Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Wana group wenzangu rehma na amani za muumba wetu ziwe mioyoni mwenu.

Najua wengi wenu mnafahamu tabia yangu. Japokuwa huwa si mtu wa kupost mara kwa mara kwa hili lililoanza kujitokeza nalazimika nilizuie kwa n guvu zangu zote.

Miongoni mwetu kuna mmoja ameanza tabia ya kunizushia mambo ambayo si tabia yangu na hakika hii hali ninaomba isiendelee la sivyo ninaweza kuchukua hatua stahiki hata kama kwenda kwenye vyombo vya sheria. Najua mnajua sheria za matumizi mabaya kwenye mtandao. Inanisikitisha sana na kwa kweli sikutegemea jambo hili la kunizulia lianzie kwenye group letu.

Kuna mwenzetu mmoja amesambaza taarifa eti mimi huwa sipendi kualikwa eti kwa sababu sili pilau, wali wa nazi, wali wa maji, ndizi nyama, nyama ya mbuzi, kuku na vinywaji vilipoa yaani baridiiii.

Naomba nikanushe taarifa hizo si za kweli mimi na familia yangu tupo tayari kupokea mualiko hata sasa hivi. Maana mpaka sasa hatujapata mualiko wowote sababu ya uzushi uliotolewa. Natumaini mmenielewa.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kuna aina mpya ya Pilau imegundulika
Inaitwa Pilau Makinikia Hili ni pilau lenye kiasi kidogo cha nyama, yaani nyama mpaka uzitafute saana
 
Pana mtu mzima mmoja tulikutana penye choo cha bar na alikuwa ameutwika mtungi kisawasawa anayumba tu baada ya kufungua zipu na kuutoa mpini akaanza kusema "bwana mdogo sio kila kazi unaweza kumtuma mtu akufanyie "nikawa sijamuelewa akaendelea kama hii huwezi mtuma mtu akakojoe kwa niaba yako.
 
Watu wagumu kutoa mwaliko[emoji115] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…