Kama una mtoto/ndugu wa kiume mfundishe haya

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Mwanaume anasemwa kutokana na mafanikio yake.
Sio lazima kuwa Bakhresa.
Ila ni ile thamani anayoongeza kwenye jamii inayomzunguka. Mtu anayechota maji mtaani anathaminiwa kuliko mtu anayekesha kwenye vibanda vya kucheza gemu.
Hivyo ajitahidi aweze kipengele fulani cha maisha na akitumie kuimarisha jamii.

Aishi na wanawake kiakili.
Asitegemee pesa zake tu.
Wanawake wanazidi kukombolewa hivyo asitegemee kuwa pesa zake ndo kila kitu. Ni jambo zuri wanawake nao pia kujiweza kiuchumi. Lakini hili jambo limepelekea wanaume wengi kuwashindwa wanawake kwa kujiona wadogo. Na kuwaogopa wanawake.
Pia atambue ufanyaji wa maamuzi ni tofauti kati mwanaume na mwanamke. Mara nyingi wanawake hutumia hisia zao kufanya maamuzi.
Hivyo, asiyumbishwe na hisia tofauti tofauti za mwanamke kila muda.

Asitumie bangi au pombe kuficha udhaifu wake.
Kuwa na madhaifu si vibaya.
Pia mtu anaweza kutumia vilevi kujiliwaza.
Lakini akitumia kilevi kwa ajili ya kukwepa majukumu si jambo zuri. Nguvu ya wanaume inahitajika sana kujenga taifa, katika sekta tofauti kulingana na alivyojaaliwa na Mungu.

Asilalamike sana, au kuongelea maisha ya wengine mno.
Umbea aachie wanawake.
Kulalamika maana yake ni kuchagua kukwepa kutatua changamoto. Kulalamika haipendezi. Kuongelea maisha ya mwingine maana yake ni kusimamisha ujenzi wa maisha yako.

Ajiamini.
Asiruhusu tatizo lolote kumrudisha nyuma.
Kama mwanaume ameumbwa kutatua changamoto. Lakini ili azitatue ni muhimu ajiamini kuwa anaweza.

Asijiwekee visingizio vingi. Mfano, mpaka niwe tajiri ndo nimtongoze mwanamke ninayemtaka. Au mpaka niweze kuhitimu chuo ndo nianze biashara zangu.
Pia ajiamini kuongea na kufanya akitakacho. Asijifiche fiche kuwa vile atakavyo ili mradi havunji haki za wengine.

Achague marafiki vizuri.
Marafiki zake ndio lebo yake ya mafanikio. Kama watu hatuwezi ishi bila marafiki hivyo ni muhimu kuchagua marafiki vizuri. Sio kujiachia na kukubali kila mtu atakayekuja maishani mwake.

Awe na msimamo.
Asiyumbishwe katika msimamo wake.
Hasa kwa mwanamke wake.
Endapo mtu hatoweza kuishi kulingana na misimamo yake asimlazimishe bali amuache na kuruhusu watu wapya watakaoendana naye.

Kurudia kosa ndio kosa.
Makosa yapo.
Hasa pale tunapofanya kitu tofauti na tulivyozoea au ukiwa kwenye hatua nyingine ya maisha. Hakuna asiyekosea. Cha muhimu ni Kujifunza alipokosea na ajifunze afanye nini ili asirudie kosa.
Asijilaumu sana na kujiona hafai.
Bali aone kukosea ni kama hatua muhimu ya kujifunza.

Njia pekee ya kuepuka makosa ni kutofanya chochote cha kukupa changamoto. Kubweteka. Na akiishi hivyo hatosonga mbele kimaisha atadumaa sehemu aliyopo.
Uzuri wa maisha ni kwamba huleta kosa hilo hilo mpaka ujifunze na kubadilika.

Ni muhimu asiache kujifunza. Mtu yoyote anaweza kumpa somo muda wowote katika maisha yake. Hivyo asing'ang'anie tu kile akijuacho kwamba ndo inabidi iwe ivo milele. Pia aamini anaweza badilisha maisha yake muda wowote atakao.

Na asidharau watu.

Share Na Wengine Wapate Kujifunza.
 
umeliweka vizuri sana, katikati ya somo lako nilisita kwenye misimamo na kusema nitakueleza kuwa sio misimamo yote ni chanya na ikiwa hasi akubali kujifunza. Lakini hapo aya ya mwisho uliliweka vizuri sana kuwa asiache kujifunza ikiwa pamoja na misimamo yake.

barikiwa sana tumekuelewa.
 
Asante.
 
Back
Top Bottom