Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kutoboa biashara.
1. Kuwa mbunifu kuja na idea ya biashara unayoipenda na yenye uhitaji, acha ujinga wa kufuata mkumbo kufanya biashara fulani kisa umesikia inalipa.

2. Usiwe na akili mgando kusubiri wateja waje uwauzie tu kisa wewe mwamba una mtaji na bidhaa zipo dukani, jifunze sales and marketing.

3. Usiwe na akili mgando kupata faida bila kufanya saving yoyote. Jifunze elimu ya fedha na siyo ujuzi wa kuuza tu bidhaa na kurudisha chenchi.

4. Usiwe na akili mgando kufanya biashara moja na kutegemeana kwa asilimia mia moja kiasi kwamba huna back-up yoyote in case biashara hiyo ikiyumba, hapa ndo dhana ya ndumba inapoanzia na kuwa na akili kama za mtoa mada.

5. Acha kuwa na akili mgando kufuata kila ushauri wa kibiashara au kimaisha unaotolewa Jf, wengine humu wana matatizo kuanzia ukoo wa babu zao hivyo matatizo hayo yanaama ukoo hadi ukoo.

Wenye akili za mkumbo wote huwa fursa kwa wanaojielewa. Chunguza utagundua.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nikishapata experience kwa kushuhudia hata uje na makontena ya ngonjera sikusikilizi kamwe. Nimeshuhudia watu wanapigwa kipapai alafu mtu atoke uko aniambie hakuna uchawi, atahangaika sana.

Mimi nitajikinga tu na wabaya, hayo mambo ya kuongeza mvuto siyaamini lakini kwenye kudondoshana siwezi kubali unipoteze. Nitatafuta ngome ya kulipia na isiyo na complications. Na nitasali sana na kutoa sadaka. Ukinambia ni ushetani hayo unayajua wewe, kwani wapi Mungu alisema tupulize ubani. Mbona raia wanapuliza, wanavaa sare, wanafanya rituals za kidini.

Sidhani kama kuna mganga atanambia mkane Mungu nikupe dawa.
 
Fanya hivi, tumia dawa hizo uite wateja utajirike na ala usije hapa kutangaza biashara
 
Upo sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha ajabu mkuu kuna baadhi wanafuata hizo njia na wanatumia kimzizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha ajabu mkuu kuna baadhi wanafuata hizo njia na wanatumia kimzizi

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikatai mkuu ila suala la kutumia mzizi ni la kiimani zaidi kutegemeana na mtu. Kama wewe ni mkristo/muislamu uliyekomaa vizuri basi fuata hizo mbinu na umuombe Mungu sana, ila kama huamini katika Mungu mmoja basi automatically utaangaukia kwenye hilo kundi la wazee wa mizizi kama hutokuwa makini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh hatare

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tembea mzee daaah hatar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…