Kama una shamba limekaa tu, panda Miti ya Mulberries, ina zero cost za utunzaji

Kwa kinyakyusa tunaita Mang'ang'a, Yamenikumbusha mbali nilikula fimbo nyingi mno sababu ya hayo matunda😀 nilipewa kazi home nikaiacha nikaenda na friends kula hayo matunda wee kurudi home ni fimbo zisizo na idadi😀
 
Kwa kinyakyusa tunaita Mang'ang'a, Yamenikumbusha mbali nilikula fimbo nyingi mno sababu ya hayo matunda[emoji3] nilipewa kazi home nikaiacha nikaenda na friends kula hayo matunda wee kurudi home ni fimbo zisizo na idadi[emoji3]
Nimesubiri sana kuona komenti inayoyataja hayo kama "maang'ang'a". Ila sasa haya meusi sio matamu sana kama yale ya chini chini ni mekundu hivi kwa rangi....afu kuna yale maan'gang'a yana rangi ya orange.....yani yale ndo yana balaa kwa utamu.
Haya meusi hayanipagi vibe kabisa yn
 
Unayajua mang'ang'a aina zote mkuu, yale ya njano ni balaa ni matamu kama soda hivi😋
 
Yani yale ya njano ni yana balaa zito....basi yale unachuma kamoja kamoja then yakishajaa kiganjani yatupie mdomoni.....ndugu yangu acha tu. Ni nouma.
Au uyaweke kwenye chupa hivi afu unapondonda ukinywa kama soda kweli aisee😀😋 those moments, ila siku hizi sijui yamepotea mbona siyaoni kijijini kwetu🙆‍♂️
 
Nina shamba liko na ardhi mbovu in mawe na ni mwinuko,specification zikoje za ardhi Tena sehemu kuna nyani wa kutosha na nguruwe pori na wafugaji ng'ombe wapo pia
 
Nina shamba liko na ardhi mbovu in mawe na ni mwinuko,specification zikoje za ardhi Tena sehemu kuna nyani wa kutosha na nguruwe pori na wafugaji ng'ombe wapo pia
Haya matunda sio mageni, wewe angalia kama inafaa simika vijiti, unaweza kata vijiti ukaotesha iwanza kwenye vimfuko vya kuoteshea miche then ukahamisha shambani baadae.
 
picha yake mkuu,kama utapata
 
Watu wengi wameyakata na kujifanya wanaweka migomba ya matoki
Kabisa Mkuu, Pointi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…