Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Habarini Waungwana!

Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.

Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.

BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.

A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.

Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.

B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.

C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.

D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.

E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.

F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
  • Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
  • Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
  • Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
  • Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
G. Malipo

Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?

Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.

ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.

Nitalifanyia kazi hili wazo.Ahsante sana mkuu
 
Nzuri. Kwa anaye anza mdogo mdogo nunua mbuzi chinja. Ya ndani pika supu. Ya nje kata mapande, uza 4,000 weka kibanda karubu na kituo kikubwa cha mabasi. Kaa karibu na mtu wa chapati. Chukua na ndizi iwe karibu.
 
Nafatilia mkuu,ntatia neno

Ova

Uko salama lakini mkuu? Umepotea sana.
Hivi viwanda kama kweli wananunua kiasi chochote utakachopeleka na hawako na usumbufu kwenye malipo, watakua wazuri.

Hapo kwenye mzigo kupimwa bila uwepo wako ndio naona kuna mushkel kidogo.
 
Simple, kama huwaamini unachukua mbuzi wako unaenda kupambana na madalali Vingunguti 😅 ndio ukaone vibweka sasa kama hujarudi mbio mbio hapo kiwandani!

Bora ya hawa hata kama wanakupiga lakini uhakika na mfumo wao umekaa sawa kidogo. Madalali unaweza kujikuta umegeuka Hamza na pesa yako hauipati.
 
Kama hao wamiliki wa kiwanda ni wa China, narudia tena ni waChina mimi siwaamini hata kidogo maana hawa ni wahalifu sana hivyo nahisi kwa asilimia kubwa ninyi mnaowauzia mbuzi mnapigwa sana.Ki utaratibu ilitakiwa waweke utaratibu wa kila muuza mbuzi ashuhudie yeye mwenyewe au mtu aliyemteua uzito wa nyama tena kwenye mizani iliyo hakikiwa na watu wa vipimo (WMA).
Wangenunua mbuzi akiwa hai ingekuwa nzuri zaidi, bei iwe 6,000 ao 6,500 /KG kuliko wanunue nyama 6,800 ao 7,000/KG. AMINI NAKWAMBIA!!!!! WANAPIGA KWENYE UZITO WA NYAMA
 
Habarini Waungwana!

Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.

Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.

BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.

A. Upatikanaji wake

Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.

Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.

B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.

C. Bei ya mbuzi

Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.

D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.

E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.

F. Changamoto zake

Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
  • Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
  • Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
  • Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
  • Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
G. Malipo

Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?

Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.

ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.

Ahsante sana kwa kua muazi mkuu japo umesema baada ya wewe kupata kazi nyingine. Ila mtririko wa wa biashara ni mzuri, ila hiki kipanda ndo kimeharibu hiyo biashara bepari an exoploit hapa kwa nini asiwe muazi?

"......Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma....."

Bepari anapata faida ×3 ya muangaikaji polini hapo ngozi ya mbuzi ni sh 7000 kwa open market, utumbo wa mbuzi unakausha na kutegeneza chakula cha [emoji241] kilo gharama ni 5000, kama mzani ni wake mpimaji niyeye mnunuzi niyeye duh hiyo sio fair play. Ata akipunguza 0.5kg kwa kila mbuzi ni faida kubwa sana.... wanyonge tutabaki hivo hivo paka pale tutakapo pigania fair trade na matajiri. Hiyo biashara ni nzuri kwa kujikimu ila kutajirika ujenge apartment au mall sio.
 
Yah hawa ndio watu wanaotakiwa wawe wengi nchini ili tusonge mbele ila kibaya wamejaa wachoyo, roho mbaya na wazandiki tu! Mtu anakwambia tafta hela wewe ila mbinu hakupi 😅 shwaini kabisa kwani zinaokotwa hizo hela?
Mtu mweusi akiacha ubinafsi tutafika mbali sana,

Wengi tunaamini tulikuja duniani kukusanya tunasahau kuwa tulikuja kufanikisha mambo, ukitoa hata mawazo tu ni sadaka kubwa sana.
 
Kichwa kinauma toka niliposoma hapa mda huu Niko tu nimekaa sina cha kufanya nafsi inaumwa balaa...ningekua na 2m hapa mda huu Niko mbezi Nnapmshapaland KVC au Shabiby ya Dom niamkie Huko urangini ila ndo napambana hapa mpk kieleweke aseehh!kumbe tunapoteza tu mda kirahisi hivi ila bi idhn lllaah hii ntakomaa nayo hata mwisho wa mwezi huu!!
 
Nb: research ni muhim mnoo
 
Ahsante sana kwa kua muazi mkuu japo umesema baada ya wewe kupata kazi nyingine. Ila mtririko wa wa biashara ni mzuri, ila hiki kipanda ndo kimeharibu hiyo biashara bepari an exoploit hapa kwa nini asiwe muazi?

"......Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma....."

Bepari anapata faida ×3 ya muangaikaji polini hapo ngozi ya mbuzi ni sh 7000 kwa open market, utumbo wa mbuzi unakausha na kutegeneza chakula cha [emoji241] kilo gharama ni 5000, kama mzani ni wake mpimaji niyeye mnunuzi niyeye duh hiyo sio fair play. Ata akipunguza 0.5kg kwa kila mbuzi ni faida kubwa sana.... wanyonge tutabaki hivo hivo paka pale tutakapo pigania fair trade na matajiri. Hiyo biashara ni nzuri kwa kujikimu ila kutajirika ujenge apartment au mall sio.
kwwnye kutajirika na kujenga malls itategemea na mtaji wako na nidhamu kwa faida unayoingiza...kama mbuzi wawili mpk watatu wanaweza kulipa gharama zote ndogo ndogo...hlf kwa kila mbuzi lets say mbuzi 100, ukapata faida ya buku 5 - 6 nadhani sio faida mbaya kama una uhakika wa kuzungusha kila wiki.
 
Nafuga kondoo na mpka sasa Mimi ni mtaalamu mzuri ktk ufugaji kondoo...kuna kitu naona bado kinanitesa sana ktk maisha yangu kwa sababu sijakikamilisha ipasavyo nafuga kondoo wachache tu bado sijafikia lengo na bado sijaanda mazingira ya kufuga kondoo wengi hichi ndo kitu kinantesa
Naishi kijijini ila ni kijiji ambacho umeme upo,maji yapo, Barabara zinapitikaa na usafiri wangu wa boxer kwenda mjini na kurudi unanitosha sana...kijiji chetu naweza kufuga hata kondoo 900 na zikala majani mpka zikayaacha huwa napiga hesabu nikitimiza majike ya kondoo 300- 400 na madume 5 tu hapa kijijini... Mimi ni TAJILI uwezo wa kuwa nazalisha kondoo 900-1000 kwa mwaka upo...kondoo anazaa Mara 2 kwa mwaka anabeba mimba miezi mi3 je nkizalisha 800 na nkiwauza sh50000 kwa kila kondoo moja....hapa kijijini NTATAMBA si mchezo ngoja niandae mazingira.
 
Umeandika vizuri na umeeleweka ukiona mtu anauliza swali huyo Hana nia na hawezi mikiki mikiki ya hyo kazi sababu umeandika vitu muhimu na umenyoosha.

Binafsi nishafanya Ila ilkua n nguruwe mnadani unatakiwa uwe mjanja na mshapu Ila door to door n nzuri muhimu uwe unajua kwa macho kuwa huyu ukimuangalia hakosi KG kadhaa hvyo unakata hata 7kg ndo unaongea Bei na mnunuzi.

Changamoto ya Door to door unatakiwa ujue kuishi na watu ukikuta watu wanakula ugali wa mdama na dagaa wa kuchemsha unga usilete swaga, Kuna muda inabidi ulale hukohuko bush kwa wenyeji Kama n kulala chini lala Kama n kwenye ngozi lala faida yake utakuja kuiona baadae.

Ukiingia Kijiji unakutana na mjanja wao Sasa wewe kuwa mjanja zaidi yake wengi wanaongea kilugha hvyo jifunze kujua maneno muhimu kwenye Biashara yako katika sehemu unayokwenda kutafuta mifugo.

Jifunze kumsoma mtu usoni pindi mnaposalimiana tuu au akiongea maneno matatu hii itakusaidia kupata kwabei nafuu.

Vijana tupambane usisubiri mpaka ufike 1million ndo uanze Anza na hicho hicho ulichonacho Kama una Nia inakutoa bila shida hata Kama n laki moja we Anza na pale inapowezekana.
 
Back
Top Bottom