Kama una shamba limekaa tu, panda Miti ya Mulberries, ina zero cost za utunzaji

Kama una shamba limekaa tu, panda Miti ya Mulberries, ina zero cost za utunzaji

Kwa kinyakyusa tunaita Mang'ang'a, Yamenikumbusha mbali nilikula fimbo nyingi mno sababu ya hayo matundašŸ˜€ nilipewa kazi home nikaiacha nikaenda na friends kula hayo matunda wee kurudi home ni fimbo zisizo na idadišŸ˜€
 
Kwa kinyakyusa tunaita Mang'ang'a, Yamenikumbusha mbali nilikula fimbo nyingi mno sababu ya hayo matunda[emoji3] nilipewa kazi home nikaiacha nikaenda na friends kula hayo matunda wee kurudi home ni fimbo zisizo na idadi[emoji3]
Nimesubiri sana kuona komenti inayoyataja hayo kama "maang'ang'a". Ila sasa haya meusi sio matamu sana kama yale ya chini chini ni mekundu hivi kwa rangi....afu kuna yale maan'gang'a yana rangi ya orange.....yani yale ndo yana balaa kwa utamu.
Haya meusi hayanipagi vibe kabisa yn
 
Nimesubiri sana kuona komenti inayoyataja hayo kama "maang'ang'a". Ila sasa haya meusi sio matamu sana kama yale ya chini chini ni mekundu hivi kwa rangi....afu kuna yale maan'gang'a yana rangi ya orange.....yani yale ndo yana balaa kwa utamu.
Haya meusi hayanipagi vibe kabisa yn
Unayajua mang'ang'a aina zote mkuu, yale ya njano ni balaa ni matamu kama soda hivišŸ˜‹
 
Yani yale ya njano ni yana balaa zito....basi yale unachuma kamoja kamoja then yakishajaa kiganjani yatupie mdomoni.....ndugu yangu acha tu. Ni nouma.
Au uyaweke kwenye chupa hivi afu unapondonda ukinywa kama soda kweli aiseešŸ˜€šŸ˜‹ those moments, ila siku hizi sijui yamepotea mbona siyaoni kijijini kwetušŸ™†ā€ā™‚ļø
 
Mulberries matunda yake hakuna hata mmoja humu anaye weza pinga kwamba sio matunda matamu, Mulberries binafisi nikikutana nayo popote pale lazima niyachume nile.

Haya matunda ambayo nahisi asili yake yaliletwa na wakoloni ni matunda comercialy nchi zingine hasa Asia huko.

Haya matunda sidhani kama yana gharama na kama zitakuwepo basi ni over minimal sana.

Unaweza fanyaje?

Kama unashamba liko sehemu nzuri otesha miti ya kutosha make unakata tu vijiti unapandikiza au unaotesha kwanza kwenye viriba then unahamishia aridhini.Ukisha anza kupata matunda chuma paki kwenye kontena kama za kupakia zabibu au strawberry na nenda nazo kwenye High end super Market na kwenye juice Bar.

Pale unawaachia sample hata pakiti 10 za kutest,kwanza tukubaliane hakuna asie jua Mulberries kuanzia wazungu, wahindi, na sisi Wabongo. Watu watanunua tu labda washindwe bei.

Peleka kwenye Fruits Bar ziko mingi sana achia wao sample kadhaa free kabisa, nina uhakika utauza na itahitajika mzigo mkubwa sana utafikia wakati ushandwa.

Mulberries ni matunda matamu kuliko idadi nyingi ya haya matunda ya kugeni, bado mimi hata Zabibu hazifuati kwa Mulberries fruits.

Haya matunda yanaweza kuwa ni biashara sema sasa kwa sababu hatujaona anaye lima, na wala hatujayaona yakiuzwa pembeni ya barabara tunaamini hakuna soko, sisi soko ni hadi tuone yakiuzwa hadi pembezoni mwa Barabara.

Kuna products zina soko ila hutakaaa uone wala kusikia zinauliziwa na mtu kwa sababu hazipo sokoni, so mtu hawezi jisumbua kuulizia kitu ambacho hakipo sokoni.Ila siku akikiona lazima atakitaka kwa sababu anakijua au alisha wahi kukila kipindi fulani kwenye maisha yake.

Mfano: Mchaga akienda labda Canada,hawezi jisumbua kuulizia mbege au mtori, kwa sababu anajua hakuna chakuka cha aina hio kule Canada,Ila siku ya siku anapiga zake misele akakutana na Mbege au Mtori atautaka kwa sababu ilikuwa ni moja ya chakula alisha wahi kukila kwenye maisha yake.
View attachment 2835965View attachment 2835966View attachment 2835967
Nina shamba liko na ardhi mbovu in mawe na ni mwinuko,specification zikoje za ardhi Tena sehemu kuna nyani wa kutosha na nguruwe pori na wafugaji ng'ombe wapo pia
 
Nina shamba liko na ardhi mbovu in mawe na ni mwinuko,specification zikoje za ardhi Tena sehemu kuna nyani wa kutosha na nguruwe pori na wafugaji ng'ombe wapo pia
Haya matunda sio mageni, wewe angalia kama inafaa simika vijiti, unaweza kata vijiti ukaotesha iwanza kwenye vimfuko vya kuoteshea miche then ukahamisha shambani baadae.
 
Nimesubiri sana kuona komenti inayoyataja hayo kama "maang'ang'a". Ila sasa haya meusi sio matamu sana kama yale ya chini chini ni mekundu hivi kwa rangi....afu kuna yale maan'gang'a yana rangi ya orange.....yani yale ndo yana balaa kwa utamu.
Haya meusi hayanipagi vibe kabisa yn
picha yake mkuu,kama utapata
 
Watu wengi wameyakata na kujifanya wanaweka migomba ya matoki
Hiyo miti ina faida sana kwa mtu anayefuga kuku, sungura na mifugo mingine.

Kwanza kabisa wadudu wanaotoa nyuzi za hariri wanakula majani hayo tuu.

Pili majani yake yakianikwa kwenye kivuli yakakauka yakiwa ya kijani bado ukatwanga unachanganya na chakula cha kuku yana kiwango kikunwa cha protini.

Matunda ya mti huo yakianguka kama kuku wanapita wanakula nankuongeza vitamini

Mmea huo majani yake yanatengeneza chai. Fuatilia mitandaoni utajua. Inasaidia sana wajawazito. Tafiti zaidi utajua

Miti yake ni migumu inaweza kutengeneza viti vya kukalia vile. Vinavyochanganywa na ngozi.

Matunda yanaweza kukaushwa na kutengeneza vitu mbali mbali. Au kuweza kutumika kwenye mikate na keki.

Matunda yanaweza kutengeneza mvinyo, juice, crush, smoothie, etc

Majani yanaweza kuliwa na mbuzi na mifugo mbali mbali
Kabisa Mkuu, Pointi.
 
Back
Top Bottom