Ilikuwa kipindi Niko shule,ndoto za kifo zikawa zinanijia Ila Mara napotezea...
Sometimes nikikaa mawazo yananijia kwamba Stella uliota ndoto hii..nikawa sitilii maanani ukizingatia kipindi hicho bado umri mdogo na nilikuwa sijakomaa Sana kiimani.
Nikawa Tena napata mawazo ya nguo, yaani Kama ndoto inanijia dadangu ameshona nguo yake halafu ikapotea(Dada yangu alikuwa fundi cherehani)
Nimerudi likizo mwezi June nikaambiwa dada kihoma kinamsumbua.
Nikafunga safari kwenda kwake kumsalimia...hakuwa serious Sana yaani ilikuwa homa ya kawaida tu alienda hospital wakampima wakakuta ana typhoid,wakampa dozi ya typhoid.
Bado aliendelea kuugua ,akaenda hospital nyingine akapimwa akaambiwa vidonda vya tumbo.
Huo Ni mwezi June.
Hali ikazidi kuendelea..
Yale mawazo yakawa yananijia Tena lakini masikini sijui Ni kutokutambua au utoto,nikawa siyatilii maanani.
Mwezi huo huo akapelekwa Tena hsp akakutwa na tatizo la figo,japo alikuwa fiti tu,hajawahi kuugua ugonjwa wa Figo nyuma,familia hazina historia za magonjwa hayo,kwamba ana HIV hakuna..ilikuja tu from no where.
Tukawa tumeanza maombi,
Binafsi nikaanza maombi kwa ajili yake.
Shida ikawa upande wa mume,wakampeleka kwa waganga wa kienyeji..wakawa wanaambiwa maneno mengi,mwingine anasema Mara fulani alikuroga ,mwingine fulani (dereva)amekuroga,,Huyo dereva alikuwa dereva wa gari la familia la biashara,baada ya kuona anaingiza loss sana akapokonywa gari na likaenda kupakiwa pale nyumbani kwa dada maana Yeye ndiye alikuwa msimamizi wa hayo mapato.
Alipogundulika na Hilo tatizo alianzishiwa tiba ya hosp.
July Mimi nikarudi shule nikimuacha Dada yangu anaendelea vizuri,shida ikawa hiyo michanganyo..Mara waganga,Mara maombi na hosp.
Kuna mtumishi aliongea naye akamuombea akafunuliwa hayo ya nguo.
Kipande Cha nguo kilichukuliwa kikaenda kufanyiwa Mambo huko na kikazikwa.
Nilijitahidi weekend moja kuomba ruhusa na kurudi kumuona dada ..ilikuwa October..nikakuta Hali yake SI nzuri.
Baadaye naye alichoka Yale madawa ya kienyeji ..nilirudi hiyo siku nilikuta wametoka hsp kufanyiwa dialysis.. Hali yake ikazidi kuwa mbaya..
Alinambia mdogo wangu nashindwa kula,nashindwa kuongea vizuri,nashindwa kutembelea,niombee
Niliomba Sana,nilirudi shule ratiba yangu ilijikita Kwenye kumuombea dada...
Walikuja watumishi wanaojiita manabii akaomba kupelekwa.
Kweli nabii alimpitia akamwambia una shida ya Figo, akamwambia ndiyo..akamtazama baadaye akaondoka.
Mara wakawa wanasema kuonana naye Hadi utoe hela laki 3 ..hizo taarifa nilizipata baada ya kuwapigia simu kuongea nao.
Tuliendelea kuomba,,nilipata Tena muda nikarudi nyumbani,aliniomba nimuombee..nikamuombea.
Wiki hiyo alizidiwa akarudishwa hsp,akawa analumulia machine,siku tatu mfululizo..ya nne akapata nafuu,wanaenda kumuona yaani Hadi anaongea vizuri.
Hiyo wiki nipo Kwenye mfungo..
Asubuhi nimeamka Mara bega likawa linanicheza Sana.
Nikakaa nikatulia Sana mawazo yakawa yananijia kwamba nyumbani Hali SI nzuri Kama Kuna tatizo.
Mchana matron alipigiwa simu na shemeji kumpa taarifa za kifo Cha dada yangu(shemeji yangu mume wa dada yangu mwingine(Sio Huyo mgonjwa ) alikuwa mwalimu pale shule ninayosoma.
Matron akamtafuta rafiki yangu, akamwambia anirudishe nyumbani bila Mimi kujua chochote, wakapanga mpango hapo..rafiki akaja akasema matron ameniruhusu nikamuomba tutoke wote..kweli? Namuuliza ananijibu ndiyo..kwenda kumuuliza matron akakubali,sikustuka kwa sababu matron alikuwa ananiruhusu Mara nyingi kwenda home.
Yule rafiki akasema twende kwanza kwenu tukawasalimie halafu tupike na chakula Cha kurudi nacho shule.
Tumefika mitaa ya home nashangaa jirani ananiambia msiende hivyo,njoo mchukue vitenge mvae..nikajua hapa tayari.
Nikawa najiuliza,nimalizie mfungo au nikate tu muda huo ,ninayemuombea amekufa asubuhi
USHAURI WANGU
Ukiamua kusimama upande wa Mungu,Basi simamia huko.
Changamoto huja pale wengine wanaamini Hiki,wengine kile,
Hamuwezi kufikia mafanikio.
Usipuuze mawazo yanayokujia.
Mara nyingi Mungu anasema na sisi kwa njia ya mawazo na ndoto lakini tumekuwa tukipuuzia.
Ile sauti unayoisikia akilini jifunze kuisikiliza.
Jifunze kuombea ndoto.
Ndoto nyingine huwa zinatokea kweli.
Mimi niliota na nikaipuuza licha ya kukumbushwa Mara nyingi.
mahondaw
Yna aika
Heaven Sent
Sent using
Jamii Forums mobile app