Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kuna kipindi flani kuna hali huwa inanitokea sana, sijui ni nini hasa lakini huwa naifurahia sana!

Enzi nikiwa mdogo (primary school level) kila nilipokuwa naingia kulala, baada ya muda kidogo nilikuwa nahisi kitanda kinazunguka taratibu na nahisi kupaa kabisa!

Yani kabisa sijaingiwa sana na usingiz ile hali naihisi nikiwa bado niko active kias baadae nalala!
Baadae nilipokuwa mkubwa ikapotea!

Nilishajiuliza sana ile hali ilikuwaje inanitokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee,sijategemea kukutana na maneno kama haya,yani hii imenitokea HIVYO-HIVYO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nisimulie ilikuaje mkuu....
Ulikutana na nini??
Nilivyokuwa narudi nilikutana na mtu tu wakawaida sana ila sijawahi muona akaniuliza unahisi kitu unachotaka fanya ni sahihi?? nikamwambia sijakuelewa akaniambia umenielewa ila tu hutaki kuelewa akaenda zake niliogopa sana ila niliamini Mungu yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee,
Hii hali ya kuhisi mtu yuko nyuma yako lakini ukigeuka unakuta hakuna kitu mnaizungumziaje??


Au mtu kusikia unaitwa kabisa jina lako lakin walioko karibu yako hawajasikia na wanabaki kukushangaa nako ni ishara ya nini?

Pia hizi ndoto za kuamka na kutembea kabisa ilhali mtu bado angali usingizi nazo hazina nguvu za giza? Kuna mmama mmoja kijijini kwetu huko alikuwa anaamshwa na kutoka nje usiku wa manane na kwenda kuçhimba madawa usiku kisha anarudishwa kulala!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dizain ya kuua ( hii nilisoma sehemu sijui kuna ukweli gani )

1.Kwa kusaini hati ya kifo inakua hivi. .
From nowhere mtu anaweza kukupigia cm au hata kukuuliza tu bila simu kuwa kesho utakuepo?? Wewe Bila kujua unaeza jibu hapana sitakuepo ( labda kama hio kesho una ratiba fulani? Unknowingly Utajibu sitakuepo ..pale unapojibu sitakuepo tu tayari unakua umeshasaini hati ya kifo wewe mwenyewe. .mtu akikuuliza hivo unachotakiwa kujibu ni kuwa : ndio kesho nitakua sehemu fulani ( unaitaja hio sehemu mfano kesho saa fulani nitakua kanisani au nitakua sokoni au kwa fulani ) automatic unakua umevunja na kuharibu huo mpango/kapo cha kifo wakukuua kwani watu wakiokufa ndio hawapo na wenye uhai wapo sehemu mbalimbali

2. Kutumia nyoka ( waliotumwa kichawi lakini )
Wachawi pia hutumia sana nyoka katika kutaka kuua. Inakua hivi. Wanamtuma huyo nyoka ( wakiwa wameshafanya madawa yao ) kwenda kwenye nyumba ambayo muhusika wa kuuawa yupo .
Kama mnavojua nyoka akionekana automatic watu hutaka kumuua hapohapo. So mkimuua huyo nyoka tu mnakua mmemuua huyo mtu alielengwa kuuawa kichawi. Kiuhalisia huyo mtu Anaeza asife hapohapo lakini ipo siku atakufa tu mtake msitake. So wengine husema kuwa ili kuepuka hili kemeeni kwanza pia hutakiwi kumuua huyo nyoka kitu ambacho ni kigumu sana na Sidhani kama Inawezekana kumuona nyoka nyumbani msimuue sijui inakuaje hapo na ukiona unaota manyoka nyoka mara nyingi kunakua na roho ya kishetani /kichawi inakufatilia

3. Kutumia vitu hivo vitu wakishavichukua huenda kuvifanyia dawa huku wakinena na kufanya mambo yao ya kichawi

So sometimes hawa wadudu wadudu pia hutumiwa (hii nilishuhudia kwa dogo) japo nyoka hupendelea kutumia zaidi ndiomana wengine wakiona nyoka na kukemea/ kusali / kuomba gafla huyo nyoka hupotea Saint anne

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei hutofautiana na matumizi,muda pamoja na afya ya (kijakazi) ndilo jina analoitwa kokote kule Mchawi ataitwa Mshirika na msukule anaitwa (Kijakazi)
Kuhusu Bei sijui nimeacha tangu 2018, Nachojua bei hutofautiana kulingana na hadhi au Nini alichonacho (Nyota)

Kuhusu kiwango cha pesa nilichokua nanunua hapa mkuu nitakukwepa kujibu .

Kwa shughuli za shamba Ni vigumu kujua wanalima wangapi na hawaruhusu ujue unalipa pesa mnapeana muda kazi yako Ni kukagua tu,mm nlinunua mmoja na siku kumaliza muda mrefu niliwafata wamchukue

Kuhusu shamba si kulima tu,baadhi ya shugul za shambani watafanya,mfano mzuri nenda siku ya gulio Matombo au kipindi Cha mavuno,angallia mabosi wanaokuja kuleta au kuchukua mzigo ,Kuna vibarua hua badhi yao huja nao ukiwachunguza kwa umakini utagundua Ni wale ambao tunasema wamekwisha kufa lakini bdo wanaishi.

Binafsi sijawahi kuwafuga Wala kuishi nao ila nachojua Mchawi kuwalaza hata mtaroni haoni kwake hasara ,hawana mahala sahihi kwa kuwekwa ila utakapoenda kununua wapo ktk vyumba wanafungiwemo humo


Si kila kitu ktk kilimo watafanya,shughuli nyingine zinahitaji Maarifa si nguvu,lengo la kutumia hawa vijakazi Ni urahisishaji wa kazi,na gharama nafuu

Ufanyaji wa kazi hutegemeana na Aina ya kazi,kilimo hakiwezi kufanywa mchana, muda mzuri Ni kuanzia saa sita usiku Hadi 11Alfajiri

Vijakazi Ni binadamu,Kama wengine huhisi,hutafakari,hung'amua isipokua uwezo wa kujinasua Ni mdogo kwao,wametekwa Ni watumwa it's hard to them to escape,if wakinyimwa chakula mazingira si rafiki,afya kuzorota huchangia vifo vyao.


Mkuu

hawa misukule huwa wanaumwa?

Naje wakifa wanazikwa?

Pia mwenyewe akifa inakuwaje?

Je kuna wachawi ambao hawaoa misukule wao au kuolewa na misukule?

kuna misukule wazungu au foreigners?

Watoto wadogo misukule hua wanakua wakubwa?
 
Kweli aisee. .Halafu kwa huyo mtoto wa dogo wangu shangazi yake alikiri kuwa angeenda kumtunza akamlea mpaka atakapokua umri fulani angeanza kumtumia kwenye shughuli zake. .sasa Sijui angemuua ile kumuaa kichawi au angemchukua tu kimazingara. ..
God forbid.

Cc Smart911
Bila ujasiri pengine asingepata mtoto wake tena.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilivyokuwa narudi nilikutana na mtu tu wakawaida sana ila sijawahi muona akaniuliza unahisi kitu unachotaka fanya ni sahihi?? nikamwambia sijakuelewa akaniambia umenielewa ila tu hutaki kuelewa akaenda zake niliogopa sana ila niliamini Mungu yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ooohh Zaburi 91:11-12

Imeandikwa

"Kwa kuwa atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote"
Mikononi mwao watakuchukua usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe"

Mungu hakutaka ujikwae mguu wako katika jiwe.
 
ila inategemea unatabiri kwa jina la nani na unatumia nini?? Kama mtu anatabiri kwa jina la Yesu hakuna shida kabisa.....maana hakuna uhusiano direct WA nguvu za nuru na giza

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanatumia jina la YESU huku wamevaa hirizi

Kwa mfano wako huo unadhan manabii wote waliojazana hapa dar na mikoani wametumwa na Mungu kisa wanatumia jina la Yesu?

Mm nawajua wengi ni matapeli na wanatabiri na kufanya miujiza kwa jina la Yesu
 
Wazee,
Hii hali ya kuhisi mtu yuko nyuma yako lakini ukigeuka unakuta hakuna kitu mnaizungumziaje??


Au mtu kusikia unaitwa kabisa jina lako lakin walioko karibu yako hawajasikia na wanabaki kukushangaa nako ni ishara ya nini?

Pia hizi ndoto za kuamka na kutembea kabisa ilhali mtu bado angali usingizi nazo hazina nguvu za giza? Kuna mmama mmoja kijijini kwetu huko alikuwa anaamshwa na kutoka nje usiku wa manane na kwenda kuçhimba madawa usiku kisha anarudishwa kulala!



Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo kama Kisa changu hapo juu haya makitu ya kuitwa usiku jina kutembea huku umelala mpaka Leo naamini ni mauzauza sio hali ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliambiwaga Ukisikia kuitwa hivo especially usiku ukiwa umelala usiitike ( unaeza kuta ni wachawi wanafanya manyanga yao huku wanakuita jina lako ukiitika tu kitu kitu kibaya lazima kitakutokea) ..au kama ni usiku wa kawaida tu mkiwa ndani ukasikia mtu anakuita nje ya mlango subiri mpaka akuite mara tatu badae ndio uitike . Sijui imekaaje hii

Cc Smart911
Wazee,
Hii hali ya kuhisi mtu yuko nyuma yako lakini ukigeuka unakuta hakuna kitu mnaizungumziaje??


Au mtu kusikia unaitwa kabisa jina lako lakin walioko karibu yako hawajasikia na wanabaki kukushangaa nako ni ishara ya nini?

Pia hizi ndoto za kuamka na kutembea kabisa ilhali mtu bado angali usingizi nazo hazina nguvu za giza? Kuna mmama mmoja kijijini kwetu huko alikuwa anaamshwa na kutoka nje usiku wa manane na kwenda kuçhimba madawa usiku kisha anarudishwa kulala!



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanatumia jina la YESU huku wamevaa hirizi

Kwa mfano wako huo unadhan manabii wote waliojazana hapa dar na mikoani wametumwa na Mungu kisa wanatumia jina la Yesu?

Mm nawajua wengi ni matapeli na wanatabiri na kufanya miujiza kwa jina la Yesu
Hivi kuna watu bado mnawaamini hao manabii( wafanyabiashara) ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hii ya kuhisi mtu yuko nyuma yako inakuwaje?

Halafu excel anakusalimia sana!
Niliambiwaga Ukisikia kuitwa hivo especially usiku ukiwa umelala usiitike ( unaeza kuta ni wachawi wanafanya manyanga yao huku wanakuita jina lako ukiitika tu kitu kitu kibaya lazima kitakutokea) ..au kama ni usiku wa kawaida tu mkiwa ndani ukasikia mtu anakuita nje ya mlango subiri mpaka akuite mara tatu badae ndio uitike . Sijui imekaaje hii

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Mimi sijui wanavyotengeneza wala sijawah itumia ila nishawah kuwa na company ya marafiki wanayoitumia


Cha kukusaidia tu tafuta mmasai anaeuza dawa za asili muulize atakupa info kuhusu ndere ilivyo kuwa mdadisi tu
MM naomba unifafanulie kuhusu ndele.
Inatengenezwaje? Inatumikaje baada ya hapo? Je kuna manuizi?

Sent using Jamii Forums mobile app
m

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Honestly unazidi kunipa curiosity ya kujua kilichotokea
Ilikuwa kipindi Niko shule,ndoto za kifo zikawa zinanijia Ila Mara napotezea...
Sometimes nikikaa mawazo yananijia kwamba uliota ndoto hii..nikawa sitilii maanani ukizingatia kipindi hicho bado umri mdogo na nilikuwa sijakomaa Sana kiimani.

Nikawa Tena napata mawazo ya nguo, yaani Kama ndoto inanijia dadangu ameshona nguo yake halafu ikapotea(Dada yangu alikuwa fundi cherehani)

Nimerudi likizo mwezi June nikaambiwa dada kihoma kinamsumbua.
Nikafunga safari kwenda kwake kumsalimia...hakuwa serious Sana yaani ilikuwa homa ya kawaida tu alienda hospital wakampima wakakuta ana typhoid,wakampa dozi ya typhoid.
Bado aliendelea kuugua ,akaenda hospital nyingine akapimwa akaambiwa vidonda vya tumbo.
Huo Ni mwezi June.
Hali ikazidi kuendelea..

Yale mawazo yakawa yananijia Tena lakini masikini sijui Ni kutokutambua au utoto,nikawa siyatilii maanani.

Mwezi huo huo akapelekwa Tena hsp akakutwa na tatizo la figo,japo alikuwa fiti tu,hajawahi kuugua ugonjwa wa Figo nyuma,familia hazina historia za magonjwa hayo,kwamba ana HIV hakuna..ilikuja tu from no where.

Tukawa tumeanza maombi,
Binafsi nikaanza maombi kwa ajili yake.
Shida ikawa upande wa mume,wakampeleka kwa waganga wa kienyeji..wakawa wanaambiwa maneno mengi,mwingine anasema Mara fulani alikuroga ,mwingine fulani (dereva)amekuroga,,Huyo dereva alikuwa dereva wa gari la familia la biashara,baada ya kuona anaingiza loss sana akapokonywa gari na likaenda kupakiwa pale nyumbani kwa dada maana Yeye ndiye alikuwa msimamizi wa hayo mapato.
Alipogundulika na Hilo tatizo alianzishiwa tiba ya hosp.

July Mimi nikarudi shule nikimuacha Dada yangu anaendelea vizuri,shida ikawa hiyo michanganyo..Mara waganga,Mara maombi na hosp.

Kuna mtumishi aliongea naye akamuombea akafunuliwa hayo ya nguo.
Kipande Cha nguo kilichukuliwa kikaenda kufanyiwa Mambo huko na kikazikwa.

Nilijitahidi weekend moja kuomba ruhusa na kurudi kumuona dada ..ilikuwa October..nikakuta Hali yake SI nzuri.

Baadaye naye alichoka Yale madawa ya kienyeji ..nilirudi hiyo siku nilikuta wametoka hsp kufanyiwa dialysis.. Hali yake ikazidi kuwa mbaya..
Alinambia mdogo wangu nashindwa kula,nashindwa kuongea vizuri,nashindwa kutembelea,niombee

Niliomba Sana,nilirudi shule ratiba yangu ilijikita Kwenye kumuombea dada...
Walikuja watumishi wanaojiita manabii akaomba kupelekwa.
Kweli nabii alimpitia akamwambia una shida ya Figo, akamwambia ndiyo..akamtazama baadaye akaondoka.
Mara wakawa wanasema kuonana naye Hadi utoe hela laki 3 ..hizo taarifa nilizipata baada ya kuwapigia simu kuongea nao.

Tuliendelea kuomba,,nilipata Tena muda nikarudi nyumbani,aliniomba nimuombee..nikamuombea.

Wiki hiyo alizidiwa akarudishwa hsp,akawa anapumulia machine,siku tatu mfululizo..ya nne akapata nafuu,wanaenda kumuona yaani Hadi anaongea vizuri.
Hiyo wiki nipo Kwenye mfungo..
Asubuhi nimeamka Mara bega likawa linanicheza Sana.
Nikakaa nikatulia Sana mawazo yakawa yananijia kwamba nyumbani Hali SI nzuri Kama Kuna tatizo.

Mchana matron alipigiwa simu na shemeji kumpa taarifa za kifo Cha dada yangu(shemeji yangu mume wa dada yangu mwingine(Sio Huyo mgonjwa ) alikuwa mwalimu pale shule ninayosoma.

Matron akamtafuta rafiki yangu, akamwambia anirudishe nyumbani bila Mimi kujua chochote, wakapanga mpango hapo..rafiki akaja akasema matron ameniruhusu nikamuomba tutoke wote..kweli? Namuuliza ananijibu ndiyo..kwenda kumuuliza matron akakubali,sikustuka kwa sababu matron alikuwa ananiruhusu Mara nyingi kwenda home.
Yule rafiki akasema twende kwanza kwenu tukawasalimie halafu tupike na chakula Cha kurudi nacho shule.

Tumefika mitaa ya home nashangaa jirani ananiambia msiende hivyo,njoo mchukue vitenge mvae..nikajua hapa tayari.
Nikawa najiuliza,nimalizie mfungo au nikate tu muda huo ,ninayemuombea amekufa asubuhi



USHAURI WANGU
Ukiamua kusimama upande wa Mungu,Basi simamia huko.
Changamoto huja pale wengine wanaamini Hiki,wengine kile,
Hamuwezi kufikia mafanikio.

Usipuuze mawazo yanayokujia.
Mara nyingi Mungu anasema na sisi kwa njia ya mawazo na ndoto lakini tumekuwa tukipuuzia.
Ile sauti unayoisikia akilini jifunze kuisikiliza.

Jifunze kuombea ndoto.
Ndoto nyingine huwa zinatokea kweli.
Mimi niliota na nikaipuuza licha ya kukumbushwa Mara nyingi.

mahondaw
Yna aika
Heaven Sent
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom