Kama umewahi kutafuta maisha au kufanya biashara mpaka wa Kasumbalesa njoo tukumbushane visa vya huko

Kama umewahi kutafuta maisha au kufanya biashara mpaka wa Kasumbalesa njoo tukumbushane visa vya huko

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Mara ya kwanza ilikuwa ni likizo yangu December 2018, nikiwa na mwenyeji wangu ( mzambia) baada ya kupeleka mchele na kumaliza kuuza, mwenyeji wangu alinishauri tusogee Rukwa, tununue dagaa then tuwapeleke Kasumbalesa kwa kipindi hicho akadai wanalipa na yeye anawafahamu dagaa ila shida lugha ya kiswahili inamsumbua hivyo anaogopa kuibiwa.

Tulikuja Tanzania tukanunua hao dagaa na kuwapeleka huko sokoni Kasumbalesa, ndipo nilikutana na mambo haya ambayo hayajanitoka kichwani hadi leo

1. Wapo wanawake wa kitanzania wanajiuza hapo Kasumbalesa.

2.Biashara ya maeneo yale imejaa mambo ya kishirikina, unauza unahesabu pesa unajua umepata faida (ukirudi kuhesabu unagundua pesa imepungua)

3. Wakati masoko yetu Tanzania huchangamka zaidi mchana kwenda jioni, wao biashara ipo asubuhi jioni inapungua sana.

4. Bei inapungua kadri inavyoenda jioni.

5. Madalali wana nguvu na utemi mkubwa anapanga bei yeye na inabidi ukubali hata kama faida kidogo.

6. Usipeleke mzigo hapo sokoni bila kuwasiliana na dalali.

7.Ikifika mali mpya hata asubuhi saa nne ya kwako inapoa.

8. Jamaa wana lugha nyingi hapo hakuna lugha rasmi ( kiswahili kipo)
 
Aisee maisha ni kutafuta, vp ulisitisha biashara au bado unaendelea?
 
Back
Top Bottom