yeremia 31:9
Mwanzo 21:9
Mwanzo 25:29-34
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kweli mkuu. Deja vu sio ndoto. Hii ni ile hali ambapo tukio linatokea na wewe kuhisi kuwa sio mara ya kwanza kuona, kusikia ama kufanya jambo hilo (hauwezi kukariri muda wa tukio isipokuwa hisia zinakutuma tu kuwa kitu kimewahi kutokea, kwamaana nyingine ni kuwa hisia huja wakati wa tukio halisi kutukia ndpo deja vu hutokea) kesi ya msimuliaji ni tofauti, yeye aliota ndoto.case ya pili deja Vu.
Mkuu upo serious!? niruhusu nikucheki dm
Huyo jamaa alikuwa ni MchawiWataalam nina swali hapa kuhusu mambo haya tunayojadili
Kun mdau huko nyuma kaeleza kuhusu mwanafunzi mmoja kufanya mapenzi na wasichana karibu mabweni mawili usiku bila wao kujitambua. Je, huyo alikuwa mchawi au ni mtu tu wa kutumia madawa?
Halafu swali ambatatano;
Nasikia kuna watu wanatumia madawa kutongozea wanawake (yani anampata mwanamke yeyote anaemhitaji kupitia madawa)
Je, hii sayansi ipo ama ni fix?
Yani mwanamke yeyote kabisa?
Sent using Jamii Forums mobile app
Npo kigoma hapohapo ukiyaona nambie nijeMkuu naogopa na huu uzi wako umechochea hali hiyo najuuta kuusoma maana mauza uza mengi yaliyosimuliwa nikiwa peke yangu hasa usiku kama nayaona yote
Niko Kigoma
Umeona ugongelee msumari kabisaKigoma ndo penyewe kwa wazee wa shuguli yan wacha kabsa
Sent using Samsung s10
Asante kwa kujali mkuu ila tu napata tabu haswaa mida ya usiku