Kama unahangaika kuwapata watu wenye uhitaji ili upate baraka/twawabu basi fika vyuoni hasa vyuo vikuu vya serikali

Kama unahangaika kuwapata watu wenye uhitaji ili upate baraka/twawabu basi fika vyuoni hasa vyuo vikuu vya serikali

MAKANGEMBUZI

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2020
Posts
2,670
Reaction score
7,655
Naandika haya nikiwa jikoni kabisa.Nimelia sana kwa maneno ya wabunge wanaokula posho za bure kwa kugonga meza na kudharau wanazuoni.

Jamani kuna kundi kubwa sana la wanafunzi wa vyuo ndoto zao zinaisha njiani na kufa kabisa kwa sababu za ada,watu wanakosa malazi,watu wanapitia msoto mkali sana.

Ubaya wa chuo mifumo ndio inafanya kazi hujalipa ada unaambiwa postpone uje mwakani ukipata ada tofauti na secondary unaweza kwenda kumuomba hata mkuu wa shule akuvumilie.

Mikopo ya bodi ya mikopo ndugu zangu ni siasa tu watu wengi hawana mikopo. Ukiwa mtoto wa kiume ndio utakaza kibishi ila kwa watoto wa kike ndiyo mwanzo wa kuanza kudanga,na sio siri watoto wa kike wanabanduliwa kwelikweli.

Hakuna watu ambao wamejikuta na roho ngumu kwa matatizo ya wanafunzi kama head of departments. Tembelea ofisi za wakuu wa idara kipindi cha University Examinations (UE) utajionea mwenyewe.

Jamani muwakumbuke na wanavyuo wanahitaji sana support yenu, mmewasaidia elimu ya chini mnawatelekeza huku mwisho kitu ambacho kinakuwa ni sawa na kazi bure.

Achaneni na hawa wanasiasa na wajinga wengine wanaotafuta umaarufu tu ila field watoto wa wakulima au son of peasant kama bodi ya mikopo wanavyotuita cha moto tunakiona.
 
Mbona huyu jamaa Tlaatlaah amesema wanavyuo wanaishi kifahari sana?
Mnatuchanganya sasa.
zingatia engo ya hoja yangu na ya muungwana mtoa mto hoja 🐒

yeye yupo jikoni huko departments anaweza kuona mambo mengine na mimi niko huku mtaani naweza kushuhudia mengine 🐒
 
Wenye uhitaji ni wengi... maarifa na akili tulizopewa na Muumba Kama tutazitumia vyema basi hizi changamoto na Hali ya kuombaomba tutaepukana navyo

Vipi ukifika mahospitalini utasemaje?
Ukifika magerezani?
Ukifika vijijini?
Ukiona walemavu maisha yao?
Nk

Wewe Kama msomi unayesoma kwa pesa ya umma Kama mkopo hicho ulichoandika ndio suluhu? Ndio kinasadifu elimu yetu ilivyo? Elimu tegemezi? Elimu kuwa bado ni mzigo? Elimu ni omba omba?

Akimaliza hapo mtakuja kuomba ajira au kutumia maarifa uliyoyapata Kutatua changamoto katika jamii?

Au tuendelee kuwalaumu wagongameza bungeni na kuwabagua darasa la saba ata Kama wanamchango mkubwa katika jamii kuliko walio na elimu zaidi Yao?

Vilevile hao darasa la Saba bungeni inawezekana hawafiki ata 1% ila shida elimu hii huko mavyuoni inaonekana ni kuzalisha mabingwa wa lawama kuliko watatuzi wa changamoto
 
Hoj yako nini sijaielewa....uzi huu lawama zake zitaisha kama chama chako cha CCM kitotoa elimu bure vyuoni otherwise acheni siasa za majitaka.
 
Back
Top Bottom