Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Mtoto alimuuliza babake:
MTOTO: Baba, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa. Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika akamfuta mamake)

MTOTO: Mama, eti sisi wanadamu tulikuja vipi duniani?

MAMA: Wanahistoria wamesema sisi tulitokana na nyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi kwa baba)

MTOTO: Baba mbona mama anasema sisi tulikuwa nyani mwanzo?Au wanidanganya?

BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao...[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…