Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Idea nzuri lakini inahtaji uwe fighter sana. Vimichakato vyake usiwe mtoto wa mama. Kuna watoto wa mama hata mbuzi wanaogopa kushika
Hawa watu wamjini wanaitwa mmea wa viazi mchipsi wakimaanisha viazi vinautwa mchipisUmenikumbisha miaka fulani huko tumefika gairo kununua kuku vijijini Dogo wa kimara akawa kuku akikimbia tunasema mkimbize au chukua huyo kuku umfunge miguu anasema hawa hawang’ati kweli mbona wakali mwanaume huyo
Mkuu yuko vizuri ana roho ya kitajiri,Unaweza ukahisi umeandika kwa kupoteza muda ila ukweli ni kuwa kuna watu tayari umewapa wazo zuri sana la biashara na soon wataanza kulifanyia kazi. Hongera sana mkuu kwa hili wazo una roho ya kitajiri na utafanikiwa sana maishani mwako.
Soko la kondoo lenyewe likojee boss wangu..Habarini Waungwana!
Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.
Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.
BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.
A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.
Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.
B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.
C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.
D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.
E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.
F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
- Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
- Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
- Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
- Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
G. Malipo
Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?
Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.
ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.
Nje ya mada kidogo. Pamoja na kulipa ushuru huu wote, ukipata kafaida ka eg sh laki moja na ukaamua kumtumia mama yako mgonjwa kijijini akatibiwe, basi unatakiwa kilipa tena tozo ya muamula! Na mama yako anapokwenda kutoa fedha nako analipa! Na akienda hospital nako anakwenda kulipa! Kweli kweli inabidi wananchi tuamke sasa tukiwashe kwa sababu hakuna mtawala atakaye tuonea huruma. Wao wako busy kutumbua hizi fedha wanazokata kwa maskini.Maswali mazuri ndugu.
Kila mbuzi unamlipia ushuru 1000Tsh kwa kila mbuzi halafu kibali kinakuwa ni kimoja ambacho ili kupunguza gharama mbuzi wote wanakuwa chini ya kibali kimoja kama vile mwenye mzigo ni mtu mmoja, kama mzigo ni mkubwa basi sisi tulikuwa tunakata vibali viwili basi.
Kuhusu mara ngapi unaweza kupeleka mzigo itategemeana na mtaji wako na uchakarikaji wako katika kutafuta mzigo. Upande wa mtaji Nina maana kwamba unaweza kuagiza mzigo kiwandani labda wa 3M halafu kama una balance ukabakia unakusanya mzigo mwingine wakati unasubiria mzigo ufike kiwandani, mbuzi wachinjwe na pesa utumiwe. Kuna wakati inaweza kuchukua hadi siku 3 au 4 kutoka mchakato wa kusafirisha mbuzi kutoka vijijini hadi kiwandani hadi kupata pesa kwa hiyo ndani ya siku hizo unajikuta una andaa mzigo mwingine, unafanya rotation. Wenye mitaji mikubwa walikuwa walifanya hivi.
Sijui kama kuna swali nimesahau kujibu mkuu
ata Magu pia kuna kiwanda cha nyama hua wananunua Mbuzi Ngombe na kondooHata kwa wale wa mwnza pia kuna kiwanda cha nyama misungwi kuna muda walisitisha ila sijajua kama wanaendelea hivi sasa ama lah
[emoji3516]Mkuu ukifika Kondoa mjini ulizia madalali au wanunuzi wa mbuzi, watakupeleka minadani. Minada inakuwa vijijini kila kijiji kina siku yake na pale Kondoa mjini pia kuna siku yake.
Kuhusu soko hadi mimi nasitisha baada ya kupata ajira nje ya nchi, lilikuwa la uhakika sana na ilikuwa March mwaka huu. Hata ungepeleka lori zima wananunua, kiwanda ni kikubwa sana na hawa jamaa wanapeleka nyama ya mbuzi, nchi za kiarabu, Oman, Qatar na kwingineko kwa hiyo soko ni uhakika sana.