Kama unafanya kazi ndani ya nchi yako, nyumba yako ya kwanza jenga huko unakofanyia kazi

Kama unafanya kazi ndani ya nchi yako, nyumba yako ya kwanza jenga huko unakofanyia kazi

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
625
Kama unataka kujenga (nyumba yako) nyumbani ulikozaliwa tofauti na unapofanya kazi kwa kutegemea usimamizi wa ndugu zako hakikisha una moyo wa uvumilivu.

Kumpa ndugu yako cheo cha usimamizi wa hela za ujenzi wa nyumba yako ni sawa na kumkabidhi mkeo/mumeo kwa Mngoni azunguke nae kwenye semina mbali mbali nchini (Samahani Wangoni).

Ushauri wa bure: Nyumba ya kwanza jenga huko unakofanyia kazi. Nyumba ya pili ndio unashauriwa kujenga ulikozaliwa hata ukipigwa hela au ikichelewa kwisha utavumilia. Wengi tumelizwa na hatukuweza kudai hela zilizotafunwa na ndugu zetu.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 
Wangoni tumekusikia na tupo hapa Bombambili tunakunywa ulanzi tunasema uswengile!!!
 
Nyumba ya kwanza jenga huko unakofanyia kazi. Nyumba ya pili ndio unashauriwa kujenga ulikozaliwa
Kama upo kwenye mfereji wa kizimkazi, u ajenga popote tu, hata angani au majinj, si unakabashi kandarasi, unapokea mjengo...nani wa kukwamisha hapo?

Kama ni mtanzania halisi mwenye kipato halali, 95% wanajenga nyumba kwa zaidi ya miaka 10, hivyo nyumba ya kwanza inaweza kuwa ya mwisho pia, sasa wapi pa kujenga;
  • Jenga pale kwenye base yako kubwa, ni wazi, utaishi hapo itakapolazimu.
  • Jenga pale utakapotaka kuishi utakapoamua kupumzika, kustaafu au mambo yakienda mrama.

Kama sio chawa, jichanganye uone!
 
Kama unataka kujenga (nyumba yako) nyumbani ulikozaliwa tofauti na unapofanya kazi kwa kutegemea usimamizi wa ndugu zako hakikisha una moyo wa uvumilivu.

Kumpa ndugu yako cheo cha usimamizi wa hela za ujenzi wa nyumba yako ni sawa na kumkabidhi mkeo/mumeo kwa Mngoni azunguke nae kwenye semina mbali mbali nchini (Samahani Wangoni).

Ushauri wa bure: Nyumba ya kwanza jenga huko unakofanyia kazi. Nyumba ya pili ndio unashauriwa kujenga ulikozaliwa hata ukipigwa hela au ikichelewa kwisha utavumilia. Wengi tumelizwa na hatukuweza kudai hela zilizotafunwa na ndugu zetu.

RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
Ushauri mzuri sana.
Moja ya member ninaowakubali humu ni wewe Right Marker na Nikifa MkeWangu Asiolewe yaani muda wote huwa mnashauri vyema
 
Back
Top Bottom