Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mi sio mnafiki! Ila mimi Niko pamoja na Kiranga kwa sabababu majibu yake yananiingia akilini mi huwa siamini kitu ambacho huwa hakiniingilii akili mfano yesu,shetani,Petro,mMohammed,kujilipua no
Mi nahisi ni mipango
Thanks
Ili upate majibu yenye tija kwako,kwanini usifanye research kujua undani is Uchawi Exist?
Pengine itakua njia nzuri na Bora kwako kufahamu kwa mapana zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga, acha kujishusha hata kama mtu, amezikwa akiwa mzima, kuna uwezekano wa kujitoa yeye mwenyewe, kaburini. Kwa dongo lile linawekwa pale, kwa Wakristo mtu huzikwa ndani ya jeneza.
Africa sehemu nyingi sana watu wanazikwa wazima.

Kwa sababu hatuna vifaa vya kupima watu vizuri kuhakiki kwamba wamekufa.

Kifo chenyewe unajua kwamba kibaiolojia kina maana nyingi? Kuna kufa ubongo, na kufa moyo, sasa wewe unapoongelea mtu kafa, umempima vipi mpaka kujua hyu kafa?

Visa vingi ni vingapi? Una jina la mtu unaweza kunipa tuchunguze zaidi habari zake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga, acha kujishusha hata kama mtu, amezikwa akiwa mzima, kuna uwezekano wa kujitoa yeye mwenyewe, kaburini. Kwa dongo lile linawekwa pale, kwa Wakristo mtu huzikwa ndani ya jeneza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nipo chini kabisa, kujishusha zaidi ya hapo siwezi.

Kama uliniweka juu niombe radhi kwa kunipandisha.

Do not attempt to censor me on the basis of kujishusha.

Kama unazika mtu bila kuwa na uhakika kama kafariki, akizinduka utajuaje kazinduka baada ya kufa?

Kufa ni nini?

Unahakikishaje huyu kafa?

Unaelewa tofauti za mtu kuwa brain dead na mtu kuwa heartbeat dead?

Huko Tanzania mnapima vipi na kuhakikisha huyu kafa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimepitiaaa storiii na vitimbiii vya watuu kwanzia mwanzo mpaka mwishoo na mm nisipotoaa changuu nahisi nitakua cjautendeaaa hakiii huu uzii

Anyway ngja nianze kutiririka,

Mwaka 2016 wakatii npo kidato cha nne kuna jioniii moja iviii ya mwezi wa 9 nilikua zangu prep (kama ujuavyo shule nyingi za boarding hii ki2 ni must) sina hili wa lile npo zangu nakula 'muscle' kama ujuavyoo hii miezi inakuwaga karibia na necta hivyo basi shamla shamla za maandalizi zinakuaga nyingiii

Basi bhana wakt Naendelea kula 'muscle' kat kat ya prep kichwa kikaanza kuniuma kwakua haikua kawaidaa nikapuuzia asa muda ulivokuwa unazidiiii kwenda ndo jinsii maumivuu nilivyokua nazidiii kuya experience bac bhana kwakua ilikua uckuu sana nikajisemea mwenyewe "ngja nkalale may be kitapoa 2"

Basi bhana asubuhii palipambazuka ila cha ajabu safariii hiii kichwa kilizidiii sana kuniumaa. nakumbuka kuna rafiki anguu mmoja ikabidiii aende kuniombea permission ya kwenda hospital kwa 2nd master maana yeye ndo alikuwa anagawa ruhusa zote za kwenda hospital maana shulenii kulikua na kakidaspensary ambacho kalikuwa hakajitoshelezii kihuduma

Basi bhana mm na mshakajii wanguu 2kafkaa hadi hospital baada ya vipimo kadhaa nikagundulika kua sina tatizo lolote ila niliaambulia panado 2 na kuambiwa huenda no mchoko 2 ndo maana kichwa kinauma vile

Baada ya kutoka hospitalini hali ya kichwa kuuma ilizidiii mara 10 ya jana.safarii hii nikasema isiwe shidaa kwakua nlikua namilikii 'goroka' pale shulenii ikabidi nimpgie mama nimuelezee hali halisii, basi bhana ilinichukua dakika chache kufanya vile asa wakatii namwambia mama jinsi hali ilivonitokea akanambiaa inaonekana kuna ki2 hakiko sawa maana kuna ndoto jana aliiota ambayo haipo sawa na kuniahidiii Kua kesho ake atakuja kunichukuaa (maana shule ilipo na home palikua hakuna umbaliii sana )

Basi bhana kesho yake mapema mama aliacha mishe zake akaja hadi shule kuniombea ruhusaa,at a same time nlikua nina hali tete maana kichwa kiligonga balaa.kwenye saa 6 ivi mchana 2kafika home nikamkuta mzee nikamuelezea situation iliyonitokeaa pale shule na pia 2kapiga stori mbili tatu full utaniii nk.

Ilipofika jionii mama angu akapandisha majini (ana majini mpaka now) asa wakati anapandisha yale majiniii akataja Jina la mke wa kaka ake( aunt angu) na yale maneno ake aliyokua akiyaongea yalikua yana relate na ugonjwa wangu wa kichwa kuuma.dakika kama 20 iviii akarudii katika normal condition alikuwa anamuuliza mzee na watu wengine kua kuna nini kimetokea mbna amechafuka saana(siunajua tena m2 akiwa na majini anavyojigalagaza) baasi baadae ikabidi mzee amwambie maneno aliyokua anatamka mara nae b mkubwa akipigwa na butwaa..basi 2kaa pale mzee na mama na wakashauriiiana kwamba inabidiii keshoo asubuhiii twende kwa mtaalamuu,Aisee cku iyooo ucku ckulalaaa kichwaaa kiliumaaaa balaa

Keshoo mapema tyu 2kafika kwenye kilinge cha 'mtaalamuu' ila cha kunishangaza ile 2nafika tu mtaalamu akatuambia nishajua shida yenuu(hapa nilichanganyikiwa saana maana ckuwahi kuona ki2 kama hichoo 'live' maana Nlizoea kuona mwenye movie tyu) basi bhana wakatiii mganga anaendeleaa na mambo yakee ilipiga mvuaa ya nguvuu kama kwa robo saa 2 afu zen ikakataa wakatii alipokuwa unaendelea na mambo yake alikuwa anatuhimiza 2siogope kwaniii ni vi2 vya kawaida 2.bac bhana aliendelea na kazi ake kama kwa lisaa iviii afu akanivisha kitambaa fulaniiii iviii chekunduuu uku akiongeaa maneno 2cyoyajua baada ya kunitoa kile kitambaa cha kushangaza 2likiona kile kitambaa kimeambatana na irizii kubwa nyekundu lakn pia hapo hapo maumivuu ndo yakakata.

Nakumbuka kuna maji fulaniii ivii alinawa kwanza ndo akawa anaanza kuichana ile irizi na kiwembe ili ajue kilichomo ndani, baada irizi kufunguliwa ndani kulikua na kucha za mtoto mchanga ndani na picha iliyochorwa kaburiiii,

Akatuambia Kua ile picha iliyochorwa kaburiii maana ake ni kua nilikua natakiwa nife na akasema pia nina bahatiiii saana maana wangenichelewesha kama cku mbili ivii basi familia ingenikosaaa,pia akamtaja muhusika wa lile jambo ambaye alikuwa ni aunt angu,na huweziii aminiiiii adi leo ananichangamkiaaa kama hakuna ubaya aliofanya vile na tangu cku hiyooo mpaka Leo kwake cjawahiii kwenda hata!![emoji2955]

Aisee uchawiii upo wakuu kama unaona ni mambo ya kusadikika ngja yakukute

Wassalam










Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unapoteza muda, kuchangia mada, ambazo kunachojadiliwa wewe hukiamini na wala hakikugusi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumulika ujinga na uongo kwa elimu na ukweli kamwe hakuwezi kuwa kupoteza muda.

Kwa nini kuwe kupoteza muda?

Mtu akisema ana dawa ya ugonjwa X, wakati hana, na najua hana, nikisema huyu muongo hana dawa, hata kama siamini na kwa kweli najua hana dawa, hakuwezi kuwa ni kupoteza muda.

Kwa sababu, kutasaidia kuonesha uongo uko wapi na ukweli uko wapi.

Kama kuna watu wanaamini uongo, hata kwa kununua dawa hiyo ya uongo, watasaidiwa kujua ukweli.

Sasa hoja yako ya kwamba mtu kuzungumzia kitu asichoamini ni kupoteza muda, inaonesha si tu umekosea, bali pia inaonesha huwezi kufikiri kimantiki na hujui uthabiti wa kufikiri.

Jipange upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salange, Mimi kwenyewe nimewahi kusumbuliwa na kuumwa sana na kichwa nikiwa na umri baina ya miaka 14-16. Kichwa kilikuwa kinauma mpaka napoteza faham. Nikipelekwa hospital hawagundui tatizo. Siku moja mshua akanipeleka kwa MZEE mmoja(mtaalam). Yule MZEE akacheki vipimo,akachukua pembe ya Ng'ombe. Akawa ananichanja chale maeneo mbalimbali ya kichwa,baadae akawa anaibana na pembe ya Ng'ombe kila chale mithili ya MTU anayebana kizibo cha bic kwenye ulimi.

Baadae pembe inaachia taratibu kisha inadondoka. Kila ikidondoka kinatolewa kijiwe cheupe mithili ya goroli. Vilitolewa vijiwe 4, tangu siku hiyo mpaka Leo hii,sijawahi sumbuliwa na kichwa. Uchawi upo,asiyeamini amuombe Mungu aendelee kumpa uhai. Maana ukiwa hujafa,hujaumbika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona ma Aunt wanaongoza kwa kuloga na wengi kuliwa kimasiharaa anyway ngoja na mimi nitoe kisa changu.

Kiukweli mimi binafsi huwaga sinywi maziwa yaliyochemshwa kabisaaa yani kuanzia chai ya maziwa mpaka maziwa fresh nikinywa natapika balaa na kujisikia ovyo au hata nikisikia harufu yake.. Nilikuwa sijui sababu lakini kuna siku mama alinambia kuwa kuna aunt yangu aliniwekeaga dawa kwenye maziwa fresh aliyoleta nyumbani so niliumwa sana na kutapika sana niliponaje mama hakusema.

Lakini kuna siku niliamka asubuhi aisee home nikawa nasikia kuna harufu kali ya maziwa fresh na pale home hakuna utaratibu wa kupika maziwa ile harufu ilinikera balaa nikaanza kuwauliza home nani kaleta maziwa humu ndani aisee mzee akasema hakuna maziwa fresh humu ndani me nikatoka nje lakini harufu nkawa bado naisikia aisee kichwa kiliuma balaaa lakini baadae kidogo mzee akapigiwa simu kuwa Aunt yangu amefariki yule aloweka kitu kwenye maziwa yangu so mzee akasema inawezekana ndo sababu ilipofika kesho yake baada ya yeye kuzikwa sikusikia tena ile harufu na kichwa kikapoa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1.Tukio la kwanza.

Nikiwa Tabora Wilaya ya Urambo miaka ya 90.(1992).Nakumbuka ilikuwa ni kawaida yetu watoto wa mtaani kwetu kukusanyika na kuanza kuimba nyimbo za kwaya hasa Ulyakulu na baadhi ya nyimbo za kwaya ya Nkinga. Nakumbuka ilikua siku ya Ijumaa. Dada yangu mkubwa alikuwa kaolewa mtaa ng'ambo ya pili kutoka nyumbani. Hivyo siku hiyo aliniomba niwakusanye vijana twende tukaimbe kwake. ( kumpa kampani) alikua na shughuli ya kuandaa vyakula usku ili kesho yake watu wakamlimie shamba kwa ule mtindo wa zamani wa kualikana. Siku hizi sijui kama bado upo.

Basi bwana nikawaambia dada zangu niliokua nawafuata kuwa wawaambie marafiki zao wa kike ili tukaimbe. Zamani maisha yalikua poa sana askwambie mtu.

Basi baada ya chukula cha saa 2 usiku tukajikusanya vijana wengi tu kama 15 huku wengine wakiunga tela bila mwaliko mpaka tunafika kwa dada tukiwa zaidi ya 20. Basi tukapokelewa vizuri tukaimba nyimbo za album yote ya Ulyakulu nyimbo kama Samson, Wakati wa Nuhu n.k. mpaka hadi saa 7 usku tukamaliza basi tukaaga. Mpaka tunamaliza vijana wengine weeengi walikua wameshaondoka, hivyo tubakia mimi dada zangu 2 na watoto wengine wachache ambao tunakaa jirani sana na nyumbani. Hivyo dada akawaomba vijana 3 ambao walikua ni ndugu wa shemeji yetu watusindikize

Lakini hapo kabla wakati tukiendelea kuimba tulikuwa tukiona vimondo vikipita angani kwa kasi sn na kuonekana kudondoka kwenye msitu ambapo kuna makabuli ya kijiji. Na pembeni kidogo na huo msitu ndio kuna njia ya sisi kupita kurudi nyumbani. Mbaya zaidi wakati tunajianda kuondoka kilipita kimondo kikubwa sn aafu kikaishia tena kwenye msitu ule. Hofu ilitujaa hasa ukizingatia kwenye kikundi chetu mabinti ndo walikua wengi zaidi. Baadhi wakapendekeza tulale tuondoke asbh. Hofu ikaja wazazi hawatawaelewa hasa watoto wa kike maana hata kwenda kuimba tuliondoka kwa ruksa. Sisi watoto wa kiume tuliongozana nao km walinzi. Those days ndivyo tulivyowalinda dada zetu iwe harusi,au sikukuu mtoto wa kiume unakabidhiwa kumlinda dada yako. Akijichanganya tu unamlamba makofi km si bakora. Akiwa mkubwa unarudi kumeselea nyumbani na anakula mbarata za kutosha. Hivyo ili shemeji ampate kirahis binti lazma kwanza ajenge urafiki na kaka mtu vinginevyo manati na mawe vinamhusu.

Basi baada ya kuomba msaada wa kusindikizwa tukaanza safari. Hapo ilikuwa kama 7 :30 usiku. Hali ilikua kimya ni upepo pekee ndio ulikua unavuma. Kutoka kwa dada hadi kuikuta barabara tutakayopita kuelekea nyumbani ilikuwa dk km 10 hv. Basi tukafika kwenye kona ili safari ya kufuata hiyo barabara kurudi nyumbani ianze.

Hapo ndo tulipoanza kuona malue lue ya ajabu. Kwanza binti mmoja wa kiislamu tuliekuwa nae nakumbuka alikua anaitwa Chausiku majini yakapanda. Akapiga kelele sn akaanguka chini.
Story itaendelea punde.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom