Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Umeandika vizuri na umeeleweka ukiona mtu anauliza swali huyo Hana nia na hawezi mikiki mikiki ya hyo kazi sababu umeandika vitu muhimu na umenyoosha.

Binafsi nishafanya Ila ilkua n nguruwe mnadani unatakiwa uwe mjanja na mshapu Ila door to door n nzuri muhimu uwe unajua kwa macho kuwa huyu ukimuangalia hakosi KG kadhaa hvyo unakata hata 7kg ndo unaongea Bei na mnunuzi.

Changamoto ya Door to door unatakiwa ujue kuishi na watu ukikuta watu wanakula ugali wa mdama na dagaa wa kuchemsha unga usilete swaga, Kuna muda inabidi ulale hukohuko bush kwa wenyeji Kama n kulala chini lala Kama n kwenye ngozi lala faida yake utakuja kuiona baadae.

Ukiingia Kijiji unakutana na mjanja wao Sasa wewe kuwa mjanja zaidi yake wengi wanaongea kilugha hvyo jifunze kujua maneno muhimu kwenye Biashara yako katika sehemu unayokwenda kutafuta mifugo.

Jifunze kumsoma mtu usoni pindi mnaposalimiana tuu au akiongea maneno matatu hii itakusaidia kupata kwabei nafuu.

Vijana tupambane usisubiri mpaka ufike 1million ndo uanze Anza na hicho hicho ulichonacho Kama una Nia inakutoa bila shida hata Kama n laki moja we Anza na pale inapowezekana.

Kijana una upeo mkubwa, nimefurahishwa sana na comment yako hii. Ni ufafanuzi unaothibitisha Uwezo wako mkubwa wa kufikiri na kupambanua mambo kwa weledi.
 
Habarini Waungwana!

Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.

Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.

BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.

A. Upatikanaji wake

Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.

Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.

B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.

C. Bei ya mbuzi

Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.

D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.

E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.

F. Changamoto zake

Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
  • Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
  • Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
  • Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
  • Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
G. Malipo

Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?

Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.

ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.

Huu uzi kwanini usihamiishiwe kule kwenye "Stories of change "?
 
Wazo zuri sana, ahsante mkuu.
Ila hapo kwenye viwanda kuchinja na kuwataarifu kg (uzito wa mifugo yenu) ndio wanapotengeneza super profit.

Ni kama mabenki wanapopeleka pesa BoT, hua wanapewa taarifa tu kwamba zimepungua kadhaa, wanakatwa huko huko juu kwa juu na hauwezi kuthibitisha kwa vile unakua haupo eneo la tukio wakati wa kuhesabu.
Najaribu kuwaza wakichukua kg moja moja tu kwa kila mbuzi, wanapata pesa nzuri tu.

Lakini mtu akiamua kuweka mfumo imara wa ujusanyaji huko vijijini kwa uhakika wa hiki soko, anaweza asiajiriwe na akapiga pesa ndefu tu.

mrangi pitia huku!
That friend of "ours" aliwahi nidokezea hii na mzee wake wa kiyemen, unakumbuka? sema yeye info zake zilikuwa na manyokanyoka mengi kama kawaida yake...
 
That friend of "ours" aliwahi nidokezea hii na mzee wake wa kiyemen, unakumbuka? sema yeye info zake zilikuwa na manyokanyoka mengi kama kawaida yake...

Mambo mengi, version tofauti sana na hii.
 
Daah!kaka jebel ahsante sana!!kama yupo MTU anahitaji hyo business na yuko busy hana mda snipe dili hill mi antume tunaingia mkataba hata was miezi sita mi namfanyia kila kitu mradi maelewano tu
Uko wap mkuu
 
Hongera mkuu kwa wazo zuri la biashara.


Niliwahi kufanya biashara inayofanana na hii ya mbuzi
Nilikuwa nanunua nguruwe wilaya ya Chato napeleka Mwanza ( uwanja wa fisi )
Ilikua biashara nzuri na changamoto ni kama zinafanana
Nilipata changamoto zaidi kwenye usafiri na ukusanyaji wa nguruwe lakini soko lilikuwa la uhakika na faida haikosekani.

Umenikumbusha mbali sana mkuu.
Ulitumia usafiri gani kuwasalimisha kiongozi?
 
Ulitumia usafiri gani kuwasalimisha kiongozi?
Nilikuwa natumia gari ndogo mkuu, sana sana kirikuu
Nawakusanya kwa siku kama mbili au tatu halafu napiga simu Mwanza wanaleta gari

Changamoto unaweza ukanunua nguruwe kwenye nyumba kumi maeneo tofauti gari ikija mnaanza kupita nyumba moja mpaka ya mwisho tunapakia tunaondoka
Pia ukishawalipia wakati unasubiri usafiri
mwenye mji anakwambia gharama za kuwalisha ni zako mpaka utakapokuja kuwachukua.

Kirikuu inakaa wastani wa nguruwe 12 wodogo na 9 wakubwa

Kibali ilikua tunakata Buselesele
kila nguruwe Tsh1000

Kila nguruwe nilikuwa naweza kupata faida ya Tsh 50,000 ila sehemu kubwa ya faida inaliwa na usafiri.
 
Nilikuwa natumia gari ndogo mkuu, sana sana kirikuu
Nawakusanya kwa siku kama mbili au tatu halafu napiga simu Mwanza wanaleta gari

Changamoto unaweza ukanunua nguruwe kwenye nyumba kumi maeneo tofauti gari ikija mnaanza kupita nyumba moja mpaka ya mwisho tunapakia tunaondoka
Pia ukishawalipia wakati unasubiri usafiri
mwenye mji anakwambia gharama za kuwalisha ni zako mpaka utakapokuja kuwachukua.

Kirikuu inakaa wastani wa nguruwe 12 wodogo na 9 wakubwa

Kibali ilikua tunakata Buselesele
kila nguruwe Tsh1000

Kila nguruwe nilikuwa naweza kupata faida ya Tsh 50,000 ila sehemu kubwa ya faida inaliwa na usafiri.

Mkuu cheki PM tafadhali
 
Umenikumbisha miaka fulani huko tumefika gairo kununua kuku vijijini Dogo wa kimara akawa kuku akikimbia tunasema mkimbize au chukua huyo kuku umfunge miguu anasema hawa hawang’ati kweli mbona wakali mwanaume huyo
😅😅😅😅
 
Hii biashara ni nzuri hata Arusha maana Kikatiti, na kule namanga kuna wanunuzi wa kenya wanakuja kununua mbuzi na wamaasai wanadai wanafunguka pesa nzuri sana, japo sikuwa kuingia front kwenye hili, lakini kikatiti huwa kuna mnada wa mbuzi na ng'ombe kwa hapa Arusha, nadhani Kikatiti bei za mbuzi huanzia 60,000 huwa bei zao mnadani ndiyo hizi hazishukagi. Kondoa ndiyo ninasikia wapo mbuzi mpaka wa 30000 na wana weight ya kuridhisha

Nitafuatilia pia updates cha kiwanda cha nyama Arusha.
 
Alisema amepata mchongo nje ya nchi nadhani😅 we sahizi upate line ya Marekani utakataa uendelee kuswaga mbuzi bongo?
Yeye ametoa mapendekezo kuwa ile ilikuwa ni biashara yenye afadhali hukosi pesa kabisa yaani sio sawa na kukaa bure au kufanya mavitu pasua kichwa.
 
Nilikuwa natumia gari ndogo mkuu, sana sana kirikuu
Nawakusanya kwa siku kama mbili au tatu halafu napiga simu Mwanza wanaleta gari

Changamoto unaweza ukanunua nguruwe kwenye nyumba kumi maeneo tofauti gari ikija mnaanza kupita nyumba moja mpaka ya mwisho tunapakia tunaondoka
Pia ukishawalipia wakati unasubiri usafiri
mwenye mji anakwambia gharama za kuwalisha ni zako mpaka utakapokuja kuwachukua.

Kirikuu inakaa wastani wa nguruwe 12 wodogo na 9 wakubwa

Kibali ilikua tunakata Buselesele
kila nguruwe Tsh1000

Kila nguruwe nilikuwa naweza kupata faida ya Tsh 50,000 ila sehemu kubwa ya faida inaliwa na usafiri.
Asante kwa taarifa zenye kujitosheleza..umeeleza vizuri Sana.
Naomba nikuulize swali..lingine..wateja uliwapataje wa kununua nguruwe wengi kwa wakati mmoja..?
 
Back
Top Bottom