Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Sio katika kila jambo unaweka dhana mbya tu..jifunze kuyaona mazuri ktk kila jambo. Kuna mtu alisema "matajiri wako bize kutafuta fursa, huku maskini wako bize wakidhani kila fursa nni utapeli"
Ndio asili ilivyo,kila mtu anakula kupitia mwenzake,na itabaki kuwa ivyo.Kama tajiri anakula kwa kuleta fursa na masikini naye anakula kwa kuletewa fursa.Kila upande unafaidika.
Kama kutakuwa na utapeli basi upande mmoja unaliwa.
 
Nzuri
 
Mkuu ubarikiwe kwa kile ulichoamua kutishirikisha hakika hata kama hatutafanya hii biashara lakini kuna kitu tumejifunza, Nashauri hata wengine tuendelee kufanya hivyo kama unafanya biashara nzuri tushirikishane
 
Mkuu ubarikiwe kwa kile ulichoamua kutishirikisha hakika hata kama hatutafanya hii biashara lakini kuna kitu tumejifunza, Nashauri hata wengine tuendelee kufanya hivyo kama unafanya biashara nzuri tushirikishane

Karibu sana mkuu.
 
Sio mbaya ila ina mchakato mrefu na logistic ndefu sana halafu faida yake bado ni ndogo sana, yaani asilimia 10% tu.

Faida utaiona kama utapeleka mbuzi wengi sio chini ya 100 ambapo mchakato wake wa kuwakusanya na kuwasafirisha sio kazi ndogo....lakini ni biashara nzuri hasa kwa anaeweza kufuga maelfu ya mbuzi...
 
Bila shaka jamaa anahamia phase nyingine,Top level ya food chain.
Watakaoingia kwenye hii biashara sa hivi atawauzia mbuzi na kuwapiga udalali.anatafuta mbuzi wa kumuingizia pesa .
Akili za kijinga zimelala hapa
 
Mkuu shukrani kwa idea nzuri mno. Ngoja ninenepeshe Mifugo yangu kumbe solo la uhakika lipo.AHSANTE SANA
 
Sioni mirejesho ya vijana wapambanaji mpaka sasa tungeona:

Nimekusanya mbuzi 27 Ila changamoto n usafiri,

Au ndo nipo kibaha hapa kiwandani changamoto n folen

Au nimenunua mbuzi 13 kufika kiwandani mbuzi mmoja kapotea

Niliamua niingie Singida huko Nduguti au kidarafa mpaka Meatu kule aseme huku mbuzi wapo changamoto n usafiri


Huu uzi ulipaswa uwe mbali Sana kwa kusaidia vijana pia au lazima uwe mbuzi hata samaki inawezekana, mazao inawezekana. Hata bidhaa za viwandani unatoa mjini unapeleka kijijini
 
Bro mazungumzo ni rahisi kuliko vitendo...usijali mirejesho itakuja tu inshaallah..ngoja tuendelee kufanya research kwnz.
 
Kabisa sisikiimrejesho wowote
 
Mirejesho itakuja ni swala la watu nao kufanya research zao pia kabla ya kuanza
 
talentboy na azariah gody research ya kitu inafanywa field
Kuingia field kufanya research kwanza kabla hujaingiza pesa....... Ngj nikupe mfano kipindi hicho mie nafatilia hii ishu nilikuja gundua kuwa usafiri utanisumbua especially kuelekea mwanza sasa je ningeamua kuingia moja kwa moja na cash nikachukua mzigo kabla ingekuwaje zaid ya kupoteza
 
Kwenda mwanza ukiwa unatokea wap
 
Iko njema
 
Wangenunua mbuzi akiwa hai ingekuwa nzuri zaidi, bei iwe 6,000 ao 6,500 /KG kuliko wanunue nyama 6,800 ao 7,000/KG. AMINI NAKWAMBIA!!!!! WANAPIGA KWENYE UZITO WA NYAMA
Sio uzito tu wanapiga kwingi sana..hayo mautumbo..mapembe na kwako..bado ngozi kwao ni super profit.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…