Kama una pesa, wekeza kwenye viwanja

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Jana nilipewa kazi ya kumtafutia kiwanja mdau wangu wa damu sana, nikashuka kisemvule nikaingia mpera ndani ndani huko.

Viwanja vipo vya mabondeni na tambarare,

Vipo vya milion 2 vipo vya 2.3, 2.5 kifupi vipo vya hela yote,

Pia nimeonyeshwa pagale ambazo zipo sokoni

Ila kuna hiki ambacho kimenifanya niandike hapa ni kuwa kuna heka pia zinauzwa zipo kidogo mbali na mji lakin kwa dunia ya sasa hakuna sehemu mbali maana kila sehemu mchina kafika na boda boda zake,

Ukitoka kisembule stand hadi maeneo ya tulio nauli ni 1500 laki kwa kuwa boda boda huku ni nyingi kuliko idadi ya wakazi hata kwa 1000 unafika.

Huku aisee wanauza heka moja Tsh. 22,000,000

Nikauliza kwa nini pesa nyingi hiii, nikajibiwa hiyo pesa kwa wawekezaji inawalipa kwa kuwa wao wanachukua heka nyingi nyingi then wanafanya biashara, yaani wanakata viwanja katika heka moja ni viwanja 20 kwa hiyo hata akiamua kuuza kwa 1.5 x 20 = bado anapata mil 8 kama faida ndani ya muda mchache na hapo kauza vunja bei ila bei halisi ni 1.6 hadi 1.7

Na pia akiamua aache kuuza baada ya mwaka ile hela yake inaji double zaidi maana atauza kwa bei ndefu kwa kuwa tayari kutakuwa kumewaka.

Wito......

Kama uko vizuri halafu hutaki stress za kuwekeza hela sehemu huku unaongea peke yako barabarani, njoo twende ukachukue heka 5 then ukae pembeni baada ya miezi mingapi tukapige bei upate hela yako na ziada ambayo haina mlolongo mrefu.

Ni hayo tu

Nashukuru
 
Hebu rudi huku utoe ufafanuzi hii Tsh.22,000,000 kwa ekari moja imekaaje!!??
 
Hebu rudi huku utoe ufafanuzi hii Tsh.22,000,000 kwa ekari moja imekaaje!!??
@Mchanya hekari moja inatoa viwanja 20 kwa vipimo kwa kiwanja futi 40 kwa 50
 
@mdukuzi ukiendelea kuona kila kitu ni scam utachelewa sana mzeee ,utazunguka na vyeti kama mwenda wazimu.
Kama ana hayo mamilionj ya hiyo heka moja unafkiri atazunguka na bahasha?
Nafkiri sisi wa hali ya chini ni kununua za hiyo milion 2 2
 
Eka moja inatoa viwanja 9 (minimum) vya mita 20 X 20 zikiwa na barabara zake

Mimi pesa sina ila hili wazo nina uzoefu nalo muda mrefu (kwa Kigamboni)
Kama kuna mtu una pesa tunaweza andaa mikataba ya kisheria Mimi Na Ww, suala la wateja na kugawa viwanja ukaniachia mimi

Tunakubaliana Muda Tu Wa Pesa Yako kuingia Kwenye Akaunti Yako ,Kwani Nina uzoefu wa kusimamia vizuri, Ukarudisha Faida ya haraka

Kwa wanaowekeza kwenye nyumba za kupangisha, Nawashauri Waje huku kwenye viwanja, ni Bora mara mia zaidi
Hakuna stress za wapangaji wala ukarabati

Karibuni Tushauriane nipo Kigamboni, Namba zangu hizi 0718295182 /0765505909
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…