Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Kama una mtaji fanya biashara ya Mbuzi, utakuja kunishukuru

Mkuu ukifika Kondoa mjini ulizia madalali au wanunuzi wa mbuzi, watakupeleka minadani. Minada inakuwa vijijini kila kijiji kina siku yake na pale Kondoa mjini pia kuna siku yake.

Kuhusu soko hadi mimi nasitisha baada ya kupata ajira nje ya nchi, lilikuwa la uhakika sana na ilikuwa March mwaka huu. Hata ungepeleka lori zima wananunua, kiwanda ni kikubwa sana na hawa jamaa wanapeleka nyama ya mbuzi, nchi za kiarabu, Oman, Qatar na kwingineko kwa hiyo soko ni uhakika sana.
Kama ilikua inakulipa vizuri mkuu kwa nin uliamua kuajiriwa ?

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Hongera mkuu kwa wazo zuri la biashara.


Niliwahi kufanya biashara inayofanana na hii ya mbuzi
Nilikuwa nanunua nguruwe wilaya ya Chato napeleka Mwanza ( uwanja wa fisi )
Ilikua biashara nzuri na changamoto ni kama zinafanana
Nilipata changamoto zaidi kwenye usafiri na ukusanyaji wa nguruwe lakini soko lilikuwa la uhakika na faida haikosekani.

Umenikumbusha mbali sana mkuu.

Duuuuh aise nadhani usafirishaji wa nguruwe inabidi uwe na gari lako la sivyo nadhani ni paper la Physics form six!
 
Duuuuh aise nadhani usafirishaji wa nguruwe inabidi uwe na gari lako la sivyo nadhani ni paper la Physics form six!
Hahaha
Nilikuwa nasafirisha usiku ( nguruwe hawawezi kuhimili jua la mchana kama umbali ni mrefu)

Kibaya zaidi ilikuwa lazima tuvuke na pantoni pale Busisi yaani fujo tupu humo ndani..

Anyway ndio maisha mkuu.
 
huko wanakopatikana hao mbuzi ni Kondoa kijiji/mtaa gani? Au ukifika tu kondoa ukiulizia mnada wa mbuzi utapelekwa? Naomba details zaidi jinsi ya kufika huko wanakonunua mbuzi na gharama zakr za usafiri.

Na unazungumziaje uhakika wa soko huko kiwandani? Mana nisije kuchukua mbuzi wa kutosha hlf nafika kiwandani..naambiwa wanastock ya kutosha hawahitaji tena...au inabidi nifike hapo kiwandani kwnz kuona kama wanao uhitaji?
Usikurupuke kak utakuja Lia ..unasoma vxr na kumuelewa una let's mbuz unaacha unaenda watakutumia pesa na kukujulia kuwa umepata kilo ngap wkt haupo Apo achana na pesa za harakharaka
 
Hahaha
Nilikuwa nasafirisha usiku ( nguruwe hawawezi kuhimili jua la mchana kama umbali ni mrefu)

Kibaya zaidi ilikuwa lazima tuvuke na pantoni pale Busisi yaani fujo tupu humo ndani..

Anyway ndio maisha mkuu.

Ni kweli Mkuu haya maisha ni safari....nimependa sana upambanaji wako mkuu. Naamini Mungu anazidi kukufungulia milango ya baraka.
 
Ni kweli Mkuu haya maisha ni safari....nimependa sana upambanaji wako mkuu. Naamini Mungu anazidi kukufungulia milango ya baraka.
Asante mkuu,

Ni kweli, Mungu anaendelea kufungua milango tunasonga mbele
Hongera pia kwa mapambano mkuu.
 
Habarini Waungwana!

Leo nimeona nitoe mchongo wa biashara ambayo binafsi nimewahifanya kabla sijapata ajira na natarajia kuendelea kufanya baada ya ajira kuisha.

Uzuri wa biashara hii, pamoja na kuwa na faida nzuri, soko lake ni la uhakika sana na changamoto zake ni chache sana na zinakabilika kwa mtu ambaye ameamua kwa dhati kutafuta.

BIASHARA YENYEWE NI KUNUNUA MBUZI NA KWENDA KUUZA KIWANDANI.

A. Upatikanaji wake
Upatikanaji wa mbuzi. Pamoja na mambo mengine ambayo Tanzania tumejaliwa ni mifugo hasa mbuzi. Kuna upatikanaji wa uhakika wa mbuzi na kondoo katika mikoa ya Dodoma (Urangini), Singida, Tanga na Tabora. Kwa kule KONDOA kuna Warangi wazuri sana madalali ambao ni waaminifu sana tofauti na madalali ambao tumewazoea katika jiji la Dar.

Kwa ushauri wangu, sehemu nzuri zaidi ya kununua mbuzi kwa bei nzuri, wenye ubora (Uzito) na faida nzuri, urahisi wa upatikanaji wake na hata urahisi wa usafirishaji ni KONDOA (Urangini). Huku kuna minada ya mbuzi kila siku na hivyo kwa siku unaweza kununua hadi mbuzi 50 na zaidi kama una mwenyeji mzuri.

B. Soko lake
Binafsi ningependekeza kupeleka kiwandani hasa kiwanda cha TanChoice kilichopo Soga, wilani Kibaha mkoa wa Pwani. Hapa utaweza kuuza idadi yoyote ya mbuzi japo huwa wanapenda walau uwe na mbuzi kuanzia 20 (hii ni idadi wakati mimi napeleka inawezekana kukawa na mabadiliko kwa sasa).
Sehemu nyingine ni Longido-Arusha katika kiwanda cha Eliya Food Ltd japo kwa Arusha kuna wanunuzi wengi hasa Wakenya wanatoa bei nzuri sana.

C. Bei ya mbuzi
Kwa kuwa mbuzi hununuliwa vijijini bei yake siyo kubwa kwani ina range kati ya 30-70 elfu. Mbuzi wa 30 elfu anaweza kukadiriwa kuwa na uzito wa kilo 7 au 6.5. Mbuzi wa 70 elfu anaweza kufikisha hadi 12Kg au 13Kg. Kiwandani hawapendelei sana mbuzi wakubwa sana kwa hiyo ni vema kuwa makini katika selection ya mbuzi wa size ya kati ili upate faida nzuri na soko la uhakika.

D. Bei ya nyama kiwandani
Wakati mimi napeleka mbuzi katika kiwanda cha TanChoice, walikuwa wakinunu kwa Tsh 7000/Kg kwa mbuzi na Tsh6800/Kg. Kwa Arusha inasemekana bei iko juu kidogo ila Arusha niseme ukweli sana information za kutosheleza kwani nilienda trip moja tu.

E. Kadirio la faida
Kama mbuzi amenunuliwa kwa kwa Tsh 50,000/= halafu akatoa Kg 9 za nyama ambazo ni sawa na Tsh 63,000/= faida yake itakuwa karibu 6,000Tsh hadi 7,000Tsh kwa mbuzi mmoja. Hapa unakuwa umetoa Gharama zote kuanzia usafiri kutoka Dar nimetumia kwa wakazi wa Dar hadi Kondoa, kulala guest, usafiri kwenda minadani, kuwasafirisha kutoka minadani hadi Kondoa mjini, ushuru wake na vibali, usafiri kwenda Dar kiwandani, chakula na mengineyo.

F. Changamoto zake
Kusema ukweli kila kazi ina changamoto zake na hasa inapokuja suala la biashara, basi changamoto haziepukiki. Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine ina makandokando yake kama ifuatavyo;
  • Kuna wakati kunakuwa na wanunuzi wengi wa mbuzi kwa hiyo competition inakuwa kubwa sana na kupelekea wauzaji kupandisha bei na hivyo faida kukuachia kidogo sana
  • Usipokuwa makini madalali ambao wameshawahi kufika Dar basi lazima watakulalia katika ununuzi wa mbuzi. Binafsi kwa mara ya kwanza nilijikuta kwa kila mbuzi mmoja napigwa 2000-3000Tsh. Yaani mbuzi anamununua 40,000Tsh halafu ananiambia amemchukulia 43,000Tsh.
  • Kuna wakati upatikanaji unakuwa mgumu hata kama wanunuzi siyo wengi. Baadhi ya siku unakuta wanaoleta mbuzi minadani ni wachache sana na hivyo unaweza kutumia siku nyingi kupata mzigo mzuri.
  • Uwezekano wa kuibiwa mbuzi. Kumbuka munapowanunua mbuzi kutoka mnadani basi munawahesabu na kila mnunuaji anaweza label ya kwake kwenye mbuzi kwa kutumia mkazi. Mimi ilikuwa nachora herufi K ambayo ni herufi ya kwanza ya jina la wife. I love her and she knows that. Baada ya hapo munawaweka mbuzi pamoja na kumkabidhi kijana anayewaswaga kutoka mnadani(minada ipo maporini sijui kwanini) hadi kuwafikisha mjini. Baada ya hapo mbuzi wote wanawekwa kwenye gari na kupelekwa kiwandani. Wakati mwingine mnaweza kupata gari linaloishia Dodoma na kulazimika kuunganisha na wanunuzi wengine wanaofikishia mzigo wao Dom mjini na kisha kutumia gari moja kupeleka kiwandani. Sasa inaweza kutokea au kijana anayewaswaga kutoka mnadani akapiga pande mbuzi mmoja au vijana wanaowaangalia na kuwapeleka malishoni kama unanunua mzigo mkubwa kwa siku kama tatu au zaidi.
-Mbuzi kukosa uzito wa kutosha. Hapa ndo sehemu ya kuwa makini sana. Mbuzi wanaotoka Tabora kwa mfano, uzito wake ni mdogo sana wanapochinjwa tofauti na mbuzi wa Kondoa. Kwa hiyo ukinunua mzigo Tabora kwa bei kubwa kuna uwezekano ukaingia loss na kurudi hapa kunitukana na kunilaumu. Naomba kwa atakayekuwa interested aulize maswali ya kutosha na ikiwezekana afike Kondoa kufanya preliminary investigation and research. I do recommend Kondoa kwa warangi.
G. Malipo

Unapofikisha mzigo kiwandani unaandikisha idadi ya mbuzi, na label uliyowawekea. Kisha unawaachia bank account au namba ya simu kama utapenda malipo yafanyike kwa njia ya simubank. Baada ya siku moja au mbili maximum unatumiwa kiasi cha uzito uliopatikana baada ya kuchinja mzigo wako na kisha account yako inasoma. Hapa kwenye malipo mara nyingi hakuna usumbufu japo binafsi nilifikiria sana reliability yake yaani wanakwambia umepata KG 500, kwa mfano, inakuwa ni hiyo hiyo au inawekana ilikuwa zaidi?

Hitimisho
Kila biashara ina changamoto kama nilivyosema mwanzoni lakini biashara ambayo soko lake ni la uhakika na mzunguko wake ni wa uhakika basi daima huwa ni biashara nzuri. Kwa yeyote anayependa kujaribu biashara hii, nashauri afanye utafiti wa kutosha na kisha aanze na mzigo kidogo hata wa 1M kwanza aone faida yake, changamoto zake n.k.

ASANTENI KWA MDA WAKO NAKUTAKIENI MAFANIKIO KWA KAZI UFANYAYO.

Safi sana nimependa uchambuzi wako na biashara iko transaprency sio wale kenge wanaokujaga kujinadi oh ninaingiza laki 2 kila siku ila biashara anayofanya kusema hataki anawaringishia tu!

Anyway hii mfumo wake ni kama ule wa Nguruwe tu ukiwatoa mkoani na kuwapeleka kwenye machinjio special! Sema hii huwa wanaruhusu kwenda ukapimiwe kilo kila asubuhi akichinja mzigo wako una record kabisa kilo zilizopatikana kisha ukija ku compile mwisho wake unapewa cash yako tu.
 
Hongera mkuu kwa wazo zuri la biashara.


Niliwahi kufanya biashara inayofanana na hii ya mbuzi
Nilikuwa nanunua nguruwe wilaya ya Chato napeleka Mwanza ( uwanja wa fisi )
Ilikua biashara nzuri na changamoto ni kama zinafanana
Nilipata changamoto zaidi kwenye usafiri na ukusanyaji wa nguruwe lakini soko lilikuwa la uhakika na faida haikosekani.

Umenikumbusha mbali sana mkuu.
Kuna kipindi kuna jamaa yangu alikuwa anafanya pia hii! Niliitamani sana kwa kweli ila mziki wake ni kuwasaka na kuwapata hao wadudu
 
Mkuu yuko vizuri ana roho ya kitajiri,

Naamini kuna mtu anafanikiwa kwa kupitia uzi huu.

Ikipendeza yeyote anayefanikiwa kupitia mawazo ya watu kama hawa walete mrejesho ikiwezekana kutoa hata shukrani tu inatosha sana, Mwisho wa siku tuzo ya heshima itolewe.
Yah hawa ndio watu wanaotakiwa wawe wengi nchini ili tusonge mbele ila kibaya wamejaa wachoyo, roho mbaya na wazandiki tu! Mtu anakwambia tafta hela wewe ila mbinu hakupi 😅 shwaini kabisa kwani zinaokotwa hizo hela?
 
Wazo zuri sana, ahsante mkuu.
Ila hapo kwenye viwanda kujinja na kuwataarifu kg (uzito wa mifugo yenu) ndio wanapotengeneza super profit.

Ni kama mabenki wanapopeleka pesa BoT, hua wanapewa taarifa tu kwamba zimepungua kadhaa, wanakatwa huko huko juu kwa juu na hauwezi kuthibitisha kwa vile unakua haupo eneo la tukio wakati wa kuhesabu.
Najaribu kuwaza wakichukua kg moja moja tu kwa kila mbuzi, wanapata pesa nzuri tu.

Lakini mtu akiamua kuweka mfumo imara wa ujusanyaji huko vijijini kwa uhakika wa hiki soko, anaweza asiajiriwe na akapiga pesa ndefu tu.

mrangi pitia huku!
Biashara nyingi Tanzania za kilimo na ufugaji zinatesa watu na kukosa tija sababu ya kukosa uhakika wa soko! Hilo tu yani ndio maana kilimo watu wanaki bullshit!

Ila kungekuwa na maviwanda kama haya mengi ingepunguza sana tatizo la ajira!
 
Biashara nyingi Tanzania za kilimo na ufugaji zinatesa watu na kukosa tija sababu ya kukosa uhakika wa soko! Hilo tu yani ndio maana kilimo watu wanaki bullshit!

Ila kungekuwa na maviwanda kama haya mengi ingepunguza sana tatizo la ajira!

Kweli kabisa mkuu. Fikiria unapeleka mbuzi 100 kama mdau anavyotupa hesabu za kwenye karatasi mbuzi mmoja unachezea faida ya 5,000/--6,000/- ina maana haukosi 500,000/- kwa kipindi cha wiki moja. Ukiwa na mtaji hapo kwa mwezi 2M. Licha ya changamoto na ngarambe za hapa na pale, kama uhakika wa soko upo, bora mtu ajibanze huko.

Sijamsikia mrangi atie neno bado.
 
Kweli kabisa mkuu. Fikiria unapeleka mbuzi 100 kama mdau anavyotupa hesabu za kwenye karatasi mbuzi mmoja unachezea faida ya 5,000/--6,000/- ina maana haukosi 500,000/- kwa kipindi cha wiki moja. Ukiwa na mtaji hapo kwa mwezi 2M. Licha ya changamoto na ngarambe za hapa na pale, kama uhakika wa soko upo, bora mtu ajibanze huko.

Sijamsikia mrangi atie neno bado.
Yeah huko unakomaa napo tu kila week unaingiza hela yako nzuri tu
 
Kweli kabisa mkuu. Fikiria unapeleka mbuzi 100 kama mdau anavyotupa hesabu za kwenye karatasi mbuzi mmoja unachezea faida ya 5,000/--6,000/- ina maana haukosi 500,000/- kwa kipindi cha wiki moja. Ukiwa na mtaji hapo kwa mwezi 2M. Licha ya changamoto na ngarambe za hapa na pale, kama uhakika wa soko upo, bora mtu ajibanze huko.

Sijamsikia mrangi atie neno bado.
Nafatilia mkuu,ntatia neno

Ova
 
Back
Top Bottom