Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari Wakuu!
Mambo yetu yanasikitisha mno. Yanahuzunisha Sana.
Tumezoea kulalamika.
Tumezoea kulaumu wengine huku Sisi tukifanya yaleyale.
Taikon sitaki kumlaumu yeyote. Siku zote nitakuwa msema ukweli hata Kama unaumiza.
Ukweli ndio dawa pekee ya kuikomboa nchi.
Hakunaga maendeleo pasipo kujitoa kafara!
Hakunaga Amani pasipo ncha ya Upanga.
Wananchi masikini tumekuwa tukilalamikia viongozi wetu kuwa wanaingia mikataba mibovu ya kinyonyaji isiyoinufaisha nchi. Lakini sisi nasi tunaingia mikataba hiyohiyo katika level zetu za maisha kuajiriwa na kupewa mishahara kidunchu.
Ukiona nchi au taifa lolote watu wake wanaogopa Kifo na wapo tayari kuuza utu na haki zao ili angalau waweze kuishi, taifa hilo kamwe haliwezi kuendelea Ng'oo. Taikon ndio nimeshasema baada ya kupeleleza Kwa muda mrefu.
Mtu atasema; Bora nifanye hiki kibarua ilimradi maisha yasonge hata Kama ananyonywa haki zake.
Viongozi wa nchi wataendelea kuingia katika mikataba ya kinyonyaji Kama vile wananchi wake tunavyoingia mikataba ya kinyonyaji katika vibarua vyetu.
Nchi inajengwa kuanzia ngazi ya familia.
Ikiwa familia nyingi watu wake wapo Radhi waingie mkataba wowote hata kama wakinyonyaji ili Familia zao zipate Kula unafikiri Kwa level ya kitaifa ambayo ni viongozi watafanya nini zaidi ya wao nao kuingia mkataba wowote ilimradi familia zao na kidogo nchi Yao ipate chochote.
Ikiwa Wafanyakazi wao kila siku ni kulalamika wanalipwa Mishahara midogo na wanashindwa kujitetea unafikiri wananchi haohao siku wakija kuwa viongozi wakawa wanalipwa angalau mishahara mikubwa watapigania haki za wananchi? Jibu ni hapana.
Kama mtu kashindwa kutetea haki zake iweje aweze kutetea haki za watu wengine?
Kama tunahitaji kuibadilisha jamii yetu itatupasa kila mmoja wetu aache Ubinafsi.
Jamii yetu imejawa na watu Wabinafsi kuanzia masikini Kabisa mpaka Tajiri Kule juu.
Nipumzike sasa!